Hivi mtu akifariki humu mnajuaje?

Hivi mtu akifariki humu mnajuaje?

Beesmom

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
17,202
Reaction score
28,732
Sijaanza leo kujiuliza, hivi kwa mfano MTU akapotea ghafla katika utoaji thread,uchangiaji wa mada, tunawezaje kutambua taarifa zake. Maana sijawahi ona watu kushtuka humu ndani MTU anapopotea ghafla afu mazima.

Mi naamini hata kama hatufahamiani lakini kuuliziana hali ni jambo jema na kiutu tu ambalo halihitaji gharama. Naamini pia tupo watu humu ndani twafahamiana vema kabisa hivyo tunapojuliana hali ni rahisi pia kujibiwa maswali yetu.

Hivyo hii ni nafasi yetu ya kutambua wenzetu waliopotea kusikojulikana kutambua waliko.
 
Changamoto ya humu ni kwamba, hata kama mnaishi chumba kimoja huwezi kujua mwenzako anatumia jina gani.

Inawezekana mtu na mpenzi wake wote wamo humu ila hawajuani.

Kiufupi mtu anajijua mwenyewe na akifa pia anajijua mwenyewe. Inawezekana wewe mtoa post ni mwanangu, siku ukifa siwezi nikatangazai humu kwamba to yeye amefariki na hali sijui kama unatumia jina hilo.
Kiufupi kwa humu unajijua mwenyewe kama umekufa.

Labda mitandao mengine huku ya wakona facebook.
 
Maisha ni safari,atakayekufa ujue huyo mwendo ameumaliza,
huwezi kujua kama kuna member kafa coz watu humu wanatumia fake ID's labda kwa wale wanaojuana tu.
 
Humu watu hawafi huwa wanatoweka tu,kufa wanakufa mitandao mingine.au huko mitaani.
 
Kama hutaki kuwapatia number huko PM watakujulia vipi Hali? Ili yakitokea Kama hayo mfahamu kwa urahisi?
 
Back
Top Bottom