Hivi mnawezaje kuishi maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja?

Hivi mnawezaje kuishi maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja?

Tena wengi wanaoshika dini sana ni wanafiki. Ndio wenye kufanya matendo ya ajabu zaidi ya wa wa kawaida.
 
Kumekuwa na watu wengi ambao wanaishia maisha ya aina mbili kwa wakati mmoja, mfano unakuta mtu ametoka kufanya uzinzi mchana, then jioni anapost status au post ya kawaida kwenye WhatsApp, FB na inta akiwahimiza watu kuhudhuria ibada ya maombi na akiwa confident kabisa. Unakuta kesho anaenda kuliwa Tena na akirudi anawakumbusha kwenda kwenye hiyo ibada.

Wengine unakuta anatembea na mume wa mtu Mara nyingi tu lakini Hana aibu ya kuweka content inayoonyesha Yuko vyema na Mungu.

Au anapost vifungu vya bible au kujaribu kufanya chochote kinachoonyesha yeye ni mtu wa dini sana.

Huwa najiuliza sana, watu wanaenda kanisani kuongeza idadi ya watu au kusikiliza maneno ya Mungu na kujaribu Kuishi kulingana na maneno ya Mungu na hata kama ikitokea umefanya dhambi nzito kama uzinzi basi unatakiwa kuonyesha unyenyekevu na kusali sana ili kujisafisha na kuhakikisha umeweka sawa mahusiano yako na Mungu ndipo uanze kufanya kazi ya kiwatangazia wengine habari za Mungu.

How is this possible?
Wameshakubuhu, hakuna kinachowapa hofu.
 
Unapoogopa kumcha Mungu kisa unatenda dhambi ni Sawa na mtu anaeogopa kuoga au kunawa akishachafuka. Cha Muhimu ni kutubu na kuzidi kumwomba Mungu
 
Dhambi ni uhasi (Kumkataa Mungu kwenye maisha yako )
Usiitizame dhambi kimatendo utachanganyikiwa.

Kuuwa ni Dhambi lakini je mwanajeshi au police anaweza kuuwa akiwa kazini je ni dhambi hiyo atachomwa moto kisa kuuwa adui/jambaz?
 
Unaiba pesa ofisini halafu unaporomosha lijumba likubwa na lifensi la uhakika ili wezi wasimwibie mwizi mwenzao
 
Back
Top Bottom