Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Tangu siku ile nilikataa kuulizwa leo tunapika nini niliulizwa love leo nikupikie nini nikajibu pika wali na maharage yeye akanijibu bwana maharage yanachelewa kuiva kwa nini tusipike ugali na dagaa mchele wa kukaanga pumbavu uliniuliza ili iweje sasa wakati cha kupika ulishakipanga tayari
 
Kweli watu tunatofautiana. Mbona ni swali zuri sana, lenye maana kubwa ndani yake.
1. Anakupenda, anakuheshimu na anaheshimu maamuzi yako. Ni kama anavyoweza kukuuliza avae nini wakati ana nguo kabati zima.
2. Anaridhika sana na wewe na yeye anajaribu kukuimpress kuhakikisha unaridhika pia. Hizi jitihada za kutaka kukuridhisha bila shaka huwa anazifanya mpaka kitandani.
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi
Upo sahihi sana
 
Binafsi swali hilo hua halinisumbui maana niko selective sana kwny misosi na mara nyingi nakula vyakula ambavyo haviko hapo ndani kwetu.

So kwangu ni shega tu.
Mantiki ya kula vyakula msivyo navyo ndani ni nini? Kwa nini vyakula unavyopendelea visiwe katika akiba yenu ndani?
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Binafsi inaboa ila inabidi tu nimjibu wife
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi
Swali lingekuwa utapenda kula nini ili kipikwe. Sio tunapika nini?
 
Kuna mmoja alishitakiwa mpaka kwa wazazi wake. Ametembelewa na wifi, mdogo wa mumewe, Yule mgeni akamuuliza mke wa kaka yake akiwa na nia ya kusaidia kupika. Tupike nini? Mke sijui ni kiburi au nini akamjibu wifi yake, ' kamuulize kaka yako'!
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi
Siku nikitaka kula ninachokitaka nitanunua na kukileta siku hiyo hata Kama vingine vipo.
Au nitaitoa familia nzima tukale out.
 
Hahahah yan tumeshakuwa wachumba sugu tukaamua kuhalalisha ndoa halafu uwe hujui nachopenda kula. Amna mwanaume asiependa nyama na ugali bana ila tu naachoona wanawake ambao hawana interest na ubunifu jikoni ndio watu wa kuuliza uliza hili swali.
Mwanamke asiyependa kupika ndio muulizaji wa haya maswali.
Lakini wanaopenda jiko unakuta kashamaliza
 
Duuh kwamba mtu kila siku utakula ugali na nyama tu? Aisee basi mwenzenu sikujuaga kama kuna wanaume design yenu yaani mie najuaga wanaume wote wanapenda kuulizwa wanakula nini hawataki mke apike tu chochote anachojisikia kumbe nilikuwa sijui?
Mwanamke unatakiwa kuwa mbunifu, kuna wanawake wabunifu mpaka they trully amaze!
Leo atapikà wali nyama ya kusaga mara mixa culiflower vegetables. Kesho anapika style ingine ya chakula. Vitu ni vile vile ila kuna ubunifu.

Shida ya wanawake wa kibongo anajua mapishi matano tu.
Wali maharage +mchicha.
Wali + mchuzi wa nyama.
Wali + mchuzi wa samaki.
Ugali + nyama+maharage
Ugali + Samaki+ maharage

Yani utaona assortment ni nyama+samaki+mboga ya majani+ kuku.

Akiboresha ni pilau + ndizi+ nyama au kuku. Lazma ujionee tabu kupika. Kupika ni sanaa jamani. Na bado atataka akuulize maswali
 
Ndiyo cause mie najuaga hakunaga kitu wanaume wanapenda kwenye masuala ya msosi kama kuulizwa wanajisikia kula nini

Maana kwa wanaume wengine mwanamke akipika anachotaka yeye bila kumshirikisha mume anaonekana hamheshimu mumewe

Maana anaweza akapika chakula ambacho mume hajisikii kula halafu mume asifurahi wakati yeye ndiye anayetafuta hizo pesa

Hivyo mie mwanaume ambaye hataki nimuulize anakula nini mie ndiyo nampenda maana hanikomoi naamua mie nipike nini

Sababu wengine kumuuliza mwanaume kila siku anakula nini tunaona kama ni utumwa maana anaweza akataka ambacho sipendi

Kwamba kila siku utajikuta unapika vyakula anavyotaka yeye tu wakati usipomuuliza utapika vile unavyotaka wewe na atakula tu
Hivi unaweza ukakaa na mumeo mwaka mzima usijue vyakula ambavyo anavifurahia...Like serious?
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.

Hii swali ya kawaida sana.....siku za weekend unazokua home kwa mtu anae kujari lazima akuulize utataka kula nn siku hiyo ambacho kitakua tofauti na unachukula ukiwa kibaruani!
 
Hii swali ya kawaida sana.....siku za weekend unazokua home kwa mtu anae kujari lazima akuulize utataka kula nn siku hiyo ambacho kitakua tofauti na unachukula ukiwa kibaruani!
Weekend ni sawa atleast once a week😋
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Swali la kawaida sana hili kwa wapendanao, ila isiwe kila siku mara moja moja kuulizwa insaonyesha mke ni mtu wa busara na upendo, maana kuna siku mzee anaweza kujisikia kula kitu tofauti na akiwazach yeye..
 
Back
Top Bottom