Upande mwingine kuna wafanyabiashara wenye tamaa iliyozidi kiasi. Nimewahi kutumia nguvu kufuata bidhaa kwa muuzaji niliyewasiliana naye kwa simu kabla. Nimefika dukani na kuona bidhaa nikakuta ina utofauti kidogo na nilichokuwa nataka. Nikamuuliza kama hakunielewa nilichotaka maana nilikuwa specific naye akawa amekubali kuwa anayo hiyo. Nikabaini kuwa alinielewa ila hakutaka kupoteza mteja. Akajaribu kunishawishi nichukue nilichokuta kwake, mimi nikagoma. Nikamuuliza kama anaweza kunielekeza kwingine akaniambia wazi kabisa kuwa hawezi kufanya hivyo, ninunue kwake kilichopo au nikatafute mwenyewe.
Hapo hata suala la bei halikuwa tatizo bado, na kweli hiyo bidhaa kwa specs nilizokuwa nataka ilikuwa ngumu kidogo kupatikana maana nilishazunguka kuitafuta. Nikaamua kuzunguka zaidi na bahati nzuri duka kama la tatu tu kutoka kwake nikakuta nilichohitaji, tukabargain bei nikachukua, pamoja na vingininevyo, maana ilikuwa na kwa ajili ya kazi ya mtu. Yule wa kwanza akajikuta amejiweka kwenye 'blacklist' yangu. Kazi zikipatikana siwezi kwenda kwake tena. Wapili ni miongoni wa watu wa kwanza kuwacheki kuhusu bidhaa nikipata kazi.