Jamani boxing ina kanuni zake
Boxing ni BURUDANI na sio kuuana
Kama bondia anapigwa ngumu mfululizo bila majibu na amepoteza balance ni wajibu wa refarii kumaliza pambano, na sio kusubiri hadi bondia apate kipigo cha mbwa koko ndio amalize pambano hii sio vita
Maamuzi ya refa ni pamoja na kujaribu kuzuia maximum damage kwa bondia pindi anapokosa balance anaposhambuliwa
Waswahili walisemaga Nabii hakubaliki kwao.
Watu wanahoji ujinga mwingi sio kwasababu wameona kwa hakika refarii kampendelea Mwakinyo.......HAPANA
Wanahoji kwa sababu hawaamini kama Mtz annaweza kuwa bondia bora kwa level aliofikia Mwakinyo
Unapo angalia kitu kwa jicho la husuda, chuki, visasi hakika utaona kile tu unachokitaka........NEGATIVITY
Wengi wana muhukumu Mwakinyo kwa tambo zake lakini ukweli utabakia kuwa Mwakinyo ni BORA kwa alipofikia sasa, na sio kwasababu kabebwa au kaletewa bondia mchovu. .....UWEZO
Kuna watu wanachotaka wao ni Mwakinyo APIGWE TU ili wa mprove wrong kwasababu ya maneno yake ya tambo