Hivi Mo akitoa Bilioni 20 anatakiwa kuwapa wakina nani?

Wachezaji wa Simba ni asset ya Simba wanapokuwa wana mkataba na Simba.
 
Naongezea hapo hapo,Na vipi ukamvunjia mchezaji mkataba wake na unatakiwa kumlipa hela zake,he uta-m- treat Kama creditor(liability)?

Maana haya Mambo haya.
 
Apedomia na mayala ndo chanzo.
 
Lakini mkuu hao wanachama wakija kubaki na 51, watapata nini kutokana na zile 49 walizompa Mo? Kumbuka hela ya kuuza hisa hairudi kwenye kampuni.

kuna ile unakuta kampuni ina hali mbaya basi unaomba muwekezaji aweke hela kwa mbadala wa hisa. Hapa hela huenda kwenye kampuni na hesabu yake huwa tofauti, labda kama ndicho kinachofanyika Simba.
 
Kwani haiwezekani hizo 49% shares atakazonunua Mo wanachama wakaamua ziende katika uendeshaji wa kampuni? Hivi niulize, hizi klabu za Simba nk zinajua idadi kamili ya wanachama wake, maana kama ni mwendo wa hisa si itabidi wagawane hizo hisa kwa % kutegemea na idadi yao?
 
Kama Mo ananunua 49% shares za Simba kwa 20bil, maana yake ni kuwa Simba ina thamani ya 40bil+. Je, hizo 20bil+ zilizobakia kwa wanachama ziko wapi?
 
Hili linawezekana lakini hutokea pale kampuni huwa na hali mbaya. Hutafuta muwekezaji na kumpa hisa na wao hutumia zile pesa kujikwamua. Kama kampuni inaenda poa na ikauza hisa basi zile pesa hupewa wanahisa/wamiliki.
 
Hili linawezekana lakini hutokea pale kampuni huwa na hali mbaya. Hutafuta muwekezaji na kumpa hisa na wao hutumia zile pesa kujikwamua. Kama kampuni inaenda poa na ikauza hisa basi zile pesa hupewa wanahisa/wamiliki.
Hao wanachama wanaopata huo mgao wa hisa, wao walitoa nini? Namaanisha kama mwanahisa kuna kitu unachangia, katika hizo 100% hisa walinunua, hivyo zikiuzwa wanakuwa na chao hapo. Sasa wanachama wa Simba wana nini walichochangia ili Mo akinunua hisa wao wawe wanufaika? Au ni kadi za uanachama ndio zinawabeba?
 
Mo hawezi kutoa 20B uwekezaji wake ni wa janja janja tu nafuu hata ya GSM.Mo sio mtu wa kumuamini hata kidogo ni kigeugeu simba wakae tako moja tu hakuna jingine.

Kila siku utasikia mara mchakato haujakamilika ,mara 20B hela nyingi naweza fungua bank kama anaona 20B inatosha kufungua bank si akafungue ,juzi anakuja na kisingizio cha FCC haya ss kashajibiwa na FCC haitishe press nyingine ya majibizano.

Mo ana damu ya kihindi tusijisahaulishe jamani,kama alishindwa kopesha waziri pikipiki 20 atatoa 20B huyu??
 
Wao ndiyo wamejenga timu hadi imekuwa na thamani kubwa leo. Wao ndiyo wamiliki wa timu.
 
Kama Mo ananunua 49% shares za Simba kwa 20bil, maana yake ni kuwa Simba ina thamani ya 40bil+. Je, hizo 20bil+ zilizobakia kwa wanachama ziko wapi?
Mkuu hapo ndo kimbembe maana hisa moja ina cost 40M+,je Mo akiweka mzigo wanachama wapo tayar kuweka the rest %?!,

Ila kuna baadhi yao wanasema eti wao 51% yao Ni majengo na baadhi ya assets za kampuni,

Sasa swali la kujiuliza ni kua je? Hizo assets zao zinafikia thamani ya 51%?.
 
Mkuu naona wao 51% Ni lile jengo k/Koo na uwanja wa bunju(japokua Mo aliwasaidia pa kubwa),

Kama faida club ikiiipata,naona wata-i-retain kwa club.
 
Depends on terms of partnership.
Huyu yeye ndo haelewi,hivi ukienda kununua hisa 10000 za CRDB unatoa hela nusu au hela yote? Halafu kila mkataba una terms na conditions zake.
 
Simba inatakiwa iwe transformed kutoka Simba Sports Club inayomilikiwa na Wanachama na kwenda kuwa Simba Sports Club inayomilikiwa Simba Sports Club Company Limited chini ya uenyekiti ya Mo, itakayo milikiwa na Simba Sports Club Holdings inayo Milikiwa na Mo Simba Company inayomilikiwa na Mo.

Kipi msichokielewa hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…