Hivi mnawezaje kuishi maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja?

Hivi mnawezaje kuishi maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja?

Hujanielewa. Sijasema mtu wa Mungu hawezi kufanya dhambi. Nilichosema inawezekana vipi mtu ukawa unafanya dhambi kubwa na at the same time unawaaminisha watu kuwa ni mtu wa kiroho sana. Kwanini baada ya kufanya dhambi usitubu na kubadili njia zako ndipo urudie kazi zako za dini au urudie kuwaonyesha watu kuwa uko vizuri?
Bado anastruggle kuupata ukamilifu japo anaanguka katika dhambi mara kwa mara. Hajaacha kuendelea kujaribu kurudi kwenye mstari kwani ukisema ukate tamaa unakuwa unaikatia tamaa nafsi yako mwenyewe.
 
Nakumbuka nilipokuwa secondary Kuna mdada mmoja alikuwa mwenyekit wa maombi wa ukwata. Na nakumbuka alikuwa anaongoza maombi wakati wa shughuli zingine za shule na hata kama mtu kapata shida inayohitani maombi yeye ndiyo alikuwa naaongoza na hata wakati tunamaliza form four yeye ndiye aliongoza ibada ya kutuombea zikiwa zimebaki wiki 2 kabla ya mtihani.

Sasa ile wiki ya mwisho kabla ya mtihani tukashangaa kapotea na hata akionekana anaona aibu aibu.
Kumbe alifumaniwa na mshikaji tulikuwa tunasoma naye, na story ilivyokuwa ni kwamba alikuwa anaenda geto kwa jamaa kwa kisngizio Cha kusoma tangu mwezi wa tano, na jamaa alikuwa anamla Kila akienda.

Sasa majirani walikuha kuwachoka ndipo wakapanga fumanizi pamoja na Baba wa yule dada.
 
kila mtu ana dark side yake na anajua anavyopambana nayo mkuu
Ni kweli lakini nafikiri Mungu anaijua vizuri sana hiyo dark side, so hatutakiwi ku pretend kwa watu wanaozunguka kwa kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za ibada na kujiongesha sana mbele ya watu kwamba sisi ni washikadini wazuri, huku tukijua kabisa Mungu anajua Mimi natembea na mume au mke wa mtu.

It's better ukafika ibadani ukatulia tu, na hata usihangaike kupost vitu vinavyoonyesha wewe ni mtu wa dini sana mpaka utakapo yaweka sawa na Mungu ndipo urudi kawaida.

Anyway tumuachie Mungu ndiye atakaye tutoza hesabu
 
Ni kweli lakini nafikiri Mungu anaijua vizuri sana hiyo dark side, so hatutakiwi ku pretend kwa watu wanaozunguka kwa kuwa mstari wa mbele kwenye shughuli za ibada na kujiongesha sana mbele ya watu kwamba sisi ni washikadini wazuri...
Upo sahihi mkuu tena sahihi sana lakini ubaya huo sio uhalisia wa dunia hii tuliyonayo

na kingine si kila mtu ana muono au moyo ulionao na hilo ndo linaifanya dunia isipooze yaani iwe na amsha amsha,

kikubwa kila mtu anajua nadhiri yake kama yupo sawa au anakosea na matokeo yake ni nini

hivyo kilochobaki waombee tu maana huwezi jua vifungo vilivyowafunga vina uzito kiasi gani
 
Unahukumu mjomba, hiyo siyo kazi yako.
Sihukumu hapa kwasababu uzinzi Kila mtu anajua kabisa Mungu hautaki na hata huyu mzinzi anajua kabisa ni kosa na analitendaa kimakusudi kabisa na unakuta ni mchungaji, muongoza maombi, au sometime anakuhubiria wewe au kikundi Fulani kama Whatsapp group na kuwajulisha Mambo ya Mungu. Then huyu mtu kwa bahati mbaya au kwa kukusudia anafanya uzinzi na ANAJUA kabisa alichofanya ni kosa KUBWA.

Sasa badala ya kuhangaika na Mungu kuweka sawa Hilo Jambo na kuliacha ndipo arudie uhusiano wake na Mungu ( ikihusisha kuwaonyesha watu wengine kwamba yeye ni mtakatifu sana), yeye anaamua kufanya yote mawili anaendelea na kuzini kama kawaida na anaendelea na kanisa kama kwaida Tena akiwa mstari wa mbele kabisa. hii ndiyo double life ninayoisema
 
Mwendazake jumapili alikuwa anaenda Chachi na kura kwenye uchaguzi akaiba hiyo unaizungumziaje.
 
Umeona ka post halafu ukamfatilia Hadi gesti??
 
Kumekuwa na watu wengi ambao wanaishia maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja, mfano unakuta mtu ametoka kufanya uzinzi mchana, then jioni anapost status au post ya kawaida kwenye Whatsapp, FB na inta akiwahimiza watu kuhudhuria ibada ya maombi na akiwa confident kabisa. Unakuta kesho anaenda kuliwa Tena na akirudi anawakumbusha kwenda kwenye hiyo ibada.

Wengine unakuta anatembea na mume wa mtu Mara nyingi tu lakini Hana aibu ya kuweka content inayoonyesha Yuko vyema na Mungu.

Au anapost vifungu vya bible au kujaribu kufanya chochote kinachoonyesha yeye ni mtu wa dini sana.

Huwa najiuliza sana, watu wanaenda kanisani kuongeza idadi ya watu au kusikiliza maneno ya Mungu na kujaribu Kuishi kulingana na maneno ya Mungu na hata kama ikitokea umefanya dhambi nzito kama uzinzi basi unatakiwa kuonyesha unyenyekevu na kusali sana ili kujisafisha na kuhakikisha umeweka sawa mahusiano yako na Mungu ndipo uanze kufanya kazi ya kiwatangazia wengine habari za Mungu.

How is this possible?
Mkuu kuna mtu kakufanyia timing huko nini? maana mawaidha yako yame base kwenye eneo moja na pia umeipa daraja uzinzi kama dhambi nzito, sijui kwa kipimo kipi, ukiona pilika pilika za vitoto mitaani ujue shughuli ya kufyatua inafanyika huko.......kwa hiyo jaribu kujikita kwenye mishe zako binafsi, ya kwao waachie wenyewe......
 
Usihukumu! Hiyo ni kazi ya Mungu.
Mybe uko sahihi, lakini Mimi ninawazungumzia watu ambao mioyo yao wenyewe inawaambia hii uliyofanya ni dhambi kubwa lakini kesho unamkuta anaongoza ibada kanisani na kukemea kuhusu Jambo hilo Hilo na keshokutwa unamkuta anafanya dhambi ile ile.
Au unakuta mtu kaahidiana kufanya uzinzi na mtu baada ya kutoka kanisani, na huku kanisani anaishi kama mtakatifu, kama ni mchungaji basi anahubiri kama kawaida na kama ni mwanakwaya basi anaimba kwaya yake vizuri kabisa. This is double life ninayoizungumzia.


Mfano ambao umefanya nilete Uzi hapa,
Kuna kadada kamoja kalokole kanatembea na brother angu mmoja hivi ambaye ameoa na kanajua ninajua vizuri mahusiano yao, na kale kadada ni koingozi wa timu ya maombi huko kanisani kwao. Sasa unakuta jamaa ameondoka bako kwenda guest mchana then jioni unakutana na status ya mkesha wa maombi au seminar ambayo na yeye ni moja wa speekers[emoji848][emoji848]. Na unakuta kesho Tena kaenda kuliwa na bado anapost tu hizo seminar na hata akitoka kwenye hizo seminar anaenda kuliwa Tena.

Sasa ninachouliza hapa inawezekana vipi mtu Kuishi maisha haya ambayo haufeel guilt kabisa mbele ya watu na mbele ya Mungu mwenyewe.
 
Mkuu kuna mtu kakufanyia timing huko nini? maana mawaidha yako yame base kwenye eneo moja na pia umeipa daraja uzinzi kama dhambi nzito, sijui kwa kipimo kipi, ukiona pilika pilika za vitoto mitaani ujue shughuli ya kufyatua inafanyika huko.......kwa hiyo jaribu kujikita kwenye mishe zako binafsi, ya kwao waachie wenyewe......
[emoji1787] umepiga target[emoji121].
Inauma sana kuchapiwa kimasihara pale ulipowekeza.
 
Mwendazake jumapili alikuwa anaenda Chachi na kura kwenye uchaguzi akaiba hiyo unaizungumziaje.
Yeye kaiona ya uzinzi tu na kaipa na uzito sijui wa kilo ngapi, siyo bure jamaa kafanyiwa timing kwenye mchepuko....
 
Mkuu kuna mtu kakufanyia timing huko nini? maana mawaidha yako yame base kwenye eneo moja na pia umeipa daraja uzinzi kama dhambi nzito, sijui kwa kipimo kipi, ukiona pilika pilika za vitoto mitaani ujue shughuli ya kufyatua inafanyika huko.......kwa hiyo jaribu kujikita kwenye mishe zako binafsi, ya kwao waachie wenyewe......
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom