DOKEZO Hivi Msumi ipo Dar es Salaam kweli?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hivi ndicho kipimo halisi cha akili ya muafrika. Imagine mtu anaanza kazi bila coordination na wadau wenzake muhimu. Nadhani kabla ya kuanza ujenzi ilitakiwa tayari kila mdau amehusishwa na kupangiana muda wa kuwajibika kwa kila mmoja yaani TANROAD, DAWASCO na TANESCO .
Kuna ujinga mwingi sana unaofanyika kwa baadhi ya watendaji wa taasisi za serikali NA BAHATI MBAYA SANA HATA WANAPOZEMBEA AU KUHARIBU HATA HAWATISHIKI. LABDA WASIKIE Mhe Rais ameulizia maendeleo ya ujenzi au wasikie Mhe waziri mkuu ameulizia ndipo wataanza kukimbizana na kuambiana jamani wakubwa wanafuatilia hili.

NADHANI NA UWAJIBIKATI KWA WATUMISHI WENGI NI YA HOVYOO SANA. PIA UBABAISHAJI NI WA KIWANGO CHA KUTISHA
 
Yule mkandarasi mhuni kweli kweli
Kawapigia lami kuanzia kati kamaliza 😄
Nchii f kweli kweli

Ova
 
Kuna mradi wq DMDP phase two watajenga barabara ya msumi kilometa 9.08 . Ujenzi unaanza mwezi wa saba. Kipindi wanatangaza zabuni ili mkandarasi apatikane. Tembelea page ya mkuu wa mkoa you tube autakuta kafafanua barabara ambazo zitapitiwa lami
Ktk makosa makubwa Watanzania tunafanya ni kuwaamini wanasiasa.

Mtu wa kupeleka barabara sehemu zote korofi kwa mkoa wa Dar alikuwa Dr Magufuli pekee(nazungumzia Dar sababu currently ndiko makazi yangu yalipo) the rest ni vichekesho vitupu,mimi naishi Makabe nyuma ya Msumi lakini huku ili mambo yaende tunatumia nguvu nyingi kweli kweli 2021 nilifunga maji ya dawasa ilini-cost karibia 800K na hiyo ni afadhali kuna ambao walitumia zaidi ya 1.5mill lakini form ya dawasa ada ya kufungiwa maji inasema gharama yake ni 255K.

Tatizo lililopo watu hawana mtu wa kuwasukuma,fedha zinatengwa but mpaka zije kufika kwenye mradi robo tatu yake wamegawana zinazobaki kidogo ndiyo zinaenda kwenye maendeleo kwa style hii hakuna siku tutafika.
 
Yule mkandarasi mhuni kweli kweli
Kawapigia lami kuanzia kati kamaliza 😄
Nchii f kweli kweli

Ova
Mjinga yule sehemu za kumwagwa zege vibarua wake walikuwa wanachanganya na chepe na kumwaga na vindoo kama vile wanajenga choo.

Ile ilikuwa kampuni uchwara kile kipande unachokiona pale kilijengwa zaidi ya miezi kumi.
 
Heheee manake hapo kwanza acha nicheke
 
Mkuu samahani, nikitaka kufika huko napitia wapi ? Nipo serious nataka nikafanye ziara huko nipaone.
 
Niliwahi kupanga huko mwanzo mwa 2001 niliacha kodi sehemu ni ya ajabu sijapata kuona alaaniwe yule dadali mwongo🤨
Huwezi kuwa na akili timamu ukaishi Msumi binafsi nilikaa mwenzi mmoja wa mateso nikaikimbia kama jela😳
Kwa muktadha wa kupanga upo sahihi lakini kama una makazi yako kule na una familia kubwa kwa kipato hiki cha Mtanzania wa kawaida hauwezi mtu ukawa hauna akili.
 
Itoe Makabe bro,Makabe sisi kinatutesa barabara tu issue za maji tumeshavuka japo kwa maumivu makali labda sema hospital ndiyo hatuna tunategemea ya Mbezi au tuunge hadi Mpiji Magoe.
 
Itoe Makabe bro,Makabe sisi kinatutesa barabara tu issue za maji tumeshavuka japo kwa maumivu makali labda sema hospital ndiyo hatuna tunategemea ya Mbezi au tuunge hadi Mpiji Magoe.
Mbona hapo kwa lipelanya wanakaa watu wazito kiasi na wana magritte mazuri tu lakini njiaa ya huko hawaipigii makelele

Ova
 
Mbona hapo kwa lipelanya wanakaa watu wazito kiasi na wana magritte mazuri tu lakini njiaa ya huko hawaipigii makelele

Ova
Ni kweli hata huko Msumi kuna watu wenye uwezo wanaishi ila linapokuja suala la wananchi kupata shida sample huwa inachukuliwa kutokana na wale hohehahe wa maeneo husika.

Nilikuwa namjibu mdau hapo juu kuhusu mazingira ya Makabe.
 
Itoe Makabe bro,Makabe sisi kinatutesa barabara tu issue za maji tumeshavuka japo kwa maumivu makali labda sema hospital ndiyo hatuna tunategemea ya Mbezi au tuunge hadi Mpiji Magoe.
Mpiji magoe Hospital gan au ile ya wilaya kule mabwepande?
 
Y not,.ukinikuta na hii mvua inavyonyesha utanionea huruma.😜
Kuna siku nipo pale Mbezi nikamsikia jamaa wa Bajaj anaitia ”Msumi na Bajaj buku nne” nikamwangaliaaa nikamuona hivi huyu anadhani hela watu wanaenda kuokota?nikaishia kumtukana kimoyo moyo.

Sema mkuu Msumi hata kama mateso yakizidi wokovu unakaribia ila nyie mnapata shida aisee,mtu anasubiri Eicher au DCM kwa dakika 45 inakuja anapanda halafu inaenda kuzimikia pale Mazulu au au njia panda Goba na hapo limekata spring au limetumbuka clutch na ni wazi kuendelea na safari itakuwa kesho lakini mnaendelea kuvumilia.

Hatari sana.
 
Hiyo ni kwembe,king'azi,malamba mawili,kibamba ni aibu maeneo hayo na serikali hauna hata habari,inafikiria kuongeza v8 za ma rc!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…