Hivi Mtanzania akikwambia anafika muda si mrefu huwa anamaanisha yupo umbali kiasi gani?

Hivi Mtanzania akikwambia anafika muda si mrefu huwa anamaanisha yupo umbali kiasi gani?

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
11,931
Reaction score
15,849
Hello JF,

Kuna haka katabia ka sisi Wabongo kutokuwa wakweli pindi tunapokuwa na miadi na wenzetu, mimi leo yamenikuta.

Kuna jamaa nilikuwa na miadi ya kukutana naye asubuhi ya leo saa moja kamili, sasa mimi nimefika eneo la tukio on time, lakini jamaa yeye mpaka sasa hajafika na kila nikimpigia anasema anafika muda si mrefu.

Sasa nimetafakari nikaona niulize humu: Hivi Mtanzania akikuambia anafika muda si mrefu, huwa anamaanisha yuko umbali kiasi gani?
 
Kama kuna mtu unamsubiri hadi saizi bora uondoke tuu. Hii kauli imenisaidia sana kutunza muda

Wakati ambao mtanzania anaweza kuja ni pale ambapo utakua umemsubiri hadi umechoka ndio hufika.
 
Hakuna tabia ina nikera kama hii, Unakuta mna issue sensitive ya bzness afu mtu anakosa kuheshimu ratiba za wengine. Mimi kuna jamaa kaniweka jana kutwa na mi ahadi isiyotekelezeka.
 
Utanzania unaingiaje hapo mkuu? Hiyo ni shida ya jamaa yako. Ingekua ni tatizo la watanzania hata wewe usingewahi kufika hiyo saa moja. Vinginevyo wewe sio mtanzania.
 
Watanzania ni wapuuzi wa kutumia muda ipasavyo. Yaani kwenda na muda ni ngumu kwake ila kwenda sambamba na ujinga ni tunu kwake.

Wana msemo wa "nipe dakika 0 nitakuwa hapo"
 
Mkubwa huyo yupo kama 20kms away...atafika hapo 3hours late, na atakupigia kukujulisha amefika, ila hakuoni upo wapi. 😀

Everyday is Saturday.....................😎
 
Utaratibu wangu nikifika eneo la tukio namsubiri mtu dakika 15 tu, baada ya hapo naendelea na mishe zangu
 
Hivi mpaka leo huwa unamsubiri mtu?
Me nilishaachaga kitambo sana, huwa nakuambia utanikuta mbele ya safari.
 
Time management ni tatizo sugu kwa watanzania wengi mpaka viongozi.

Nilishawahi kufanya kazi kwenye miradi tofauti na foreigners mpaka walikua wananishangaa kwa kujali muda kama sio mtanzania.

Ila ilinisaidia sana kupata connection nyingi zaidi kwa wageni kila walipokuwa wakija wapo radhi kunisubiri hata kwa siku moja mbele au mbili ili tu muwe pamoja kwenye mizunguko yao.
 
Dah... kikawaida Mimi huwa simsubiri mtu zaidi ya sekunde 90 baada ya muda wa ahadi kwa mambo ya kikazi....
Na sekunde 0 kwa KE [emoji2960]

Sent using Beretta ARX 160
 
Ukiona hivyo, miadi yenu ilikuwa na unuhimu kwako kuliko kwake.
 
Hii kitu ni tabia sio jinsia kuna jamaa yangu mmoja yeye ni mara mia moja upange kukutana na mwanamke anaweza akatokea ila sio yeye. Anaweza kukuweka sehemu halafu akaahirisha kuja bila kukutaarifu ukichoka kusubiria na kumpigia simu ndio anakuambia mimi sitakuja. Ni mara moja tu tulifanikiwa kukutana baada ya kua na miadi, na ilifanikiwa kwa sababu yeye ndio alipanga na ndio alikua ananisubiria kinyume na hapo ni maumivu tu
 
Back
Top Bottom