Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Kuuliza watu wanaoshije mahali huo ni utoto, na ukiona bado huwezi kujichagulia uishi wapi wewe ndo mwenye matatizo!
Dodoma hakuna harsh environment ya kuanza kujadili humu, watu wanaoshi mpaka Yakutsk huko baridi inaafika -60celcius na wala hawakai wakilia lia!
Huyo jamaa ukute hajawahi hata kukanyaga Dom ila amesimuliwa tu😂😂..hali ya hewa ya Dom ni "moderate" sio baridi kali wala joto kali .Ingekua baridi kali kama Makete au joto kali kama Dar mwakamzima labda ndio tungejua ana point ila hana point yoyote zaidi ya chuki+wivu
 
Nianze kwa kusema nimeishi Arusha, Mwanza, Dar Moshi, na sasa hivi nipo Dodoma unaelekea Mwaka sasa nipo huku kwa sababu za kikazi.

HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua, mchana kuna jua kali sana na vumbi halafu jioni na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .

MAKAZI
Kwa sasa hivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabisa ,Sidhani hata kama wanatumia ramani kwenye kujenga maana wanajenga manyumba makubwa kama makubwa jinga halafu mabaya hayapakwi rangi wala kupigwa lipu yanaachwa hivyo hivyo na madirishani wakiweka mifuko ya cement, mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu. Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki

USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM au STK etc huku hakufai usafiri haueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .

MAJI
Kwa mara ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi. Kama huna kazi hapakufai, maji ya kunywa ni ununue bila hivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha.

KAZI
Dodoma ofisi nyingi zinahamia huku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar, Mwanza na Arusha huku utapauka dakika 2 baada ya kushuka stand

MWISHO
Nisipoona hata mvua hii miezi iliobaki hata kwa mganga nitaenda nihame ofisi.
Lakini hapo hapo unapasifia dubai
 
Huyo jamaa ukute hajawahi hata kukanyaga Dom ila amesimuliwa tu[emoji23][emoji23]..hali ya hewa ya Dom ni "moderate" sio baridi kali wala joto kali .Ingekua baridi kali kama Makete au joto kali kama Dar mwakamzima labda ndio tungejua ana point ila hana point yoyote zaidi ya chuki+wivu

Huyu jamaa ni wa kupuuzwa [emoji3]
 
Ombaomba wa Dodoma ni pasua kichwa, ni kama wako na dawa ya kutambua huyu ni mwenyeji na yule ni mgeni. Wanaomba omba kwa kupanga foleni wanakuja mmoja baada ya mwingine
Tutajie mji wowote mkubwa Tanzania ambao hauna ombaomba....kama ombaomba wapo hadi New York,Marekani kuna cha ajabu apo😀
 
Mbona Dom hawaendi na vitambaa vya kujifuta jasho kazini kama Dar ambako masaa 24 mwakamzima ni full joto. Ofisi nyingi za Dom hazina feni wala AC kama huku Dar ambako ni lazima 😀😀
Sure, dom hakuna mtu anajenga nyumba yake anaweka feni au ac....hlf wanakwambia hali ya hewa mbaya, inachekesha sana...coz asbh ht ukipiga suti huteseki na joto kama Dar
 
huyo jamaa ni walewale "hater" nina wasiwasi kama kweli amewahi kufika Dom manake anajichanganya mwenyewe anasema eti anakaribia mwakamzima hajaona mvua wakati msimu wa masika mwakahuu Dom mvua ilinyesha ya kutosha hadi kuvunja rekodi😀😀
Anachangamsha tu wasomaji, kuona waliowahi kufika huko.
 
dodoma vijijini wanapaswa kuhimizwa kukata minyaa yote na kupanda miti ya asili

hali ya hewa pale ni hovyo sana

upasuliwe mtaro mkubwa toka ziwa victoria kuja kuilowanisha dadama iwe chepechepe miaka 5 tuh panakua kama marangu kule moshi au olimotoni kule arusha
😄😊😊😊🤣🤣🤣eti upasuliwe mfereji...
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Sure, dom hakuna mtu anajenga nyumba yake anaweka feni au ac....hlf wanakwambia hali ya hewa mbaya, inachekesha sana...coz asbh ht ukipiga suti huteseki na joto kama Dar
Kuna watu wanaichukia Dom bila sababu yoyote ya msingi😀😀...ukiwauliza wanakuja na ngonjera zilezile mara jangwa,mara ukame mara hali ya hewa mbaya 😀😀mtu huyohuyo tena utakuta anakwambia hataki miji yenye baridi kali kama njombe au jotokali kama Dar
 
Anachangamsha tu wasomaji, kuona waliowahi kufika huko.
JF sikuhz imevamiwa na vitoto vya facebook😀😀 anakwambia eti amekaa Dom karibia mwaka hajaona mvua wakati msimu wa masika Dom umeisha miezi minne nyuma🤣🤣
 
Nianze kwa kusema nimeishi Arusha, Mwanza, Dar Moshi, na sasa hivi nipo Dodoma unaelekea Mwaka sasa nipo huku kwa sababu za kikazi.

HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua, mchana kuna jua kali sana na vumbi halafu jioni na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .

MAKAZI
Kwa sasa hivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabisa ,Sidhani hata kama wanatumia ramani kwenye kujenga maana wanajenga manyumba makubwa kama makubwa jinga halafu mabaya hayapakwi rangi wala kupigwa lipu yanaachwa hivyo hivyo na madirishani wakiweka mifuko ya cement, mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu. Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki

USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM au STK etc huku hakufai usafiri haueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .

MAJI
Kwa mara ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi. Kama huna kazi hapakufai, maji ya kunywa ni ununue bila hivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha.

KAZI
Dodoma ofisi nyingi zinahamia huku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar, Mwanza na Arusha huku utapauka dakika 2 baada ya kushuka stand

MWISHO
Nisipoona hata mvua hii miezi iliobaki hata kwa mganga nitaenda nihame ofisi.
Kwa huu uandishi huwezi ishi Dodoma jombaaa.
 
Away from Kingstown to Dodoma, wewe Kweli umepoteana!
 
Unasema hujaona mvua au ulikua umesafiri nini? Mvua imenyesha mpk mwanzoni mwa mwezi wa 3 mvua ya maana yani mvua mpk mafuriko...
 
Nianze kwa kusema nimeishi Arusha, Mwanza, Dar Moshi, na sasa hivi nipo Dodoma unaelekea Mwaka sasa nipo huku kwa sababu za kikazi.

HALI YA HEWA
Huu mji toka nifike sijaona mvua, mchana kuna jua kali sana na vumbi halafu jioni na usiku upepo mkali wa baridi kama jangwani karibia napakimbia .

MAKAZI
Kwa sasa hivi Dodoma ujenzi ndo mahala pake lakini watu hawajui kujenga kabisa ,Sidhani hata kama wanatumia ramani kwenye kujenga maana wanajenga manyumba makubwa kama makubwa jinga halafu mabaya hayapakwi rangi wala kupigwa lipu yanaachwa hivyo hivyo na madirishani wakiweka mifuko ya cement, mabox au makaratasi ya magodoro ni kichefuchefu. Ukija kwenye bati ndo huzuni mabati marefu refu kama Mkuki

USAFIRI
Kama huna gari au sio wa kutokea STM au STK etc huku hakufai usafiri haueleweki wala nauli hazieleweki kila mtu na nauli yake .

MAJI
Kwa mara ya kwanza nashuhudia maji ya idara ya maji yana chumvi. Kama huna kazi hapakufai, maji ya kunywa ni ununue bila hivyo utakunywa chumvi uwe na meno kama ndugu zetu wa Arusha.

KAZI
Dodoma ofisi nyingi zinahamia huku lakini sio sehemu bora ya kuja kuanzia maisha kama huna ramani tofauti na mikoa kama Dar, Mwanza na Arusha huku utapauka dakika 2 baada ya kushuka stand

MWISHO
Nisipoona hata mvua hii miezi iliobaki hata kwa mganga nitaenda nihame ofisi.
Makazi
Ungesema unakaa wapi maana kila mkoa una sehemu miyayusho zipo otherwise ofisi unayofanyia kazi ni njaa tu

Usafiri
Dodoma usafri mkuu ni bajaji uzuri wa dodoma hamna foleni ni chapu kwa haraka usafri wa bajaji umeenda bei sana ni tsh 1500...ila sehemu nyingi ni tsh 700,800 na 1000.
Daladala pia zipo ni wewe tu na chaguo lako.

Kazi
Hapa sijakuelewa hata unataka kusema nini..ila kama unaamanisha kujitafuta dodoma ina fursa nyingi sana.

Maji
Hapa ndio umegusa kwenye mambo yangu ya geology iko hivi dodoma kuna maji ya chumvi lakini pia kuna sehemu nyingine nyingi kuna maji matamu(soft) kwa kufupi inategemeana na mwamba wa maji watu wanaoishi kwa waziri mkuu,swaswa mlimwa C maji yao ni matamu sana

Ushawahi kunywa maji ya Pugu (DSM) wewe..

Kichwa chako ni mweupe sana hata kazi sijui unafanya kazi gani umeshindwq kujua kwamba kuna kupindi cha masika na kiangazi....

Umeandika ujinga tu.
 
Back
Top Bottom