Hivi, nani anatakiwa kuchinja nyama?

Hivi, nani anatakiwa kuchinja nyama?

Je kuna ubaya gani kula nyama ya mnyama ambaye amechinjwa baada ya kukuta ameishakufa mfano kwa ajali, au ambaye hakuchinjwa kabisa
 
kwani na waislamu ni yeyote anaruhusiwa kuchinja? Mi nachujua ni shehe ndo maana nikataja na viongozi wa imani zingine kwani najua kuna kuhusisha maombi wakati wa uchinjaji! Wewe ndo unaonekana hujasoma vizuri kwani mwanzo nimetaja mashehe na sijasema kila muislamu. Tafadhali sana nahitaji ufafanuzi wa kisheria, kijamii au kiafya. Mambo ya dini weka huko.
....usungilo....Si kweli kuwa kwa waislamu anayeruhusiwa kuchinja ni shehe tu. Ninachofahamu kila muislamu mwanaume anayefahamu utaratibu wa kuchinjia kuchinja. Nikweli kuchinja kunaambatana na maombi/sala kwa ajili ya yule mnyama anayechinjwa. Katika uislamu kuna hata exception kuwa inapotokea kwenye mazingira ambayo hakuna muislamu mwanaume anayejua taratibu za kuchinja lakini kuna mwanamke anayefahamu taratibu za kuchinja basi anaweza kufanya hivyo. Hili ni suala la kiimani zaidi kwani mapokeo yanasema hivyo. Ulichouliza kinaweza ku-apply kweli kwenye jamii isiyokuwa na waislamu ambako bado watu wanachinja kwa utaratibu waliojiwekea. So kutegemea padri, askofu au mchungaji kuchinja mnyama kisha hiyo nyama akiliwa na waumini wa dini nyingine kwa mtazamo wangu nadhani itakuwa ngumu na hasa kwa nchi kama Tz ambayo nijuavyo si ya kidini kama zilivyo zingine ambazo hata katiba inaeleza wazi kuwa nchi husika inafata imani ya dini fulani.
 
mkuu nadhani umenielewa. Tangu kuasisiwa kwa udini na jk sasa hivi watu wamefikia kuhoji kila jambo la kijamii linalofanywa na upande mmoja kwa kwa nini na wengine hawahusishwi? Ndo maana nimeuliza wanasheria, wanajamii na watu wa mifugo. Vinginevyo ningeuliza tu kwa ni waislamu ndo wachinjaji? Au ningesema nachukia nyama inayochinjwa na waislamu!

Ni swali zuri na lina mantiki ndani yake kwa jamii, nilikuelewa ndugu yangu.
 
Hii kitu mkuu falsafa yake ni "complex". Waislam wamewekewa utaratibu wa namna ya kuchinja mnyama ili awe halali
kwao kula, wakristu nahisi hawana kikwazo kinachowazuiya kula nyama kwa namna yeyote alivyochinjwa!
Kwahiyo ni bora tufuate utaratibu ambao hauna shida kwa jamii yote ili kuepusha usumbufu na pia ni ajira kwa wengine!
Mungu ibariki Tanzania.

Dah..hongeara kaka umetoa maelezo mafupi na rahisi kuelewa!atakayeendelea hapo anataka ushabiki.
 
....usungilo....Si kweli kuwa kwa waislamu anayeruhusiwa kuchinja ni shehe tu. Ninachofahamu kila muislamu mwanaume anayefahamu utaratibu wa kuchinjia kuchinja. Nikweli kuchinja kunaambatana na maombi/sala kwa ajili ya yule mnyama anayechinjwa. Katika uislamu kuna hata exception kuwa inapotokea kwenye mazingira ambayo hakuna muislamu mwanaume anayejua taratibu za kuchinja lakini kuna mwanamke anayefahamu taratibu za kuchinja basi anaweza kufanya hivyo. Hili ni suala la kiimani zaidi kwani mapokeo yanasema hivyo. Ulichouliza kinaweza ku-apply kweli kwenye jamii isiyokuwa na waislamu ambako bado watu wanachinja kwa utaratibu waliojiwekea. So kutegemea padri, askofu au mchungaji kuchinja mnyama kisha hiyo nyama akiliwa na waumini wa dini nyingine kwa mtazamo wangu nadhani itakuwa ngumu na hasa kwa nchi kama Tz ambayo nijuavyo si ya kidini kama zilivyo zingine ambazo hata katiba inaeleza wazi kuwa nchi husika inafata imani ya dini fulani.

Hata Mwanamke wa Kiislamu anaweza kuchinja sio Mwanaume tu.
 
sababu ya kuchinja ni kurahisisha mapishi ya kitoweo tu! Inakuwa haipendezi kukata mguu wa ngombe kuchukua maini..., wakati yuko hai! Hivyo basi kurahisisha ni kumuua kisha mambo mengine yanafuatia! Sasa mtu akijitokeza anataka kuchinja kama ajira mpe kisha mpe kichwa cha kuku magondi na utumbo mpe nae akafaidi! Sheria sheria sisi Wagala tunaamini sheria haina Haki!
 
Yeyote mwenye kisu anaweza kuchinja. Mi mbona mke wangu anachinja kuku, bata na hata mbuzi kama siko nyumbani. Visingizio vingine hivi ni vya kujiletea wenyewe kutokana na uroho wetu. Eti jirani akikuchinjia sharti umpelekee shingo,si upuuzi huu? Mi nimempa ruhusa mke wangu kuchinja kile akitakacho. In short, anybody mwenye kushika kisu anaruhusa ya kuchinja, hii haina miiko. Ulaya mashine ndizo zinazochinja mbona utamu wa nyama ni ule ule?

Hapa mjadala sio utamu na kubadilika ladha kutokana na kuchinja mtu fulani au la. Kadhia hapa ni suala la sheria kwamba, Waislamu wao kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao, Mwanaume au mwanamke wa Kiislamu anaruhusiwa kuchinja na nyama aliyoichinja ikawa halali kuliwa na Waislamu kama atafuata masharti yanatotakiwa katika uchinjaji kama vile kumuelekeza kibla mnyama anayemchinja na kadhalika. Sasa unaposema kwamba, ladha ni ile ile hakuna anayesema kwamba, akichinja mkristo au pagani ladha inabadilika, hapana ladha ni ile ile lakini nyama hiyo kwa mujibu wa Waislamu ni haramu kuliwa na wao. Kama ambavyo ladha ya mnyama aliyekufa kabla ya kuchinjwa yaani nyamafu na aliyechinjwa ladha yao ni moja lakini tofauti yao ni uhalali na uharamu. Kama ambavyo anayefanya kitendo cha kishenzi akambaka au kumuingilia dada yake ladha ni ile ile sawa na ya mkewe lakini kwa kumuingilia dada yake anakuwa amefanya unyama na dhambi kwani kafanya tendo lisilo halali. Mwanamke wa kimada na mkeo ladha yao moja, lakini mkeo ni halali na kimada ni haramu.
 
Yeyote anaweza kuchinja hasa ikizingatiwa kuwa hizi dini nyemelezi zimemkuta mswahili akijua kuchinja kupika na kula. Nadhani anayeweza kuchinja ni suala la mwenye mnyama. By the way, nani anastahili kuchinja samaki, nyati, Swala, Nyumbu na wengine wengi? Sijui hawa walioweka masharti ya kuchinja mfano ng'ombe kama wanao kwao zaidi ya kuwafaidi toka kwetu.

I see!
 
Hebu tupe ushahidi wa mashehe wanaochinja huko machinjioni, mimi napita pita sana vingunguti kununuwa nyama, sijakutana na shehe anaechinja huko bali nimekuta vijana ndio wanachinja huko.

Au una maana ipi unaposema "mashehe"?

Atakuwa anamaanisha mashehe ubwabwa
 
Wakristo walikuwa wanafuata utaratibu huu kwa namna ileile ya kuishi vizuri na wenzao waislamu si unajua tena wakristo hawana hiyana. Vile vitu ambavyo wanakula na wenzao hawakupenda kuwakwaza waliwapelekea waislamu iliwachinje na ili waweze kula wote. Lakini Nguruwe huwa wanachinja wenyewe kwani wenzetu kidinihuwa hawali.
 
Wanaochinja mnyama kwa ajili ya kitoweo machinjoni wala si mashehe bali muislamu yeyote mwenye kufuata dini sawa sawa anaruhusiwa kufanya kazi hio. Mnyama huwa anachinjwa kwa jina la mwenyezi mungu.
 
Hilo si suala la mashehe bali kila muislam anaejua taratibu za kuchinja anaweza kuchinja. Mnyama yoyote anataka kuchinjwa lazima jina la M/MUNGU (ALLAH) litamkwe na aelekezwe Makka (Kibla) pamoja na mambo mengine. Kama dini nyengine hazizingatii hayo isiwe tabu, tueleweshwe tu tunapofika kwenye butcher

Basi unapoalikwa kwenye harusi za maana, jihadhari na vitoweo vya huko kwa kuwa kina mama huchinja bila shida, tena wasio keketwa kama dini yako inavyoamrisha
 
yoyote mwenye ujasiri anaweza kuchinja nyama ila kijamii itategemea nyama hiyo anakula yeye mwenyewe au anamchinjia mtu. kama anachinja kwa ajili ya mtu mwingine basi imani ya mtu huyo pamoja na ya kwake ndio kitakachokuwa kigezo cha kuchinja mnyama huyo.

kama mimi yeyote tu poa.
 
Wakristo walikuwa wanafuata utaratibu huu kwa namna ileile ya kuishi vizuri na wenzao waislamu si unajua tena wakristo hawana hiyana. Vile vitu ambavyo wanakula na wenzao hawakupenda kuwakwaza waliwapelekea waislamu iliwachinje na ili waweze kula wote. Lakini Nguruwe huwa wanachinja wenyewe kwani wenzetu kidinihuwa hawali.

Una uhakika?
 
Nyama haichinjwi, mnyama ndiye anae chinjwa
 
Hoja ni kidini waislamu hawatakiwi kula Nguruwe. Lakini kama unasema wanakula sasa nani anawachinjia hiyo nguruwe.
 
Back
Top Bottom