Hivi Mwigulu anajua asasi za Kiraia zimeajiri watu wangapi? Aziomba hela za NGO's kutoka USAID

HAPO MAKE KWANZA NCHEKEE [emoji91]
 
Alichokifanya sio poa, vijana wengi tumeajiriwa huko hiyo miradi huwa ina nini cha zaidi ya kuongeza gharama za maisha, mfano madarasa ya uviko licha ya kufanikiwa lakini gharama za ujenzi zimepanda tangu muda ule mpaka sasa hivi, hizo fedha zikiingia serikalini kwa mtindo huo huo hali itakuaje!
 
Hiyo akili hana na hawazi maana hayamuhusu
 
Huyu mwigulu huwa anajiona ni mtu mwenye akili sana kumbe ni kasha tupu licha ya kuwa na Phd za dukani
 
Hii sasa ni tamaa! Toka Serikali Kuu (Central Goverment) ilipo chukua kodi kwenye vyanzo vya Serikali ya Tawala za Mikoa (Local Goverment) na kupeleka HAZINA. Leo wanatani za US AID 😀😀 ndio maana Watu wanamkumbuka Magu maana yeye alisema nchi inayo PESA NYINGI
 
Mmandegesi Tukeshe kuandika Proposal waje wabugie tu ASAHAU!!! Niko jikoni ....MABEBERU teh teh teh
 
Kipindi cha yule waliwaita Mabeberu leo Wanapiga magoti na kubembeleza
 
Bila Mashirika Ya nje sekta ya Afya itayumba sana nchi hii.

Yaani itayumba vibaya saana.
So Mh. Waziri jitathimini kabla ya kutaka hizo hela.

Mwisho, hii nchi kuna siku tutaelewana tu
Mafuta
Unga
Petrol
Mbolea
Umeme
Ajira
....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…