Hivi mtu anakuwa katika hali gani ya akili hadi anakubali kuolewa mke wa tatu, wa nne nk?

Mleta mada kama wewe ni mkiristo hebu kasome πŸ‘‰ Isaiah 4:1
 
Wabongo wanaangalia hela tuu vichwa dishi zimeshayumba. Kama yuko tayari kutembea na mume wa mtu kwakuangalia hela,atakataaje kuolewa
 
Mleta mada kama wewe ni mkiristo hebu kasome πŸ‘‰ Isaiah 4:1
Kwa hiyo kila mwanamke aliekubali kuolewa mke wa pili au wa tatu au wa nne alikuwa desperate alikosa mwanaume kwa sababu fulani au kuwa na sifa mbaya akaamua kujishikisha mahali kwa nguvu?
 
Wana matatizo tu, huo ndio ukweli. Mwanamke mzuri tabia nzuri utakosajemme wako peke yako hadi uamue kwenda kubanana kwa mume wa mwenzio? nz ujue hadi anaolewa mke wa tau au wa nne alishakuwa mchepuko muda mrefu tu, hatimae mwanaume ananogewa, na anaanza kumlinganisha na mke au wake zake anaamua kumuoa kabisa.
 
Enyi wake, mume wako akikuambia anataka kuoa mke wa pili au wa tatu sijui, elewa wazi huo umekuwa mchepuko wake wa siku nyingi, huenda sasa una mimba hana namna!
 
Na ukitaka kujua kuwa hizo ndoa zinafuata mali subiri jamaa afilisike kidogo tu utaona kila mwanamke anakula kona.
 
Kwani mwanamke akiwa mke wa tatu au wa nne anapoteza nini kwa Mfano. Mwanaume kuwa na wake watatu au wanne anatumia nguvu na akili nyingi katika mahusino huwa ni mwanaume zaidi. Actual wanawake wakiondowa wivu wengi watakuwa wanalazimisha waume wao waowe wake wengi zaidi.

Wewe fikiria kwa mfano, mwanaume qliye kamilika anahitaji sex three times a day hapo hapo anahitaji kupikiwa, na anye mpikia ni mjamzito na anamtoto wa miaka mitatu , sasa kati hali kama hiyo ni mwanamke gani hatamani msaidizi katika kila eneo?
 
Uchunguzi wa kimatibabu unadokeza athari kadhaa zinazowapata wanawake wanaoolewa mke wa tatu na kuendelea
  • Kutojithamini na kujiona hapendwi na watu
    • Anaweza kukabiliana na hisia za kutostahili, kuwa "mtu mdogo" kuliko wengine, au kuona thamani yake sio kubwa, hana kitu cha kuwafanya watu wamthamini na kuwa na hasira na watu akiona hawamthamini au kumkubali
  • Wivu na ushindani
    • Hata katika tamaduni ambazo mitala ni kawaida, wivu kati ya wake wenza ni jambo la kawaida sana. Wivu wa kudumu unaweza kusababisha wasiwasi na unyogovu hata anaposhughulika na watu wengine.
  • Aibu ya ndani au hatia
    • Hasa ikiwa uamuzi wa kuwa mke wa tatu ulisukumwa na shinikizo la nje (familia, mahitaji ya kifedha, matarajio ya jamii), anaweza kupata hatia au aibu inayoendelea, wakati mwingine akiiona jamii inamkuhumu wakati wote na kuwa na mtazamo hasi kwao
  • Kupoteza hali ya utambuzi
    • Ikiwa ana maadili yanayokinzana (k.m., kuamini ndoa ya mke mmoja inayotegemea upendo lakini kukubali mitala kwa ajili ya kuendelea kuishi au matarajio ya familia), mvutano wa kisaikolojia unaweza kusababisha migogoro ya muda mrefu ya kihisia na kutoridhika maishani mwake
Kwa ufupi ni kwamba, kuna athari za kisaikolojia mtu anaekubali kuolewa mke wa tatu au ne nk
 
 

To the husband or wives?πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Ya kwamba umshangae mtu anaye taka kuolewa uke wenza ila hutomshangaa mwanamke kuliwa hovyo hovyo mwisho wa siku anazaa watoto wasio julikana baba zao wako wapi?
Kuna wanawake kwenye ndoa wanazaa na wanaume wa nje
 
Mkuu,

Kula vyakula vyenye mafuta pia kunaongeza uwezekano wa magonjwa ya moyo.

Utapiga marufuku kula vyakula vyenye mafuta pia?
Hakuna mtu anayetaka au hata anayeweza kupiga marufuku polygamy kwenye jamii kama ya kitanzania ila ni vyema watu wakawa na taarifa na maarifa kuhusu hili jambo waamue wenyewe. Ni kama vile unavyopewa onyo kwenye sigara ili unaivuta ukijua matokeo yake yanaweza kuwaje.
 
Hakuna mtu anayetaka au hata anayweza kupiga marufuku polygamy kwenye jamii kama ya kitanzania ila ni vyema watu wakawa na taarifa na maarifa kuhusu hili jambo waamue wenyewe.
Watu wengine washajua hayo yote mnayoyasema ila wameamua tu kuwa polygamist kwa sababu zao, msiwafanye wote walioamua kuwa polygamist ni wajinga wasio na taarifa.
 
Watu wengine washajua hayo yote mnayoyasema ila wameamua tu kuwa polygamist kwa sababu zao, msiwafanye wote walioamua kuwa polygamist ni wajinga wasio na taarifa.
Wote wanaovuta sigara ni wajinga wasio na taarifa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…