Swali zuri. Habari za wakati huu ni njema, na asante sana kwa kunipa pole ya majukumu, pole na kwako pia mkuu.
Kimsingi, huo ni utaratibu tu uliowekwa kisheria bila kujali misingi ya udini; kwamba kwasababu ni waislamu basi wawe na taratibu nyepesi, na wakristo wawe na mlolongo mrefu, ingeweza hata kuwa vice-versa. Hata hivyo, mawakili hawaruhusiwi kutoa uwakilishi katika Mahakama za Mwanzo, na ndiyo maana ukiwa na kesi Mahakama ya mwanzo ukataka kuweka wakili basi ni sharti uombe kuhamisha kesi hiyo iende Mahakama ya Wilaya/Mahakama ya hakimu mkazi.
Nilisahau kumalizia kwenye comment yangu ya msingi, kwamba akishapata ile hati ya usimamizi wa mirathi kutoka Mahakamani basi ataandika barua na kuipeleka kwenye mtandao husika wa simu huku akiiambatanisha hati yenyewe. Fedha zitatolewa na atapatiwa msimamizi wa mirathi kwa minajili ya kuzigawa kwa warithi wa marehemu. Asante.