Mayor of kingstown
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,898
- 4,156
Nianze kwa kusema nimeishi Arusha, Mwanza, Dar Moshi, na sasa hivi nipo Dodoma unaelekea Mwaka sasa nipo huku kwa sababu za kikazi.
HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua, mchana kuna jua kali sana na vumbi halafu jioni na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .
MAKAZI
Kwa sasa hivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabisa ,Sidhani hata kama wanatumia ramani kwenye kujenga maana wanajenga manyumba makubwa kama makubwa jinga halafu mabaya hayapakwi rangi wala kupigwa lipu yanaachwa hivyo hivyo na madirishani wakiweka mifuko ya cement, mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu. Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki
USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM au STK etc huku hakufai usafiri haueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .
MAJI
Kwa mara ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi. Kama huna kazi hapakufai, maji ya kunywa ni ununue bila hivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha.
KAZI
Dodoma ofisi nyingi zinahamia huku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar, Mwanza na Arusha huku utapauka dakika 2 baada ya kushuka stand
MWISHO
Nisipoona hata mvua hii miezi iliobaki hata kwa mganga nitaenda nihame ofisi.