Hivi mliojenga hapa mjini, mliwezaje? Mna miujiza ama ni wezi?

Hivi mliojenga hapa mjini, mliwezaje? Mna miujiza ama ni wezi?

Kujenga kunahitaji nia, nidhamu na kufunga mkonda, matumizi yako yawe yale muhimu tu, uachane na matako ya kina Sepetunga, na kujifanya kibopa kununulia watu mabia, unakomaa na hakikisha kila kifaa unanunua mwenyewe, unabana kila angle, hiyo kwa sisi wengine tuliojenga kwa vipato halali na tulio nyanyasika katika nyumba za kupanga.
 
Mbinu zinazotumika ni mchanganyiko sana, mbinu inayoongoza ni wizi( haijalishi aina ya wizi, ili mradi ulipata kiharamu), bonus ( usijali aina ya bonus, cha msingi ni bonus baada ya kusota), kudunduliza ( hapa utakuta nyumba moja imejengwa na mafundi kumi), mkopo ( toka benki, ofisini,jamaa, vikundi nk), kutunukiwa( zawadi toka ofisini, mshikaji, zali, bahati nasibu), urithi, kuokota nyumba.
Umesahau Maji ya Upako kwa Mwamposa
 
Kila kitu hapa mjini kinahitaji hela, unawezaje kusevu hela mpaka ufike hatua ya kujenga?

Na ukichukuwa mkopo benki ndiyo hatari zaidi. Kama ni mkopo wa kutegemea mshahara utakuta unakuwa mteja wa kausha damu, na kama ni biashara utaona inakufa mbele ya macho yako.

Mjini mambo yote yanahitaji fedha. Unawezaje kujenga ???

Bado kuna michango ya harusi, kitchen party, birthday party, misiba, na mitoko ya weekends, bila kusahau kusaidia ndugu na jamaa wa vijijini.

Naomba mbinu mlizotumia. Na muwe wakweli.
Wapi ambako unaweza kujenga bila pesa mkuu ili nikajenge hata gesti tu
 
Maisha ni vita mpaka kaburini hivyo inatakiwa uipambanie vita hiyo ni pamoja na ujenzi sio rahisi kama unavyonifikiria watu wanacheza michezo ya hatari mpaka kuhatarisha maisha Yao ila ni Siri ya mtu moyoni
 
Back
Top Bottom