Hivi mtu anakuwa katika hali gani ya akili hadi anakubali kuolewa mke wa tatu, wa nne nk?

Sio sawa kwa muktadha gani?

Mtu anaweza kukuambia wewe kumpangia yeye aoe vipi au azae vipi ndiyo jambo lisilo sawa hapa.
Sio kumpangia, nimeelezea mtizamo wengi. Nikisema sio vizuri mtu kuvuta sigara sijampangia bali nimeelezea tu mtizamo wangu na wa sayansi.
 
Mtizamo gani wa sayansi unatuonesha jambo hilo ni baya?
 
We unasema mke wa tatu!!!!!

Kile kipande kilichoandikwa kwenye bilblia kuwa wanawake 7 wataomba mwanaume 1 awe mume wao, wapo tayari kujifanyia kila kitu lakini walau waitwe kwa jina lake
Je unamkumbuka mke wa mwisho wa mfalme Solomoni yani mke wa elfu............

Kuolewa kwetu haibebi mapenzi peke yake ni heshima, staha na hitaji la asili kwa mwanamke hasa ukiitafakari kwa upande wa dini inaaminika kuwa mwanzo wa mwanadamu Mungu alimuumba kwa mfano wake, mtu mume akaumbwa na vingine vyote baada ya huyo mtu kuwa mpweke akaona ampe mwenzie, na kwa kumchomoa ubavu ile awe nyama na mifupa katika mwili wake,, ndipo hapo tukatokea sie wanawake,,

Kwahiyo sisi wanawake hatukuwa katika mpango wa Mungu tangu mwanzo ila tumekuja baada ya mwanaume kukosa balance huko bustanini,, kwahiyo unapokuja mjadala wa kuolewa kwa mwanamke ni jambo la tofauti kidogo na wewe unavyofikiri,

Japo pamoja na yote mwanaume maskini hayupo kwenye kundi la kuoa wake wengi hivyo,, kwahiyo tafuteni kwa bidii zote
 
Mwanaume unalalamikaje mwanamke kuolewa mke wa pili ama wa 3?

Yaani wewe unaumia wanawake kuolewa mke wa pili ama wa 3?

Kwa hiyo unaona bora aendelee kua mchepuko kuliko kua na mwanaume wa uhakika wa kumhudumia na kumstiri?
Mimi pia nimejiuliza huyu mwanaume anapojiweka nafasi ya mwanamke na kukataa kuolewa mke wa tatu au wa nne ila at least anakubali kuolewa mke wa pili.
Nimeshindwa kuelewa.
 
Juzi hapa nilikuwa Uturuki. Ni nchi ya watu ambao dini yao inaruhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini wanawake katakata hawakubali kuwa katika ndoa ya mke zaidi ya mmoja, na wanaume wao wanaelewa hilo. Nimewaheshimu sana wanawake wa Uturuki kwa kujitambua kwa namna hii.

Hili ni jambo ambalo siku zote nimeshindwa kuwaelewa wanawake, na wala mtu asiniambie dini yangu inaruhusu. Mwanamke anakuwa katika akili gani hadi anakubali kuolewa kama mke wa pili, au wa tatu?

Kuolewa mke wa pili bado naona kama ningekuwa mwanamke nisingekubali kamwe, sasa wa tatu? Wa nne? Kwamba unakuwa na shida sana ya kupata mwanaume wako au una hali mbaya ya kiuchumi ndio ukakubali?

Na siamini kabisa kwamba yule mwanamke unaemkuta kwa huyo mumeo anafurahia kitendo cha wewe kuja kama mke wa pili au mbaya zaidi, wa tatu au wa nne.

Kwa nini wanawake hamtaki kujikomboa katika jambo hili? Sidhani kama nitamheshimu mwanamke anaekubali kuolewa mke wa tatu au wa nne; labda kidogo wa pili nitamuelewa. Mie naona kama anaekubali kuingilia ndoa ya wengine ambayo tayari ina mke mmoja au wawili kufikiri kwake hakupo sawa.

Nadhani ni Safari Sound au Marquiz waliwahi kuimba, "kama nitakuwa mke wa pili nakubali, lakini kama ni watatu sikubali hata kidogo nasikitika"
Jibu:
 
We unasema mke wa tatu!!!!!

Kile kipande kilichoandikwa kwenye bilblia kuwa wanawake 7 wataomba mwanaume 1 awe mume wao, wapo tayari kujifanyia kila kitu lakini walau waitwe kwa jina lake
Je unamkumbuka mke wa mwisho wa mfalme Solomoni yani mke wa elfu............

Kuolewa kwetu haibebi mapenzi peke yake ni heshima, staha na hitaji la asili kwa mwanamke hasa ukiitafakari kwa upande wa dini inaaminika kuwa mwanzo wa mwanadamu Mungu alimuumba kwa mfano wake, mtu mume akaumbwa na vingine vyote baada ya huyo mtu kuwa mpweke akaona ampe mwenzie, na kwa kumchomoa ubavu ile awe nyama na mifupa katika mwili wake,, ndipo hapo tukatokea sie wanawake,,

Kwahiyo sisi wanawake hatukuwa katika mpango wa Mungu tangu mwanzo ila tumekuja baada ya mwanaume kukosa balance huko bustanini,, kwahiyo unapokuja mjadala wa kuolewa kwa mwanamke ni jambo la tofauti kidogo na wewe unavyofikiri,

Japo pamoja na yote mwanaume maskini hayupo kwenye kundi la kuoa wake wengi hivyo,, kwahiyo tafuteni kwa bidii zote
Huyu mleta mada ni mpuuzi tu!
 
Pesa siyo sababu kwa wote! Wapo wameolewa ndoa za mitala na wanaume masikini.
 
Mimi siyo akili gani, nikipenda mtu nilivyo na wivu siwezi kwa kweli. Yaani najua sasa hivi yuko analala huko, mbona usiku utakuwa mrefu sana.
😂😂😂😂😂😂😂 Kikubwa ni kumiliki fedha tu ili uwe unalala na wakwako tu pekee.
 
Mtizamo gani wa sayansi unatuonesha jambo hilo ni baya?
Kisayansi ni jambo zuri zaidi binadamu kuwa na genes zilizotawanyika kuliko genes zinazofanana kukusanywa sehemu ndogo, polygamy ina limit mtawanyiko wa genes na hivyo kuongeza uwezekano wa magonjwa ya kurithi na viumbe wasio na afya nzuri sana.

Lakini pia katika social science polygamy ni mfumo wa hovyo unaompa mwanaume uhuru wa kufanya mambo ambayo mwanamke haruhusiwi kufanya, kama lingekuwa ni jambo zuri lisilo la kimfumo dume mwanamke naye angeruhusiwa kuoelewa na wanaume wengi kwa wakati mmoja.
 
Mtizamo gani wa sayansi unatuonesha jambo hilo ni baya?
Jambo lingine baya kuhusu polygamy kama ikizingatiwa vizuri ni kwamba inapunguza sana uwezekano wa wanaume wengine wasio na hadhi kubwa kicheo, umaarufu au pesa katika jamii kupata wenza wazuri.
 
Nimefuatilia hiii wamwtuzidi 1m tu...31mil kwa 30mil...siowengi hivyo lama nilivyowaza....labda kwa tofauti ya 5m
Hapo bado hujaweka wanawake ambao wako zaidi ya miaka 45 ambao hawawezi kuzaa tena.
 
Juzi hapa nilikuwa Uturuki. Ni nchi ya watu ambao dini yao inaruhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini wanawake katakata hawakubali kuwa katika ndoa ya mke zaidi ya mmoja, na wanaume wao wanaelewa hilo. Nimewaheshimu sana wanawake wa Uturuki kwa kujitambua kwa namna hii.

Hili ni jambo ambalo siku zote nimeshindwa kuwaelewa wanawake, na wala mtu asiniambie dini yangu inaruhusu. Mwanamke anakuwa katika akili gani hadi anakubali kuolewa kama mke wa pili, au wa tatu?

Kuolewa mke wa pili bado naona kama ningekuwa mwanamke nisingekubali kamwe, sasa wa tatu? Wa nne? Kwamba unakuwa na shida sana ya kupata mwanaume wako au una hali mbaya ya kiuchumi ndio ukakubali?

Na siamini kabisa kwamba yule mwanamke unaemkuta kwa huyo mumeo anafurahia kitendo cha wewe kuja kama mke wa pili au mbaya zaidi, wa tatu au wa nne.

Kwa nini wanawake hamtaki kujikomboa katika jambo hili? Sidhani kama nitamheshimu mwanamke anaekubali kuolewa mke wa tatu au wa nne; labda kidogo wa pili nitamuelewa. Mie naona kama anaekubali kuingilia ndoa ya wengine ambayo tayari ina mke mmoja au wawili kufikiri kwake hakupo sawa.

Nadhani ni Safari Sound au Marquiz waliwahi kuimba, "kama nitakuwa mke wa pili nakubali, lakini kama ni watatu sikubali hata kidogo nasikitika"
Siku hizi hata wanaume wanaolewa ungejaribu kuwa wa pili au watatu ili upate eksipiriensii
 
Back
Top Bottom