Hivi mteja kama huyu unamjibuje?

Hivi mteja kama huyu unamjibuje?

Bado hujasema..

huwez kuja ofisin kwangu, nikusikilize Mimi, nijue ugonjwa wako, hujatoa hata Consultation fee, alafu dawa ukanunue kwingine .

Nitakua Sina Akili !!.

Angeenda Hosp, Hosp Huwa sio inshu, nakuandikia tu prescription unaenda mtaani kutafuta, as long as umechangia kiasi fulan Cha gharama Hosp !!.
Nakazia
 
Haitokugharimu chochote kusema hujui ikiwa hujui ama kumuelekeza kwingine endapo unajua.

Kuelekeza rizki kwa mwingine hakupunguzi rizki yako. Ikiwa hajanunua yeye atakuja kununua mwingine.
Akiwa ni mteja wangu wa kila siku hata kwenda kumchukulia naenda ila sio kwa kejeri za kupunguziwa bei kwa lazima kwani mteja ni yeye tu
 
Mjibu vizuri na tena kwa ukarimu tu ila jaribu kumfanyia marketing ya bidhaa nyingine unayoweza kumuoffer kabla hajaondoka. anaweza asinunue hapo leo ila siku nyingine akaja kwa ajili ya bidhaa nyingine uliyomgusia kuwa unaiuza
 
Sawa mkuu ntajitahidi japo yule mteja nishamkosa
 
Biashara ni ushindani, inabidi uwe mpole ukizingatia mteja ni mfalme.
Biashara haitaki hasira,vipi yule mteja anaingia dukani kwako mchana,hujapata mteja tokea asubuhi anakuulizia nataka kile,unampa anatizama,anakwambia nipe kile,unamletea items kama sita hivi,halafu anakwambia basi ntapita kesho,hapo kumbuka vingine umetoa kwenye maboksi au mifuko,vingine umetumia fimbo kuchomoa juu kwenye mashelf...
 
Upande mwingine kuna wafanyabiashara wenye tamaa iliyozidi kiasi. Nimewahi kutumia nguvu kufuata bidhaa kwa muuzaji niliyewasiliana naye kwa simu kabla. Nimefika dukani na kuona bidhaa nikakuta ina utofauti kidogo na nilichokuwa nataka. Nikamuuliza kama hakunielewa nilichotaka maana nilikuwa specific naye akawa amekubali kuwa anayo hiyo. Nikabaini kuwa alinielewa ila hakutaka kupoteza mteja. Akajaribu kunishawishi nichukue nilichokuta kwake, mimi nikagoma. Nikamuuliza kama anaweza kunielekeza kwingine akaniambia wazi kabisa kuwa hawezi kufanya hivyo, ninunue kwake kilichopo au nikatafute mwenyewe.

Hapo hata suala la bei halikuwa tatizo bado, na kweli hiyo bidhaa kwa specs nilizokuwa nataka ilikuwa ngumu kidogo kupatikana maana nilishazunguka kuitafuta. Nikaamua kuzunguka zaidi na bahati nzuri duka kama la tatu tu kutoka kwake nikakuta nilichohitaji, tukabargain bei nikachukua, pamoja na vingininevyo, maana ilikuwa na kwa ajili ya kazi ya mtu. Yule wa kwanza akajikuta amejiweka kwenye 'blacklist' yangu. Kazi zikipatikana siwezi kwenda kwake tena. Wapili ni miongoni wa watu wa kwanza kuwacheki kuhusu bidhaa nikipata kazi.
 
Kwa biashara yako wewe kwanza hauna utu!
Nimeshangazwa sana umemuandika dawa majina ya uongo na huko alipokuwa anazunguka walimwambia nini kuhusu majina ya uongo?

Kitendo cha kushindwa kumuonyesha unaondoa reputation yako, akifika sehemu nyingine atasema yule jamaa pale ana roho mbaya anasema hakuna.

Msikilize dr. Mwaka jinsi anavyopangilia maneno yake, kama unaona dalili fulani fika kituo cha afya kilicho karibu yako na ukiona kama tatizo bado linaendelea basi fika ofisini kwetu ubungo plaza. Hii sentensi wafanyabiashara wanaelewa ina maana kubwa sana.

Njoo uone kariakoo mkuu, mtu kakosa nguo fulani anaenda kuchukua kwa jirani yake anamuuzia anampa chochote, au anamwambia cheki maduka ya pale mbele utapata boss.

Unashindwa kuelewa dhana nzima ya ushindani katika biashara.
HAKUNA SEHEMU WANAONGOZA KUANDKIA WAGONJWA DAWA ZA UONGO NA MAJINA YASIYO YA KWELI KAMA HIZO HERBAL CENTRE.. yani mteja atazunguka kila mahali siku nzima na atarudi hapo kwenye hicho kituo huwa najiuliza zile dawa ni kweli za kienyeji au wanawapa dawa za kawaida ila wnaandika majina ya ovyoo ili wagonjwa wasipate huduma nje ya kituo chao.
 
Upande mwingine kuna wafanyabiashara wenye tamaa iliyozidi kiasi. Nimewahi kutumia nguvu kufuata bidhaa kwa muuzaji niliyewasiliana naye kwa simu kabla. Nimefika dukani na kuona bidhaa nikakuta ina utofauti kidogo na nilichokuwa nataka. Nikamuuliza kama hakunielewa nilichotaka maana nilikuwa specific naye akawa amekubali kuwa anayo hiyo. Nikabaini kuwa alinielewa ila hakutaka kupoteza mteja. Akajaribu kunishawishi nichukue nilichokuta kwake, mimi nikagoma. Nikamuuliza kama anaweza kunielekeza kwingine akaniambia wazi kabisa kuwa hawezi kufanya hivyo, ninunue kwake kilichopo au nikatafute mwenyewe.

Hapo hata suala la bei halikuwa tatizo bado, na kweli hiyo bidhaa kwa specs nilizokuwa nataka ilikuwa ngumu kidogo kupatikana maana nilishazunguka kuitafuta. Nikaamua kuzunguka zaidi na bahati nzuri duka kama la tatu tu kutoka kwake nikakuta nilichohitaji, tukabargain bei nikachukua, pamoja na vingininevyo, maana ilikuwa na kwa ajili ya kazi ya mtu. Yule wa kwanza akajikuta amejiweka kwenye 'blacklist' yangu. Kazi zikipatikana siwezi kwenda kwake tena. Wapili ni miongoni wa watu wa kwanza kuwacheki kuhusu bidhaa nikipata kazi.
Kwaiyo mkuu angekuelekeza kwa uyo jamaa wapili na ukakuta kile unataka kesho ungerudi pale ulipopata au kwa yule aliekuelekeza?
 
Kwaiyo mkuu angekuelekeza kwa uyo jamaa wapili na ukakuta kile unataka kesho ungerudi pale ulipopata au kwa yule aliekuelekeza?
Yes. Nisingemueka kwenye blacklist. Fursa za kununua kwake zikitokea nakuwa simkwepi.
 
Back
Top Bottom