Hivi mlianzaje biashara zenu, mbona wengine tunakwama?

Mtaji wa fedha na watu + ubabe unatoboa. Ukicheka na nyani utavuna mabua. Na bongo nyani ni wengi sana.
 
Ukiweza kubana matumizi na kuacha vitu visivyokuwa na umuhimu na biashara utaweza
 
Majibu mazuri yatakayotolewa hapa nadhani yatasaidia sana maana hii ni changamoto kwa vijana wengi miaka hii...
 
Mtaji wa fedha na watu + ubabe unatoboa. Ukicheka na nyani utavuna mabua. Na bongo nyani ni wengi sana.
[emoji23][emoji23] + ubabe umenikumbusha kitu kuna mwana hawez kunisahau maisha yake yote.
 
Kuanzisha Biashara ni kugumu sana hapa Tz, hasa kama hujawahi kuendesha biashara ni lazima mtaji wa kwanza upotee, ndo ukipata wa pili ndo utaanza kuelewa biashara
Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa, kuanzisha biashara ni sawa na mtu anayeanza kusoma darasa la kwanza. Sasa fikiria uanze kujifunza a, b, c, d.........na baadaye kuziunganisha herufi hizi ili kupata neno, na hatimaye uunganishe maneno ili upate sentensi!
Hivyo inahitaji muda kuyamaster maeneo hayo kabla hujahitinu shule! Vivyo hivyo katika biashara.....kuna hatua za kupitia mpaka kufikia kuielewa biashara. Utaanguka mara kadhaa lakini usikate tamaa, inuka na uendelee kujikongoja kusonga mbele.
Ukifika hatua za juu katika biashara yako......umeielewa, mtaji umekua, una network; panua biashara yako kwa kuweka projects tofauti tofauti (project portfolio). Hii itakusaidia ikitokea project moja ikifeli, basi zilizobaki zitaibeba ile iliyofeli (risk diversification). Mbinu hii inatumiwa sana na wafanyabiashara wakubwa. Usiweke nayai yote kwenye kapu moja, kwani hilo kapu likiponyoka na kuanguka, mayai yote yatapasuka, lakini ukiweka tofauti, mengine yatabaki!
 
"Mzigo unaisha na hela siioni"

Huoni kama hilo lilikuwa ni tatizo la kiuendeshaji badala ya kulaumu ugumu wa biashara? Maana kuuza uliuza ila pesa ndio ulishindwa kuitunza.
Biashara hizi zina changamoto nyingi sana ndugu yangu, ukiona watu wanafilisika usidhani ni wapumbavu.Mtu huwezi kufilisika kama stock ipo,unafilisika kwa sababu stock inaisha na pesa haionekani.

Na wala haihusiani na utunzaji wa fedha maana kama mimi pesa ya dukani nilikua hata siitumii kwa matumizi binafsi.

Waulize wafanyabiashara watakuambia,unauza siku nzima ikifika jioni unajikuta una elfu 10 zingine hazipo
 
Naelewa hiki unachokisema, mimi pia kwa namna moja ama nyingine nimewahi kuwa mhanga ndiomaana nikasema tatizo ni utunzaji wa fedha, ikiwa unaona fedha zinapotea katika mazingira yasiyoeleweka kwanini usitafute ufumbuzi wa hilo tatizo hadi unafikia kufirisika?

Maana yake baishara ni nzuri ila umesindwa kudhibiti huo upotevu wa fedha.
 

Aisee kumbe bado sijapoteza Wacha nikaze boot la jeje
 
Madini kama haya huwa tunaya-save kwenye notebook.
Baadae tunayapitia deeply.
Mkuu umeongea kitu kikubwa sana hapa.
 
Tuliaanza kwa kukwama kama wewe tulianguka na kupoteza mitaji mara nyingi sana lakini tulivumilia
Yes Kuna kipindi hata pesa ya marejesho tuliuza assets tulizopata lakini tukasimama Tena[emoji123]
 
Mstaafu simshauri pesa yake ya kiinua mgongo awekeze kwenye biashara kwa sababu hana uzoefu nayo

Kimbilio lao ni kujenga nyumba za wapangaji hasa hawa wa majiji makubwa kama Dar. Kama ana eneo zuri zaidi lenye pililapilika ajenge fremu za biashara za kupangisha
 
NAKAZIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…