Username 20
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 743
- 1,522
Naunga hoja mkono ,Tena ni mtesi na anahujumu haki za binadamu ( refer katazo la marekani askanyage kwao)Huyu ambae alimlaghai GSM kuwa Rais Magufuri anataka kujengewa nyumba,
Alietaka kupitisha biashara yake bandarini kwa kisingizio cha kusaidia meza na viti waalimu wa Dar
Huyu bwana ukimweka kwenye kundi la walafi wa madaraka na matumizi mabaya ya madaraka ni namba moja kwa Tanzania hivi sasa
Kwanini mnamhusisha na Uwaziri mkuu, huyu bwana hafai hata kuwa waziri kwenye wizara yoyote watu wataumia
Kabla na baada ya uchaguzi wa 2020 JPM mwenyewe alilijua hili na kama JPM angebahatika kumaliza mhura wake wa pili ndo kabisa tusingemsikia tena Paul Makonda kwenye siasa za Tanzania
Makonda alipochaguliwa kuwa Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, alifanya ziara karibu nchi nzima alikuwa akitoa amri na viyisho kama ndio Rais mwenyewe
Kubwa zaidi alinikuta mkoani Singida kikazi na hapo ndio nikafahamu kuwa kumbe alikuwa akiwataka wakurungezi wa halmashauri na manispaa wote kote alikopita wampatie Tsh mil. 10 kwa kitisho cha kuwa usipotoa hiyo pesa utafutwa kazi
Kwa mda huo kidogo tu aliodumu kama Katibu wa Itikadi na Uenezi watu walihaha mpaka Rais Samia kumtoa na kumhamisha kama RC Arusha
Huyu bwana hawafai na nina imani kubwa Rais Samia hawezi kurudia kufanya kosa tena
Yaani hadi "Kiongozi wa Maji Maji" Muuza Sembe naye yumo Mjengoni.Siyo yeye tu, bunge zima hilo halifai!
Awe mbunge, waziri, diwani, hata waziri mkuu, nafasi yoyote anatekeleza matakwa ya chama chake na si wananchi.Kwanini mnamhusisha na Uwaziri mkuu, huyu bwana hafai hata kuwa waziri kwenye wizara yoyote watu wataumia
Na baada ya hapo akateuliwa RC, vipi kuhusu aliyemteua, hajui hayo?Bashite namfahamu kwenye issue ya kumuuza Ben Saanane ,yeye ndiye aliyeinjinia utekaji wa Ben.
Bashite namfahamu kwenye kupigwa risasi Lissu.
Bashite namfahamu kwenye utekaji wa Roma.
Wote ni chama kimoja, unataka wamchague nani, nani anafaa zaidi ya mwingine, unadhani huyo anayefaa yuko kumtumikia nani?Useless country.. hii ndio maana sasa ya Kakistocracy Bashite kichwa boga Leo anapigiwa chapuo awe waziri mkuu,
Kija Yunus empty set(refer interview yake na Lissu)
Halafu mtu wa maana kama Tindu Lissu yupo Magereza..
we're living backwards Hadi najiuliza mfano tukiwa na wabunge timamu kama taifa tutapata hasara gani?why jesca magufuli?Mtu mweusi mjinga sana
Unaweza kulaumu unaemtaka ila still haibadilishi maana..Wote ni chama kimoja, unataka wamchague nani, nani anafaa zaidi ya mwingine, unadhani huyo anayefaa yuko kumtumikia nani?
Kuanzia spika, wakuu wa polisi, jeshi, majaji, maRC, DC, wakurugenzi, wote uteuzi unatoka kwa Rais, kulalamikia wateuliwa kuliko anayeteua ni matokeo ya kuongozwa na hisia kuliko logics.