Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Tundu Lissu aliulizwa swali hili kama akishinda Uenyekiti halafu Wenje akashinda Umakamu itakuwaje?Mimi kwa mawazo yangu huyu wenje ni pandikizi la Mbowe tuombe mtu mwingine achukue fomu kama Heche kwa nafasi hiyo mbona kimya.
Nawatakia Krismas njema
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Ezekia Wenje atangaza kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
Akajibu kwa ukweli na uwazi in the quintessence Tundu Lissu way, kwamba itakuwa disaster. Alitumia neno hilo, disaster.
Akasema watu washawishi viongozi wanaofaa kugombea nafasi hiyo.
Nikajiuliza sana, kama yeye hajashawishi mtu anayeona anaweza kufanya kazi naye, hilo litakuwa jambo la hatari sana na kwa kweli itakuwa lack of judgement on his part.
Tundu Lissu hatakiwi kujipanga kwenye kushinda uenyekiti tu, anatakiwa kuwa na mtu kama mgombea mwenza kwenye umakamu, mtu anayeweza kufanya naye kazi vizuri.
Vinginevyo Tundu Lissu anaweza kushinda uenyekiti, halafu tukaenda kuona disaster anayoisema kwa sababu makamu ni Wenje.
Tundu Lissu akiwa mwenyekiti na akishindwa kuwa na makamu anayeweza kufanya naye kazi vizuri itakuwa ni mistake kubwa sana.