Hivi mnaona ninachokiona au nyie ni vipofu?

Ukiwa na akili mbili ni rahisi kuwaza Kama Mtoa mada.

Dini zinaweza kuwa na kasoro Kwa sababu zimeundwa na wanadamu lakini kuongelea mambo ya Mungu Kwa namna ya kijinga ni upumbavu.

Kuna mambo ukiyafikiri Kwa akili hata ya mtoto unajua Mungu hashindwi kufufua wafu, ikiwa alituumba from Nothing from nowhere, sembuse kutoka mavumbini kuzimu?

Unapojadili ishu za Mungu itakupasa uwe na IMANI YA JUU
Unapojadili mambo ya Kisayansi itakupasa uwe na AKILI YA JUU
Unapojadili mambo ya Mapenzi itakupasa uwe na UPENDO WA JUU.
Unapojadili mambo ya Vita itakupasa uwe na Ujuzi wa kijeshi wa Hali ya juu.
Unapojadili mambo ya Afya itakupasa uwe tabibu wa ngazi za juu.

Sasa mtu huna Uelewa wowote wa mambo ya kiungu alafu unajadili vitu usivyovijua huo ni upumbavu.

Ni Sawa na jitu linalojadili mambo ya magonjwa huku halina ABC za Utabibu, halijui lolote.

Kama huna Imani kubwa huwezi elewa mambo ya kiungu, lazima uonekane mwendawazimu Kwa sababu huna ujualo.

Hata zamani wajinga walipoambiwa Kitu kinaweza Paa angani walikataa Kwa sababu ya ujinga wao, lakini wenye akili walishaona uwezekano huo. Vipi leo ndege, drone na balloon hatuvioni vikipaizwa juu na watu?

Siku zote wenye hekima hukaa kimya Kwa mambo wasioyajua, wakisubiri wakati kuamua.

Kuwa na mashaka na Jambo Fulani haikufanyi ukatae halipo, ni kwamba unataka uthibitisho, na wakati ndio hutoa uthibitisho siku zote.

Wahenga walisema, Mpumbavu husema moyoni mwake HAKUNA MUNGU.

Na Kama hujui kuna ufufuo/uwezekano WA kufufuka ni kwamba hutambui huwezi wa Mungu.
Jambo ambalo ni dogo sana Kwa mtu hata asiye na Imani lakini akawa na akili nzuri ya kufikiria.

Mtu mwenye elimu tuu ya jiografia, Fizikia au Biolojia anatambua Kwa urahisi hakuna lisilowezekana chini ya jua Kwa sababu yupo MUWEZA WA YOTE, Mungu mwenye Enzi, Mungu aishiye mahali pa juu Sana.
 
Halafu hata mimi huwa najiuliza kwanini ibilisi atupwe duniani kutusumbua??kwanini Mungu asimwadhibu huko huko mbinguni mpaka aletwe duniani kutusumbua hivi??Kwanini yeye asikae nae huko huko kama ni kumfunga amfunge huko huko mi nnaona kuna ukweli hapa duniani tunapigwa sana aisee.
 
😂😂 Ile kamba sio ya kitoto sijui wengine hawaoni nini!!
 
Dini ni bangi za watu.

Imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo ndilo TUMAINI kuu.
 
Unawezaje kuamini kufanya muujiza kwa imani?
Ati ukiwa na imani Kama chembe ya haradani unaweza kuuambia mlima ng'oka na ukajitupe baharini!
Kwa hiyo hapo waliposema kuhusu kung'oa milima kwa uelewa wako unafikiri ni mlima Kilimanjaro au milima ya uluguru,? 🤔Biblia ukiitafsiri kihivyo hutoielewa na hutoiamini
 
Kwenda mbali wewe mwandishi uchwara, sio lazima kila mtu aamini unavyo waza wewe. Shwaiiin
 
Kwa hiyo hapo waliposema kuhusu kung'oa milima kwa uelewa wako unafikiri ni mlima Kilimanjaro au milima ya uluguru,? 🤔Biblia ukiitafsiri kihivyo hutoielewa na hutoiamini
Hapana ni meno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…