Hivi mteja kama huyu unamjibuje?

Nakazia
 
Haitokugharimu chochote kusema hujui ikiwa hujui ama kumuelekeza kwingine endapo unajua.

Kuelekeza rizki kwa mwingine hakupunguzi rizki yako. Ikiwa hajanunua yeye atakuja kununua mwingine.
Akiwa ni mteja wangu wa kila siku hata kwenda kumchukulia naenda ila sio kwa kejeri za kupunguziwa bei kwa lazima kwani mteja ni yeye tu
 
Mjibu vizuri na tena kwa ukarimu tu ila jaribu kumfanyia marketing ya bidhaa nyingine unayoweza kumuoffer kabla hajaondoka. anaweza asinunue hapo leo ila siku nyingine akaja kwa ajili ya bidhaa nyingine uliyomgusia kuwa unaiuza
 
Mjibu vizuri na tena kwa ukarimu tu ila jaribu kumfanyia marketing ya bidhaa nyingine unayoweza kumuoffer kabla hajaondoka. anaweza asinunue hapo leo ila siku nyingine akaja kwa ajili ya bidhaa nyingine uliyomgusia kuwa unaiuza
Sawa mkuu ntajitahidi japo yule mteja nishamkosa
 
Biashara ni ushindani, inabidi uwe mpole ukizingatia mteja ni mfalme.
Biashara haitaki hasira,vipi yule mteja anaingia dukani kwako mchana,hujapata mteja tokea asubuhi anakuulizia nataka kile,unampa anatizama,anakwambia nipe kile,unamletea items kama sita hivi,halafu anakwambia basi ntapita kesho,hapo kumbuka vingine umetoa kwenye maboksi au mifuko,vingine umetumia fimbo kuchomoa juu kwenye mashelf...
 
Upande mwingine kuna wafanyabiashara wenye tamaa iliyozidi kiasi. Nimewahi kutumia nguvu kufuata bidhaa kwa muuzaji niliyewasiliana naye kwa simu kabla. Nimefika dukani na kuona bidhaa nikakuta ina utofauti kidogo na nilichokuwa nataka. Nikamuuliza kama hakunielewa nilichotaka maana nilikuwa specific naye akawa amekubali kuwa anayo hiyo. Nikabaini kuwa alinielewa ila hakutaka kupoteza mteja. Akajaribu kunishawishi nichukue nilichokuta kwake, mimi nikagoma. Nikamuuliza kama anaweza kunielekeza kwingine akaniambia wazi kabisa kuwa hawezi kufanya hivyo, ninunue kwake kilichopo au nikatafute mwenyewe.

Hapo hata suala la bei halikuwa tatizo bado, na kweli hiyo bidhaa kwa specs nilizokuwa nataka ilikuwa ngumu kidogo kupatikana maana nilishazunguka kuitafuta. Nikaamua kuzunguka zaidi na bahati nzuri duka kama la tatu tu kutoka kwake nikakuta nilichohitaji, tukabargain bei nikachukua, pamoja na vingininevyo, maana ilikuwa na kwa ajili ya kazi ya mtu. Yule wa kwanza akajikuta amejiweka kwenye 'blacklist' yangu. Kazi zikipatikana siwezi kwenda kwake tena. Wapili ni miongoni wa watu wa kwanza kuwacheki kuhusu bidhaa nikipata kazi.
 
HAKUNA SEHEMU WANAONGOZA KUANDKIA WAGONJWA DAWA ZA UONGO NA MAJINA YASIYO YA KWELI KAMA HIZO HERBAL CENTRE.. yani mteja atazunguka kila mahali siku nzima na atarudi hapo kwenye hicho kituo huwa najiuliza zile dawa ni kweli za kienyeji au wanawapa dawa za kawaida ila wnaandika majina ya ovyoo ili wagonjwa wasipate huduma nje ya kituo chao.
 
Kwaiyo mkuu angekuelekeza kwa uyo jamaa wapili na ukakuta kile unataka kesho ungerudi pale ulipopata au kwa yule aliekuelekeza?
 
Kwaiyo mkuu angekuelekeza kwa uyo jamaa wapili na ukakuta kile unataka kesho ungerudi pale ulipopata au kwa yule aliekuelekeza?
Yes. Nisingemueka kwenye blacklist. Fursa za kununua kwake zikitokea nakuwa simkwepi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…