Hivi mnaielewa hii hukumu ya rufaa ya kesi ya Bernard Membe dhidi ya Cyprian Musiba?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Nimekutana na hii taarifa ya maamuzi ya rufaa ya kesi ya Bernard Membe dhidi ya Cyprian Musiba.

Kwanza ikumbukwe kesi ilipokuwa inasikilizwa Mahakama Kuu, upande wa washitakiwa, yaani upande wa Musiba, hawakutokea Mahakamani kwa hiyo kesi ilisikilizwa upande mmoja na mdai yaani Membe kupewa ushindi wa fidia ya shilingi bilioni 6.

Baada ya hukumu hiyo, upande wa washitakiwa wakakata rufaa. Kiufupi, Mahakama ya Rufaa imekubali maelezo ya upande wa utetezi, yaani upande wa Musiba uliodai kuwa mashahidi watatu wa Membe, akiwemo Membe mwenyewe, hawakutoa viapo kabla hawajatoa ushahidi wao. Kwa hivyo, Mahakama imeamuru kesi hiyo irudi Mahakama Kuu na ianze kusikilizwa upya kuanzia hatua ya kutoa ushahidi.

Najiuliza kushindwa kutoa kiapo ni kosa la nani? Majaji wa Mahakama Kuu waliruhusu vipi ushahidi utolewe bila kiapo cha mashahidi kutolewa? Pia Mawakili wa Membe wanasema viapo vyenyewe vilitolewa na vipo katika kumbukumbu ya Mahakama.

Je, inawezekana kumbukumbu ya Mahakama imechakachuliwa ili kuwapa washitakiwa nafasi ya kuanza kesi upya wakijua Mdai kwa sasa ni Marehemu?

Embu tuelimishane kidogo hapa.
 
Hizo ni technicalities, na ndizo zinazoshinda kesi. Unaweza ukawa na haki, lakini ukashindwa kwenye technicalities.

Asilimia kubwa, hawajala kiapo, kama walikula kiapo basi watakuwa na ushahidi wa stenographer. Kama ni affidavits unakuwa na copies zako za affidavit.

Kwa nchi zingine, proceedings zote ukipata hukumu unaruhusiwa kuomba copies zote, za records zote.
 
Nimekutana na hii taarifa ya maamuzi ya rufaa ya kesi ya Bernard Membe dhidi ya Elvis Musiba.

Kwanza ikumbukwe kesi ilipokuwa inasikilizwa Mahakama Kuu, upande wa washitakiwa, yaani upande wa Musiba, hawakutokea Mahakamani kwa hiyo kesi ilisikilizwa upande mmoja na mshitakiwa yaani Membe kupewa ushindi wa fidia ya shilingi bilioni 6.

Baada ya hukumu hiyo, upande wa washitakiwa wakakata rufaa. Kiufupi, Mahakama ya Rufaa imekubali maelezo ya upande wa utetezi, yaani upande wa Musiba uliodai kuwa mashahidi watatu wa Membe, akiwemo Membe mwenyewe, hawakutoa viapo kabla hawajatoa ushahidi wao. Kwa hivyo, Mahakama imeamuru kesi hiyo irudi Mahakama Kuu na ianze kusikilizwa upya kuanzia hatua ya kutoa ushahidi.

Najiuliza kushindwa kutoa kiapo ni kosa la nani? Majaji wa Mahakama Kuu waliruhusu vipi ushahidi utolewe bila kiapo cha mashahidi kutolewa? Pia Mawakili wa Membe wanasema viapo vyenyewe vilitolewa na vipo katika kumbukumbu ya Mahakama.

Je, inawezekana kumbukumbu ya Mahakama imechakachuliwa ili kuwapa washitakiwa nafasi ya kuanza kesi upya wakijua Mdai kwa sasa ni Marehemu?

Embu tuelimishane kidogo hapa.
Badilisha kwanza jina la huyo jamaa kutoka Elvis Musiba, na kuwa Cyprian Musiba, kwa ajili ya kuweka sawa kumbukumbu! Ok?
 
Hizo ni technicalities, na ndizo zinazoshinda kesi. Unaweza ukawa na haki, lakini ukashindwa kwenye technicalities.
Asilimia kubwa, hawajala kiapo, kama walikula kiapo basi watakuwa na ushahidi wa stenographer. Kama ni affidavits unakuwa na copies zako za affidavit.
Kwa nchi zingine, proceedings zote ukipata hukumu unaruhusiwa kuomba copies zote, za records zote.
Pia Mawakili wa Membe wanasema viapo vyenyewe vilitolewa na vipo katika kumbukumbu ya Mahakama.

Hizo ni techinicalities za Tanzania? Inasikitisha
 
Tanzania hatuna stenographer. Sheria inasema atakuwepo ila jaji mkuu hajawahi kuwatangaza au kuweka kanuni zake.

Kukosekana kwa stenographer imekua mwiba sana hasa kama hakimu anakua anataka kukupoteza, unaongea hivi yeye anaandika vingine. Ukishindwa kesi kwenye rufaa wanasoma tu kumbukumbu na inaonekana uliongea mwenyewe vitu vinavyosababisha ushindwe kesi.

Jaji Mkuu wa sasa tutamkumbusha umuhimu wa kuwa na stenographer.
 
Nimekutana na hii taarifa ya maamuzi ya rufaa ya kesi ya Bernard Membe dhidi ya Elvis Musiba.
Rekebisha kwanza jina, sio Elvis Musiba, Musiba huyu ni lile jinga lenye jina la Musiba, ambaye ni mwandishi wa habari kilaza fulani hivi, kanjanja na pia ni kichaa kabisa, ila haokoti makopo! Kichaa mmoja, anaweweseka sana juu ya Zitto, kamtungia uongo, umebuma, Zitto tuko nae hapa Dodoma,

Elvis ni yule alikuwa mwandishi wa vitabu, Kufa na Kupona, Njama, Kikosi cha Kisasi etc.

Ila masikini Membe, nilimshauri kitu Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

P
 
Tamaa Mbele nyuma giza
 
Mods Cookie nisaidieni kurekebisha kichwa cha habari kwa kubadili jina Elvis Musiba kuwa Cyprian Musiba.
 
Pia Mawakili wa Membe wanasema viapo vyenyewe vilitolewa na vipo katika kumbukumbu ya Mahakama.

Hizo ni techinicalities za Tanzania? Inasikitisha
Inasikitisha na kutisha kwamba Mahakama inaweza kuchezewa kiasi hiki.
 
Hizo ni technicalities, na ndizo zinazoshinda kesi. Unaweza ukawa na haki, lakini ukashindwa kwenye technicalities.
Asilimia kubwa, hawajala kiapo, kama walikula kiapo basi watakuwa na ushahidi wa stenographer. Kama ni affidavits unakuwa na copies zako za affidavit.
Kwa nchi zingine, proceedings zote ukipata hukumu unaruhusiwa kuomba copies zote, za records zote.

Pia Mawakili wa Membe wanasema viapo vyenyewe vilitolewa na vipo katika kumbukumbu ya Mahakama.

Hizo ni techinicalities za Tanzania? Inasikitisha

Kama vipo si vingeonyeshwa? Au hakuna rekodi za mashtaka?
Makosa ya technicalities inabidi yawe uliyofanya wewe ila hili la kiapo mbona kama ni kosa la Mahakama yenyewe kama kweli limefanyika? Inakuwaje Majaji wakaendelea kusikiliza ushahidi kama Mashahidi hawakutoa kiapo?
 
Tanzania hatuna stenographer. Sheria inasema atakuwepo ila jaji mkuu hajawahi kuwatangaza au kuweka kanuni zake.

Kukosekana kwa stenographer imekua mwiba sana hasa kama hakimu anakua anataka kukupoteza, unaongea hivi yeye anaandika vingine. Ukishindwa kesi kwenye rufaa wanasoma tu kumbukumbu na inaonekana uliongea mwenyewe vitu vinavyosababisha ushindwe kesi.

Jaji Mkuu wa sasa tutamkumbusha umuhimu wa kuwa na stenographer.
Uko sahihi kabisa. Inatisha mbinu zinazotumika Mahakamani kupindisha haki za watu.

Yaani mtu hata Mahakamani hakutokea kujitetea, halafu anasubiri hukumu anakuja kusema mashahidi hawakutoa viapo kabla ya kutoa ushuhuda wao na Mahakama inakubaliana naye.
 
‘Actio personalis moritur cum’, meaning a personal right of action dies with the person.

Kesi ya madai ya damages kama defamation inatakiwa kuisha naturally pale plaintiff anapofariki.

Ni njaa tu za wanasheria wa Membe na kuchezea muda wa mahakama; hakuna tena kesi hapo.
Hukumu ya awali ilishatoka wakati akiwa hai. Sidhani na sina uhakika kama hiyo ina apply wakati wa rufaa.

Kitendo cha kurudisha kesi ianze kusikilizwa upya kwa njia za panya ni kujaribu kuhalalisha hicho ulichosema.
 
Back
Top Bottom