Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Mbona leo tu nimempokea demu kutoka dodoma pisi kali sana kuliko hata wahapa au dodoma yawapi?
 
Nianze kwa kusema nimeishi Arusha, Mwanza, Dar Moshi, na sasa hivi nipo Dodoma unaelekea Mwaka sasa nipo huku kwa sababu za kikazi.

HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua, mchana kuna jua kali sana na vumbi halafu jioni na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .

MAKAZI
Kwa sasa hivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabisa ,Sidhani hata kama wanatumia ramani kwenye kujenga maana wanajenga manyumba makubwa kama makubwa jinga halafu mabaya hayapakwi rangi wala kupigwa lipu yanaachwa hivyo hivyo na madirishani wakiweka mifuko ya cement, mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu. Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki

USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM au STK etc huku hakufai usafiri haueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .

MAJI
Kwa mara ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi. Kama huna kazi hapakufai, maji ya kunywa ni ununue bila hivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha.


KAZI
Dodoma ofisi nyingi zinahamia huku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar, Mwanza na Arusha huku utapauka dakika 2 baada ya kushuka stand

MWISHO
Nisipoona hata mvua hii miezi iliobaki hata kwa mganga nitaenda nihame ofisi.
Una karibia Mwaka hujaona mvua eti, kama sio unaku ni nini sasa unabonga
 
Hivi toka lini mvua ndio imekuwa main factor? mikoa mingi yenye kupata mvua nyingi kwa mwaka tena nyingi sana lakini haina fusra. Mimi nahisi kunachuki nyingi sana kutoka kwa wakazi wa Dar ile kuchukuliwa hadhi ya kisiasa au cake kugawanywa tu imekuwa kero kwao. Nchi hii watu wamepata shida sana ilikuwa ukitaka chochote lazima uende Dar sasa leo watu wanayapata maeneo yao na kikubwa mji wa Serikali ukikamilika 100% ndio basi Dar ni biashara tu.
Huyo ndugu nadhani hajatembea nchi hii wala haijui Dodoma vizuri. Ni kweli jitihada za kupanda miti zinatakiwa kuongezwa ukizingatia kuwa ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira iko hapa Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma wanaweza kuja na mkakati maalum wa upandaji miti ili kubadili hali ya jangwa iliyopo japo kwa sasa hali si mbaya kama ilivyokuwa miaka 10 nyuma.

Ukiacha hilo la hali ya hewa Dodoma ndio mji unaoongoza kwa kuwa na mpangilio mzuri wa mji kwani ujenzi unazingatia ramani ya mipango miji tofauti na miji mingi ya Tanzania kama Arusha na Mbeya unakoweza kudhani ni kambi za wakimbizi.


Pia usafiri wa umma upo na ni mzuri na bei zinaratibiwa na LATRA kinyume na mwandishi anavyotaka kupotosha. Mimi niko Dodoma huu ni mwaka wa 28 naongea kwa uzoefu na nimeishi pia mikoa mingi ya nchi hii na hata nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom