Hivi Mo akitoa Bilioni 20 anatakiwa kuwapa wakina nani?

Moo alikurupuka kutaja hizo hela.
Ni wazi atakayeumia Ni yeye.
Brand ya Simba hauwezi kuwa na thamani ya bilioni 20 kwa mkupuo.
Atafakari upya.
Kama anatoa atoe tu sadaka Ila kurudi na faida JUU hyo ni NDOTO
 
Kutokana na sheria na taratibu zetu,wananchii(wanachama wa Simba) ndo watakua wamiliki wa hizo 51%,Maana Mo alitakaga kuchukua 100% ila sheria ikambana.
Mkuu kwasasa Wanachama si wanamiliki asilimia 100? Sasa wanapata nini na kuuza kwao 49?. Hiyo 51 ni yao toka zamani.
Au Mo si mnunua hisa. Maana ukinunua hisa pesa haziendi kwenye mtaji wa kampuni bali zinaenda kwa wamiliki wa hisa/ kampuni, kwa Simba wanachama.
 
Moo alikurupuka kutaja hizo hela.
Ni wazi atakayeumia Ni yeye.
Brand ya Simba hauwezi kuwa na thamani ya bilioni 20 kwa mkupuo.
Atafakari upya.
Kama anatoa atoe tu sadaka Ila kurudi na faida JUU hyo ni NDOTO
Ni kweli boss Mo alikurupuka kutaja hiko kiasi,Maana mpaka Leo hawajui club ina thamani gani,Wanachama wao wangapi TZ nzima n.k
 
Nani anayemiliki hiyo Simba sport club company. Maana huyo ndiye hasa anauza hisa na ndiye anatakiwa kupewa pesa.
Simba sports club company Ni mtu kisheria,ina management yake na bodi ya wadhamini ambao wanaimiliki Simba kwa niaba ya wanachama,hao ndo watakabidhiwa hiyo pesa.Tatizo wote wanaumwa apedomia.
 
Atapewa waziri anayemiliki wakina simba naona leo kaomba msamaha
 
Moo alikurupuka kutaja hizo hela.
Ni wazi atakayeumia Ni yeye.
Brand ya Simba hauwezi kuwa na thamani ya bilioni 20 kwa mkupuo.
Atafakari upya.
Kama anatoa atoe tu sadaka Ila kurudi na faida JUU hyo ni NDOTO
Ni zaidi ya hiyo. Maana kama 49 ni sawa na bilioni 20 basi asilimia 100 ni zaidi ya bln 40

kiufupi Mo ameithaminisha Simba kwa zaidi kidogo ya bilioni 40
 
Simba sports club company Ni mtu kisheria,ina management yake na bodi ya wadhamini ambao wanaimiliki Simba kwa niaba ya wanachama,hao ndo watakabidhiwa hiyo pesa.Tatizo wote wanaumwa apedomia.
Unavyosajili kampuni unaandika majina ya shareholders. Hao ndiyo wamiliki. Kwa Simba sport club company ni wakina nani?.
Hao ndiyo hupewa hela hisa zikiuzwa.
 
Ikumbukwe Simba wapo katika member's tier bado,kwahyo hamna mtu ambae ana miliki hisa,Hata wanachama wenyewe hawana hisa,

Kwahyo baada ya kuchange club managerial structure Mo dewji ndo anakua anaipa Simba sports club B20 kwa kuomba 49% ya umiliki wake,Afu the rest % ndo zinakua zinamilikiwa na members,

Karibu.
 
Ni kweli boss Mo alikurupuka kutaja hiko kiasi,Maana mpaka Leo hawajui club ina thamani gani,Wanachama wao wangapi TZ nzima n.k
Mchakato ulifanya kienyeji, inawezekana mo amepigwa au Simba wamepigwa.
Kuna soko la mitaji ya hisa wana wataalamu kibao wangewasaidia au kuna kampuni kama kpmg au price water coopers wangeweza kuweka mambo sawa.
Tofauti ya mo na Simba, mo anajua anachofanya ndio maana alipoingia akataka hati ya jengo na akataka mahesabu ya nyuma ya miaka mitano yakaguliwe.
Mahesabu yakikaguliwa na madeni yakiondolewa unaweza kukuta Simba wanalipwa bilioni moja au pungufu kwani madeni makubwa wanayodaiwa Simba yanatoka kwa mo.
 
Me nlikua najua nawafanyia hisani,kumbe madeni.
 
Swali langu kwa wale watalaamu wa uhasibu,Hivi simba ikiwa kampuni Assets zinatajumuisha na wachezaji? na kama hapana vipi pale wanapouza wachezaji wanakuwa wanauza nini ki- uhasibu, yaani treatment yake kwenye vitabu inakuwaje.Angalizo hapa panahitaji jibu la kihasibu,kama siyo mhasibu jipe nafasi ujifunze kutokana na majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…