Hivi mtu anakuwa katika hali gani ya akili hadi anakubali kuolewa mke wa tatu, wa nne nk?

Mwanaume unalalamikaje mwanamke kuolewa mke wa pili ama wa 3?

Yaani wewe unaumia wanawake kuolewa mke wa pili ama wa 3?

Kwa hiyo unaona bora aendelee kua mchepuko kuliko kua na mwanaume wa uhakika wa kumhudumia na kumstiri?
Inashangaza kuwa mwanamme anakuwa na mke mmoja na wanawake (side chicks) wawili, watatu mpaka wanne, lakini hiyo siyo neno kwao. Na wala wasitudanganye hata huko Ulaya na Marekani tabia za wanaume ndiyo hizo hizo za kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja (hata huyo Trump mwenyewe si ndiyo hivyo tena).

Na wala asitudanganye vya Uturuki, mimi mkwe wangu ana asili ya huko na baba yake alikuwa na wake wawili. Labda aseme kwao siyo kawaida kama huku kwetu.
 
Ndoa ni scam tuepuke kupangia watu kufanya mambo yanayowapa furaha! Wafalme kina Suleiman na wengine chungu nzima wa kiafrika walikuwa na wake wa kutosha tu na hawakuwa na makaratasi toka kwa padri, shekhe wala DC.
As long as wana furaha na maisha yanaenda inatosha
 
NB
Hakuna aliyelezimishwa, kama huwezi tulia
Katika kulazimishwa wengi wanalazimishwa either na msukumo wa jamii; utamaduni au hata arranged marriages.., na hii hata historically na hata kwa wafalme walikuwa wanapeleka watoto wao kuolewa sehemu fulani ili mfalme kupata mshirika wa kivita au kuongeza himaya yake au kupata mtu wa kumlinda asishambuliwe na wengine...

In short wanawake walikuwa bidhaa / commodities kama commodity nyingine yoyote katika mfumo dume.
 
Acheni kulazimisha mwanamke na mwanaume wafanane, nyinyi ndo mmewafanya wanawake wa kisasa kujilinganisha na wanaume mwisho wa siku wanaangukia pua ,huyo mwanamke akiruhusiwa kuolewa na wanaume watatu kwa wakati mmoja na wote wakataka watoto ataweza kuwabebea hizo mimba kwa wakati mmoja?
Mwana mke na mwanaume ni watu wawili tofauti na wana majukumu tofauti kabisa ndani ya dunia hii ila kwasababu nyinyi wanaharakati uchwara mnajifanya kujua zaidi ya mungu aliye umba binadamu hilo sio shida yake.

Utofauti wa mwanamke na mwanaume upo kimaumbile na hawawezi kuwa sawa kama nyinyi mafemenist mnavyo jaribu kuaminisha watu ,na ndio maana mwanamke anaweza,kubeba mimba, kuzaa, kunyonyesha, wakati mwana mme hawezi ,na ndio maana mwanaume anaweza kuwabebesha mimba hata wanawake 100 kwa wakati mmoja lakini mwanamke hana uwezo wa kubeba mimba za watu wawili kwa wakati mmoja.
Mwanamke anaingia kwenye hedhi wakati mwanaume haingii kwenye hedhi, mwanamke kazaliwa na bikra mwanaume hana hiyo bikra, mwanamke ana matiti makubwa wakati mwanaume hana, mwanamke ana k na mwanaume ana mboo sasa watu wenye tofauti kubwa kimaumbile kiasi hichi utalazimishaje wawe sawa katika majukumu na haki za kiulimwengu?
Suala la mwanaume kuruhusiwa kuoa zaidi ya mwanamke mmoja,na mwanamke kukatazwa kuwa na mwanaume zaidi ya mmoja zaidi ya mmoja lipo kimaumbile zaidi ?
 
Mimi pia nimejiuliza huyu mwanaume anapojiweka nafasi ya mwanamke na kukataa kuolewa mke wa tatu au wa nne ila at least anakubali kuolewa mke wa pili.
Nimeshindwa kuelewa.
Kwa sababu huwa huelewi siku zote
 

Hisia tu kuna data za kuthibitisha haya?
 
Huyu Raisi wetu Samia ni mke wa tatu? Unatutania Mkuu.😳😳😳😳😳😳

Kweli kabisa wala sio utani.
Hebu nikuulize. Tuseme wewe dada yako kwenye familia, au mtoto wako wa kike, anakuja kuwaeleza nimepata mchumba. Mnafurahia, nk. Halafu mnapomdadisi zaidi anawaambia mchumba wangu tayari ana wake wawili mie naenda kuwa mke wa tatu, hivi mtajisikiaje? Nadhani wengine mtaona hayuko sawa katika kufanya maamuzi sahihi, sivyo?

Sasa nikuambie mshangao wangu unatoka wapi - kwamba mtu anaeamua kuwa mke wa tatu bila kuona tatizo ndio anatuamulia mambo mazito ya nchi yetu, kweli anaweza kuwa anafanya maamuzi sahihi? Nimesema hapo juu sidhani utakutana na mwanamke Mkurugenzi, Waziri nk, ambae ni mke wa pili au wa tatu. Hiwa hawana uwezo wa kufika huko.

Mie naona ni sawa na kuwa umemwona dereva anafanya maamuzi ya ajabu sana akiendesha gari Dar, halafu unaamua huyo ndio atuendeshe safari ya kwenda Arusha!
 
Hisia tu kuna data za kuthibitisha haya?
Nipe mfano mmoja tu!

Anyway, kuna mtu kanishangaza kwamba Raisi wetu ni mke wa tatu. Basi naona kwenye siasa inawezekana.

Wewe binti yako akija akasema amepata mchumba, ni mume wa wake wawili tayari utajisikiaje? Utaona ana uwezo wa kuamua mambo sawa?
 

We ndio mwenye hoja kiongozi, tupatie data za kuprove hayo mambo ya kisirani na mengine kwamba yanasababishwa kuwa kwenye ndoa za wake wengi! Kama hamna statistics basi na ibaki kuwa hisia tu ya kimapokeo. Ndoa za wake wengi zilianza kupungua sana miaka ya 70 tu hapa majuzi baada ya brainwashing ya kutosha toka kwa wazungu!
 
Mkuu,nimeishi sana na jamii zenye wanaume wenye wake zaidi ya mmoja, Tanzania na hata Nigeria. Yaani wee acha tu. Wanawake walioolewa kama mke wa pili, wa tatu nk, wana issues sana za kisaikolojia
 
Mkuu,nimeishi sana na jamii zenye wanaume wenye wake zaidi ya mmoja, Tanzania na hata Nigeria. Yaani wee acha tu. Wanawake walioolewa kama mke wa pili, wa tatu nk, wana issues sana za kisaikolojia

Probably sababu zingine nyingi pia zipo, ni ngumu sana kuprove tuseme ina uhusiano bila conclusion, sisi tuliozaliwa kwa familia za baba mwenye wake wengi na tukaishi kwenye upendo na kufanikiwa maisha yetu hatuoni tatizo lolote! Na hatuamini kwenye ndoa zilizoletwa na waarabu na wazungu! Baba yangu angekuwa na mke mmoja nisingekuwepo duniani kabisa, na tumezaliwa wengi na wote tuna mahusiano mazuri kwa kuwa baba yetu aliwaongoza wake zake na ndugu tukawa pamoja bila kujali katoka kwa nani!

So mwanamke anaongozwa na mumewe tu, ukitaka awe kiburi ni kwamba kimeundwa na mumewe kimsingi unamfanya awe alivyo wewe, hata wakiwa 10
 
Amini unachokiamini wewe na waache wengine waamini wanavyo amini kwenye iman yao🙎🏾
 
Asante kwa ufafanuzi huu nimeelewa mkuu, kwanini wewe ushtushwe na hilo. Thanks.
 
Sio kweli huko ndiko wanaoa sana
 
Kwani wewe ni mke wa ngapi?
 
Hapa tatizo ni dini fulani, kwa nini uchukie wa tatu na wanne TU bila kuchukizwa na mila za makabila ya kiafrika ambao huoa bila kikomo, mbaya zaidi mke wa kwanza anapewa haki zaidi kuliko wake wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…