mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 7,074
- 5,486
Kwani huyu yupo huru, si alifungwa baada ya kuua? Mademu wa Kichagga sijuwi ni nani aliyewaroga kuwa matapeli wa mapenzi?Nimemkumbuka huyu mwandishi wa habari wa zamani ITV siku hizi simuoni jamani mwenyewe information zake au alishastaafu?
Pesa mbeleKwani huyu yupo huru, si alifungwa baada ya kuua? Mademu wa Kichagga sijuwi ni nani aliyewaroga kwa utapeli wa mapenzi?
Aisee! Ni hatari ila Nimepata mwanga.Ni story ndefu na ilikuwa wazi kwenye vyombo vya habari.
Kwa kifupi sana Ufoo Saro alikuwa ripota maarufu na kipekee wa ITV katika matukio ya kusisimua hususani Dar katika siasa, na watu wengi tulimuona kama mwanamke aliyetulia na kujiheshimu mpaka siku yaliyomkuta yakajulikana!
Kilichotokea ni kuwa, kumbe Ufoo Saro alikuwa anadanga na jamaa mmoja hivi anaitwa Mr. Mushi (nadhani jamaa mjeshi? Usalama? ambaye alikuwa yuko special UN mission huko Darfur), sasa jamaa akawekeza pesa zake ikiwemo kujenga nyumba na kummilikisha Ufoo Saro, nyuma ya pazia kumbe Ufoo Saro alikuwa na mishe zake zingine za siri, mkorofi na huku akitaka kumdhulumu msela, sasa jamaa kwa kuwa alikuwa amekolea kwa Ufoo Saro akawa mara kwa mara anatafuta suluhu na mama yake Ufoo saro akiwa msuluhishi, lakini msuluhishi (Mama wa Ufoo Saro) alikuwa akimpendelea binti yake kwa kuwa walikuwa na njama moja ya kumdhulumu msela. Siku moja Msela alipogundua hilo akachukua bunduki (pisto?) kisiro akijifanya anakwenda kusuluhishwa akatinga nyumbani kwa kina Ufoo Saro kwa nia ya kuua wote. Akampiga risasi Ufoo Saro tumboni, akamlamba risasi mama Ufoo Saro kichwani na kufa, akijua kazi imekwisha naye akajiua kwa kujipiga risasi kichwani/mdomoni?. Bahati nzuri Ufoo Saro hakufa.
Jasho la Mtu huwa haliendi bure hasa pale ukiamua Kundhulumu chake na kitakachofuata ni Wewe Kulaanika, Kutaabika na Kuathirika Kisaikolojia ambako kutakupelekea Ufanisi wako wa Kiutendaji kufungua, Kudhoofika, Kukosa Amani na Kumsubiria tu Israeli Mtoa Roho afanye yake Kwako na ukakutane mbele ya Safari ( Mavumbini ) na yule Uliyemdhulumu kwa Kushirikiana na ama Ndugu au Wazazi au Mzazi. Karma haiepukiki kwa Wanadamu Makatili na Wadhulumati.Nimemkumbuka huyu mwandishi wa habari wa zamani ITV siku hizi simuoni jamani mwenyewe information zake au alishastaafu?
Nimemkumbuka huyu mwandishi wa habari wa zamani ITV siku hizi simuoni jamani mwenyewe information zake au alishastaafu?
Hakufungwa Wala hakuwa na kesi, coz jamaa alijichukulia Sheria mkononi kwa kumuua mama mkwe, kumjeruhi ufoo na Kisha kujiua yeye mwenyewe.Kwani huyu yupo huru, si alifungwa baada ya kuua? Mademu wa Kichagga sijuwi ni nani aliyewaroga kuwa matapeli wa mapenzi?
[emoji706]Mwanamke alikuwa sawa kabisa, mwanaume ndio alikuwa fala pro-max, unawekezaje kwa mwanamke ambaye hujamuoa?!
Moja kati ya soldier mpuuzi alikuwa yule, nilimpa kongole Ufoo Saro always mwanamke akikutana na mwanaume fala lazima amuache kwenye mataa.
Kumbe alifufuka(ga)?Atakuwa bize kutafuta ama kumuandaa mtu wa kumuua tena
Dah! Lile tukio lilisababisha mshtuko mkubwa sana kwenye jamii. Na baada ya pale, hakuwahi kusikika/kuonekana tena hadharani dada wa watu.Dah! Kweli aisee. Watu tumemmisi sana. Binti wa kimachame alitrend sana mitandaoni kipindi kile alipokoswakoswa kutolewa roho na bwana Mushi. Yule mwamba alidhamiria kuua Ufoo Saro, Mama yake Ufoo Saro na yeye mwenyewe. Mungu akamuokoa Ufoo Saro.
We utakuwa umezaliwa juzijuzišSamahani, elezea kidogo mkuu