Hivi na nyie wake zenu wanawapa unyumba kwa kunung'unika kama huyu wangu?

Hivi na nyie wake zenu wanawapa unyumba kwa kunung'unika kama huyu wangu?

Isenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2024
Posts
1,985
Reaction score
5,167
Tumsifu Yesu Kristo.

Huyu mke wangu kila nikimuomba unyumba atalalamika mara aseme "Baba J" umeanza usumbufu wako.

Mara aseme kachoka, mara aseme yuko Period kumbe sio kweli, mara aseme hajisikii vizuri, mara aseme ana usingizi.

Yaani mimi tendo la ndoa napewa kama hisani wakuu.

Je, na nyie wanaume wenzangu mnapewa na wake zenu kwa manung'uniko kama huyu wangu?
 
Dalili za awali za kuwa umeoa mwanamke asiyekupenda ni kukunyima tendo la ndoa pasi na sababu za kimsingi ambazo zinatambulika kibinadamu......

Mwanamke mwenye afya njema ya mwili na akili huwa anapenda sana kufanya tendo la ndoa lakini na mtu aliyemridhia kutoka moyoni mwake......

Ukiona mkeo huna ugomvi naye na hana tatizo lolote la kiafya kimwili na kiakili lakini amekuwa msumbufu kwenye kutoa tendo la NDOA...basi ujue kuwa huyo mtu upo naye kimwili lakini kihisia yupo mbali na wewe
 
Mna muda gani tangu muoane? Je hali hiyo ya kukupimia unyumba imeanza lini? Je ni tangu muoane?

Mimi ninavyojua wanawake ndo wanapenda unyumba kuliko wanaume. Mara nyingi wao ndo wanaanza kuomba au kutengeneza mazingira ya kuliwa.

Ongea naye vizuri kuna kitu hakiko sawa na inawezekana haujampa nafasi nzuri ya kuongea ya moyoni mwake.
 
Kuna mtu anamchosha kabla Yako!!

Wengi walianza kwa visingizio kilichofuata ni kugundua usaliti na kuachana!!

Nakumbuka ilianza hivyo hivyo kwa jamaa, baadae alihama chumba, alivyotaka kujua zaidi ndio aliharibu akajikuta hawezi endelea tena simply he had to run as far as his legs could!!!

Siasa ya wanawake, watoto, mali na tendo la ndoa kwenye jamii ndio siasa inayoumiza zaidi tangu tupate uhuru!!
 
Back
Top Bottom