Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

NI kajinga flani hivi kanadhani sote ni wajinga eti nyumba mbaya na zinajengwa kiholela
Angesema nyumba mbovu na mbaya ziko kwenu Usukumani na hasa Mwanza is Slum,Dom ni something else😬😬😬😬👇👇
Screenshot_20241008-193403.jpg
 
Dodoma hakuna milima wala mito hata mmoja ila vichuguu kibao.
😀😀Kumbe kule walipojenga Udom ni vichuguu!!?,Kwa Waziri Mkuu Area D ni vichuguu!!? ,Imagi Hill kwenye minara ni vichuguu...!!? Ihumwa Jeshini ni vichuguu..!!?, Ikulu ni vichuguu..!!? Milima nyuma ya gereza la Isanga ni vichuguu...!!?
Chuki+wivu ni hatari kwa afya yako aisee
 
Upo sahihi Mkuu.

Dodoma ni uwe umeyapatia maisha tayari. Ni pagumu mno, lakini huwenda ndio sehemu inakua kwa kasi na fursa zinaonekana.

Ni kupambana hapohapo.
Sio huwenda ,Bali ndio ukweli kwamba Jiji linakua Kwa Kasi.

Dom sio sehemu ya kuishi maskini,hao Waendelee Mwanza,Dar,Mbeya,Songwe na Sumbawanga wanakokula chapati na maharage Kwa jero.
 
huyo jamaa ni walewale "hater" nina wasiwasi kama kweli amewahi kufika Dom manake anajichanganya mwenyewe anasema eti anakaribia mwakamzima hajaona mvua wakati msimu wa masika mwakahuu Dom mvua ilinyesha ya kutosha hadi kuvunja rekodi😀😀
Hao ni wale wanaosimuliwa.Kwanza Dom ya Sasa imepandwa miti Mingi sana na sijui huo Ukame wanaoutaja ni upi 😂😂
 
Nilikaa wiki 2 tu ngozi ikawa na madoa doa meusi 😃😃😃
 
Nianze kwa kusema nimeishi Arusha, Mwanza, Dar Moshi, na sasa hivi nipo Dodoma unaelekea Mwaka sasa nipo huku kwa sababu za kikazi.

HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua, mchana kuna jua kali sana na vumbi halafu jioni na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .

MAKAZI
Kwa sasa hivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabisa ,Sidhani hata kama wanatumia ramani kwenye kujenga maana wanajenga manyumba makubwa kama makubwa jinga halafu mabaya hayapakwi rangi wala kupigwa lipu yanaachwa hivyo hivyo na madirishani wakiweka mifuko ya cement, mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu. Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki

USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM au STK etc huku hakufai usafiri
20241012_091736.jpg
haueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .

MAJI
Kwa mara ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi. Kama huna kazi hapakufai, maji ya kunywa ni ununue bila hivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha.


KAZI
Dodoma ofisi nyingi zinahamia huku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar, Mwanza na Arusha huku utapauka dakika 2 baada ya kushuka stand

MWISHO
Nisipoona hata mvua hii miezi iliobaki hata kwa mganga nitaenda nihame ofisi.
Karibu Hapa Kili
20241015_060450.jpg
20241015_060438.jpg
20241012_143143.jpg
20241012_091736.jpg
20241012_091721.jpg
 
Dom hapana hizo situation nilizotaja,no anything extremely so pako liveable Kwa factors nyingi sana kushinda Dar
Si unaweza kuishi uko wewe?
Mimi sipataki na sina ulazima kuishi Dodoma.
Hutaki kuishi Njombe na Dar na unaona uko sawa, ila mtu akisema hataki kuishi Dodoma unamuita mjinga. Wewe mwenye akili ishi Dodoma wala usitumie nguvu nyingi kulazimisha kila mtu aishi uko.
 
Nilikuwa nimejifanya ngunguri nikaenda pale Chef Asili kusubiri basi mida ya saa moja.Nilipigwa na baridi mpaka nikanunua uji wa mchele bila kupenda.Kuna upepo Dodoma usiku sijawahi ona.
Hahahaha 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 😂
Nimecheka sanaaaa aisee!!!!
Vipi haujaungua mdomo baada ya kumaliza uji
 
Back
Top Bottom