Hivi mnaelewa kweli kinachoendelea siku hizi kwenye migogoro ya ndoa? Talk is so easy

Joined
Aug 26, 2015
Posts
32
Reaction score
120

Hivi mnaelewa kweli kinachoendelea siku hizi kwenye migogoro ya ndoa? Talk is so easy.​

Kuna jambo ambalo nimekuwa nikilitafakari sana. Mimi siungi mkono kuumizana kwa hali yoyote ile. Mtu akimdhuru mwenzake, hasa kwa kiwango cha kuchukua uhai, hakuna sababu ya kuhalalisha jambo hilo.

Lakini pia tusifanye kosa la pili: kumhukumu mtu kwa kusikiliza upande mmoja tu.

Siku hizi mtu akisema ameumizwa, akalia kidogo, akasimulia upande wake na watu wakaguswa kihisia, tayari jamii inamwekea mwingine lebo ya kuwa ndiye mwenye makosa. Wakati mwingine hata kabla ya kujua kilichokuwa kinaendelea ndani ya hiyo familia.

Na niseme wazi: sizungumzii wanawake wote. Lakini kuna baadhi ya wanawake siku hizi wamekuwa “wasanii mno” kwenye migogoro ya ndoa. Wanajua nini cha kusema, kwa nani wa kusema, wakati gani wa kusema na namna gani ya kujenga picha kwamba wao ndiyo waathirika pekee.

Tatizo ni kwamba jamii yetu mara nyingi inasikiliza anayelalamika kwanza kuliko anayelalamikiwa.

Maisha ya ndoa hayako kwenye picha za WhatsApp​

Ukiangalia picha ya wanandoa wakitabasamu, ukawaona wamekumbatiana au wamepiga picha nzuri pamoja, unaweza kudhani kila kitu kiko sawa.

Lakini ukweli ni kwamba kamera haikai ndani ya chumba cha ndoa.

Haioni maneno yanayosemwa usiku.
Haioni ugomvi wa mali.
Haioni mashaka.
Haioni wivu.
Haioni namna ndugu wanavyoingilia.
Haioni mtu anayefungiwa nje ya nyumba.
Haioni mtu anayelia peke yake.

Ndiyo maana ninapowaona watu wanatoa hukumu nzito kutokana na simulizi moja tu, huwa najiuliza: Tumesikia upande wa pili?

Mimi mwenyewe nimewahi kupitia hali kama hii​

Mke wangu alikuwa na changamoto kwenye suala la usafi wa nyumbani. Kuna wakati angeacha shuka kitandani wiki mbili bila kutandikwa wala kuondolewa. Siku moja alisafiri. Akaondoka kwenda kuwaona wazazi wake na baada ya takribani wiki tatu akarudi. Wakati huo nilikuwa nimebaki na mtoto wetu na nilikuwa nalala naye kitandani. Siku ya kurudi akanisingizia kwamba nilikuwa nimelala na dada wa usafi (baada ya kuona shuka chafu).Huyo dada wa usafi akafukuzwa na hata akapigwa. Ugomvi ukawa mkubwa, kuepesha shali siku hiyo nilitoka baada ya kuona anakosa adabu kama mke (hakunipikia chai asubuhi,chakula cha mchana hakupika kisingizio eti nimelala na dada baada ya kukuta shuka chafu sijui aliona nini ) siku hiyo nakumbuka nilirudi usiku baada kugonga hodi hakufungua.alinifungia nje ya nyumba na akanipigia "ndulu" kwa kushirikiana na rafiki zake na polisi wahuni tena saana siku hizi nikalazwa ndani. Kisa akaondoka na kwenda kwao, akiwa ameshaaminsha watu eti kwamba amenifumania na nilitishia kumpiga ndio maana alinifungia nje mpaka leo hajarudi.

Sasa mtu wa nje akisikiliza upande wake tu, anaweza kujenga picha yake mwenyewe na kunihukumu.

Lakini je, amesikia upande wangu?

Hapo ndipo ninaposema: tusikimbilie hukumu.

Ndugu na wazazi nao wakati mwingine wanaongeza tatizo​

Kuna wakati ndugu wanaingia kwenye migogoro ya wanandoa bila kujua historia nzima.

Mmoja anapiga simu kwao na kusema, “Nimefanyiwa hivi…”

Wao wanaamini.

Kesho mwingine anasimulia upande wake, nao tayari wanaona ni mtu wa kulaaniwa.

Badala ya kutafuta suluhisho, kila upande unaanza kutafuta watu wa kuwapa support.

Mwisho wa siku, tatizo la watu wawili linakuwa ugomvi wa familia mbili.

Na viongozi wa dini? Hapa pia tunahitaji kusema ukweli​

Zamani, viongozi wa dini walikuwa na nafasi kubwa sana katika kusuluhisha migogoro ya familia.

Mchungaji, padre, kasisi au kiongozi wa kanisa angeweza kufuatilia familia, kuwasikiliza wanandoa, kwenda nyumbani na kujaribu kuzuia jambo lisifikie hatua mbaya.

Lakini siku hizi, kwa baadhi yao, mambo yamebadilika.

Sadaka, michango, matoleo na shukrani vinafuatiliwa kwa bidii sana.

Ukipunguza mchango, wanakukumbuka.

Ukipata jambo la kushukuru, wanakukumbuka.

Lakini ukisikia familia inaelekea kuvunjika?

Kimya.

Nilishawahi kwenda kwa padre wa St. Joseph nikamweleza issue yangu. Nilitegemea angesikiliza pande zote na kutusaidia.

Badala yake nikasikia maneno ya aina hii:

“Hata mimi nina mdogo wangu ana matatizo na mke wake. Sisi siku hizi hatuingilii mambo hayo.”
Nikajiuliza: Kama hamuwezi kusaidia watu kuimarisha familia zao, basi mnaingia kwenye maisha yao kwa kazi gani?

Kama kweli hamtaki kuingilia migogoro ya familia, basi msiingilie pia kwa kuchukua upande bila kujua ukweli.

Familia ikivunjika, mnaachia serikali ifanye maamuzi. Lakini kabla haijavunjika, msaada wenu uko wapi?

Na cha kushangaza, wakati mwingine watu wakishatengana, bado kanisa linaweza kuwafuatilia kwa sadaka, shukrani na michango, lakini linapokuja suala la kuwasaidia kabla hawajafika huko, unaambiwa, “Hayo ni mambo yao binafsi.”

Hii nayo tunahitaji kuitafakari.

Tatizo si kwamba kila anayelalamika ni muongo​

Tusije tukakoseana hapa.

Kuna wanawake wanaoumizwa kweli. Kuna wanaume wanaoumizwa kweli. Kuna watu wanaoteseka kwenye ndoa na hawapati msaada wowote.

Lakini pia kuna watu wanaoweza kuwasilisha upande wao kwa namna ambayo inamfanya mwingine aonekane monster kabisa.

Ndiyo maana tunahitaji kusikiliza pande zote mbili kabla ya kutoa hukumu.

Mtu akisema, “Mume wangu amenifanyia hivi,” tusikimbilie kusema, “Mwanaume huyo ni mbaya.”

Na mwanaume akisema, “Mke wangu amenifanyia hivi,” tusikimbilie kusema, “Huyo mwanamke ni mchawi.”

Kaa chini. Sikiliza wote.

Kwa sababu huenda ukweli ukawa katikati.

Na hili la “kuanza upya” nalo tulitumie kwa akili​

Watu wanapenda sana kusema:

“Kama hamuelewani, kila mtu aanze upya.”
Ni rahisi kusema hivyo ukiwa nje.

Lakini ndoa si kama kubadilisha simu.

Kuna watoto.
Kuna mali.
Kuna historia.
Kuna miaka ya kujenga.
Kuna familia mbili.
Kuna hisia.
Kuna mambo ambayo watu wa nje hawajui.

Ndiyo maana siungi mkono mtu kuvumilia unyanyasaji au hatari, lakini pia siungi mkono watu wa nje kuharakisha kuvunja familia kwa ushauri wa dakika tano bila kujua kinachoendelea.

Na zaidi ya yote, hakuna ugomvi unaompa mtu ruhusa ya kumuua au kumdhuru mwenzake.

Kifo kikitokea, tumepoteza maisha ambayo hayatarudi.

Lakini kabla hatujafika huko, jamii, ndugu, wazazi na viongozi wa dini wanapaswa kujiuliza:

Tulikuwa wapi wakati hawa watu walikuwa bado wanahitaji msaada?

Kwa sababu wakati mwingine si kwamba watu hawakutaka kuongea.

Walizungumza.

Tatizo ni kwamba hakukuwa na aliyesikiliza pande zote mbili.
 
jamii inatakiwa kubadilika na kuendana na wakati wasasa, kuna vitu lazima vitazamwe upya,
 
Taasisi ya Ndoa inatakiwa ifanyiwe maboresho, ili kuendana na wakati wa sasa, vinginevyo, Vilio ni endelevu.
 
Ukizingatia kwenye jamii yetu hatuna mifumo ya kuwafundisha vijana kuja kuwa wazazi bora wa baadae, hali itazidi kuwa mbaya jando na unyago hatutaki,wazazi ndio hivyo wabinafsi ndio maana talaka kila siku, jamii imepagawa kila mtu kimpango wake.Utu hamna fedha ndio imepewa thamani.
 
Ivi mashahidi kwenye kiapo cha ndoa jukumu lao ni lipiii?
 
Pole sana Mkuu, tusichoke kuwakumbusha vijana wetu suala la KATAA NDOA, NDOA NI UTAPELI, japo wana vichwa vigumu sana....
 
Umesema ukweli wote mkuu.
Mke anakuaga anakwenda masomoni unamruhusu. Kwa miaka yote mitatu likizo kwao wazazi hawamuulizi. Hapo Kuna mharibogu wa ndoa kama mzazi?
 
Uisilamu uko powa sana mkishindwana mnaachana au ukiona ana kiburi unamletea mwenzake aje amfundishe
 
Kweka na Urassa wamekuwa mjadala mkubwa sana!
 
Back
Top Bottom