mambo mengine ni yakijamii zaidi,kwa upande huu,jamii imegawanyika katika pande mbili,kuna anayekula nyama iliyouwawa kwa namna yoyote,eidha kwa rungu,risasi,kisu,sumu,n.k pia tendo hilo laweza ambatana na tamko lolote likitegemeana na mtendaji au lisiambatane na tamko.Kundi la pili tendo la kuuwa linafanyika na mwislamu tu ambaye anatumia kisu tu,kwa maana hiyo tendo lake ni kuchinja na si vinginevyo,na kuchinja huko kunafanyika baada ya dua maalum aliyoambiwa na muumba wake atumie kabla ya kuchinja mnyama au ndege yeyote kwa ajiri ya kitoweo.
Ndio maana kiustaarabu kwa kuwa kundi la kwanza lenyewe halina shida basi jamii imeamua kuwaruhusu wale wa kundi la pili wafanye tendo hilo kwa kuwa katika familia zetu tuko mchanganyiko.
Pia ukisoma bibilia yote hutapata andiko linalofundisha namna ya kuchinja,lakini quran inaeleza ustaarabu wa kuchija kwa hiyo ndilo linalofanyika katika machinjio yetu.
Lakini kitoweo chako nyumbani kama wewe ni kundi la kwanza anaweza chinja yoyote hata kama si mwislam ila akija mgeni wako mwambie hii hajachija mwislamu kwa hiyo kwa ustaarabu na ukarimu wa mtu hutumia nyama iliyochinjwa kwa dua maalum ya mwislam ili kila mtu aweze kula.