Mtu amehangaika kusoma tangu chekechea, akakaza buti mpaka Masters, akapata kazi yake, akajenga maisha yake, akaoa… halafu anaambiwa: “Tuachane, tugawane mali.”
Hivi mnajua maumivu ya mtu aliyepambana miaka yote kujenga maisha yake?
Mwingine alianza kuhangaika akiwa na miaka 15. Akatoka kijijini kwao, akaanza kuuza vitu vidogo, akapambana siku hadi siku. alivumilia kuchekwa ni mbahili, Polepole akafungua duka, akajenga biashara, akapata magari, viwanja na mali nyingine.
Halafu baada ya miaka yote hiyo anasikia tu: “Mali zigawanywe.”
Hivi mnajua inauma kiasi gani kuona mtu anataka sehemu ya kile ambacho hakushiriki kukijenga?
wapo waliopambana kwenye migodi miaka nenda rudi. Jua, vumbi, njaa, kukata tamaa na risk kila siku. Miaka inapita bila mafanikio. Ghafla mambo yakatiki akaanza kununua assets na maisha yakaanza kubadilika.
Lakini mtu ambaye hakuwahi kujua joto la mgodini, hakuwahi kujua mateso ya kutafuta madini wala kujibonda vidole, anapotokea wakati wa mwisho anasema: “Tugawane.”