Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Mbona leo tu nimempokea demu kutoka dodoma pisi kali sana kuliko hata wahapa au dodoma yawapi?
 
Kuna mgombea mwaka 2020 alidai ataipeleka bahari Dodoma.
 
Una karibia Mwaka hujaona mvua eti, kama sio unaku ni nini sasa unabonga
 
Huyo ndugu nadhani hajatembea nchi hii wala haijui Dodoma vizuri. Ni kweli jitihada za kupanda miti zinatakiwa kuongezwa ukizingatia kuwa ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira iko hapa Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma wanaweza kuja na mkakati maalum wa upandaji miti ili kubadili hali ya jangwa iliyopo japo kwa sasa hali si mbaya kama ilivyokuwa miaka 10 nyuma.

Ukiacha hilo la hali ya hewa Dodoma ndio mji unaoongoza kwa kuwa na mpangilio mzuri wa mji kwani ujenzi unazingatia ramani ya mipango miji tofauti na miji mingi ya Tanzania kama Arusha na Mbeya unakoweza kudhani ni kambi za wakimbizi.


Pia usafiri wa umma upo na ni mzuri na bei zinaratibiwa na LATRA kinyume na mwandishi anavyotaka kupotosha. Mimi niko Dodoma huu ni mwaka wa 28 naongea kwa uzoefu na nimeishi pia mikoa mingi ya nchi hii na hata nje ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…