Asalaam Aleykum wana JF wenzangu.
Rejeeni mada tajwa hapo juu.
Mimi nikiwa kijana Mzalendo wa Kitanzania, huwa ninakerwa sana na baadhi ya wabunge akiwemo Joseph Kasheku aka Musukuma hasa kwa tabia zao za kuwaona wale wenye maoni ya tofauti na serikali (au maoni yao wenyewe) kama ni wajinga, waharifu n.k.
Hii imejidhihirisha pia juzi ambako baadhi ya video clips zinamwonesha akivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwashughulikia wale wanaopinga mpango wa serikali kuzimilikisha/kuzibinafsisha bandari zetu.
Hivi kweli hiyo ni akili kweli?!
Kwa hiyo kwa mtizamo wa Musukuma, anataka sisi wananchi wa kawaida tukae tu kimya hata pale tunaona mambo hayaendi sawa?
Je, huo ni uzalendo au ni ujinga?
Kwa ninavyojua, Mzalendo ni yule ambaye yuko tayari kufa akiitetea nchi yake kwa hali na mali.
Hivyo Musukuma badala ya kuwashambulia wale wenye maoni ya tofauti na yake kuhusiana na suala la Bandari, kwanza kabisa angewapongeza kwa uzalendo na mapenzi yao mema kwa kwa nchi yao, na pili angejielekeza zaidi kwenye kuwaelimisha zaidi wananchi (nikiwemo pia) juu ya umuhimu wa kumilikisha Bandari zetu kwa wageni, na faida za kiuchumi, ulinzi na usalama kwa nchi yetu zitakazopatikana..
Nahitimisha kwa kumtaka Musukuma pamoja na wabunge wenzake wenye tabia hiyo, watuache Watanzania wenzao pale tunapokuwa tunatoa maoni yetu juu ya nchi yetu. Tanzania ni yetu sote. Hivyo sote tunawajibika katika kuilinda na kuitetea nchi yetu.
Ahsanteni sana.