Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Kuuliza watu wanaoshije mahali huo ni utoto, na ukiona bado huwezi kujichagulia uishi wapi wewe ndo mwenye matatizo!
Dodoma hakuna harsh environment ya kuanza kujadili humu, watu wanaoshi mpaka Yakutsk huko baridi inaafika -60celcius na wala hawakai wakilia lia!
 
Kwani wakaazi wa Dom ni Wagogo tu ...vp Warangi,Wanyambwa,Wakaguru,Wasagara,Wasandawe wapo wapi!!?
vyasaka wote uliowataja.

Kuna mrangi kwenye mataa ya DAr es salaam?
Kuna Msandawe kwenye mataa ya Dar es salaam?
Kuna Mkaguru kwenye mataa ya Dar es salaam?
 
Nakumbuka nilivyoenda Dodoma mara ya kwanza 2019, Juwa liliniwakia wiki moja tu nikawa nimapasukapasuka ngozi ya uso na mikono,nikaacha kodi ya nyumba maeneo ya nkuhungu na vitu vya ndani nikapanda Kapricon kurudi arusha.
Jua la Dodoma linachoma utosi hata likiwa la saa 10 jioni🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Yn ni umemaliza kila kitu, nimesoma huko lkn sijawah kupapenda yn ni hovyo tu.
 
Lile jua ss linakufanya ngoz ifubae yn mana linakupiga hlf hutoki jasho 😄
 
Amna mtu mwenye akili aweke hate na hili jangwa
Mkuu wewe ukisema hapafai, Mfano Mimi hapa Dodoma panafaa sana, inategemea na Wewe unapendele Nini! Kwenye story ya Biblia kuna wapelelezi walitumwa wakaipeleze nchi flani,wajumbe walirudi na majibu tofauti!1:Nchi ile hafai Ina majitu yanayotisha na marefu.2:Nchi ile inafaa sana Ina maziwa na Asali:SuRUHISHO:Mfalme akaona kweli nchi inafaa!Maana majitu marefu na yenye miili,manake yameshiba chakula kingi.Hivyo Wewe mawazo Yako ni Nyumba au jangwa,mafundi wabovu?Kama ni kujenga watu wanatumia mainjinia na Wengine wanaagiza mafundi wanaowaamini.
 
Kuuliza watu wanaoshije mahali huo ni utoto, na ukiona bado huwezi kujichagulia uishi wapi wewe ndo mwenye matatizo!
Dodoma hakuna harsh environment ya kuanza kujadili humu, watu wanaoshi mpaka Yakutsk huko baridi inaafika -60celcius na wala hawakai wakilia lia!
Kweli Mkuu Bado nchi zetu za Afrika tunaneema hata huko kwa kina Biden kila siku ni vimbunga.
 
dodoma vijijini wanapaswa kuhimizwa kukata minyaa yote na kupanda miti ya asili

hali ya hewa pale ni hovyo sana

upasuliwe mtaro mkubwa toka ziwa victoria kuja kuilowanisha dadama iwe chepechepe miaka 5 tuh panakua kama marangu kule moshi au olimotoni kule arusha
 
Jua la Dodoma linachoma utosi hata likiwa la saa 10 jioni🙆‍♂️🙆‍♂️
Mbona Dom hawaendi na vitambaa vya kujifuta jasho kazini kama Dar ambako masaa 24 mwakamzima ni full joto. Ofisi nyingi za Dom hazina feni wala AC kama huku Dar ambako ni lazima 😀😀
 
we jamaa ni muongo sana nadhani wewe ni dent wa chuo na wala sio mfanyakazi. ukae mwaka usione mvua hizi zilizonyesha hadi mwezi wa tano zilikuwa manii ama upalata?

Nauli haziko fixed wapi? Route ndefu mfano Mjini Ihumwa ni 900 kwingineko ni 600 kwa wakazi wa Kikuyu wao hawana daladala ni bajaj ambayo ni 1000 haizidi hata anayekaa Chidachi.
Rudi kwenu
Samahani naomba kujua kwanini wakazi wa Kikuyu hawana daladala kama maeneo mengine? Nini kimefanya eneo hilo likose daladala!

Sent from my SM-A325N using JamiiForums mobile app
 
dodoma vijijini wanapaswa kuhimizwa kukata minyaa yote na kupanda miti ya asili

hali ya hewa pale ni hovyo sana
Hakuna sehemu inaitwa dodoma vijijini...Dodoma kuna Dom CC,Kondoa TC,Kondoa DC,Chamwino,Bahi,Mpwapwa,Kongwa na Chemba
 
Ombaomba wa Dodoma ni pasua kichwa, ni kama wako na dawa ya kutambua huyu ni mwenyeji na yule ni mgeni. Wanaomba omba kwa kupanga foleni wanakuja mmoja baada ya mwingine
 
Back
Top Bottom