Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

Mwanamke unatakiwa kuwa mbunifu, kuna wanawake wabunifu mpaka they trully amaze!
Leo atapikà wali nyama ya kusaga mara mixa culiflower vegetables. Kesho anapika style ingine ya chakula. Vitu ni vile vile ila kuna ubunifu.

Shida ya wanawake wa kibongo anajua mapishi matano tu.
Wali maharage +mchicha.
Wali + mchuzi wa nyama.
Wali + mchuzi wa samaki.
Ugali + nyama+maharage
Ugali + Samaki+ maharage

Yani utaona assortment ni nyama+samaki+mboga ya majani+ kuku.

Akiboresha ni pilau + ndizi+ nyama au kuku. Lazma ujionee tabu kupika. Kupika ni sanaa jamani. Na bado atataka akuulize maswali
Mmhh wanawake wa kibongo wengi siku hizi wanajua kupika vyakula vingi tu labda mseme hao wa kwenu mnawaokota wapi

Shida ni kwamba what if akapika hayo mavikolombwezo yote halafu wewe ukawa hujisikii kula wacheni maneno mengi
 
Hili ndio tatizo la kuoa wakati umri umeenda sana. Wenye ndoa za ujanani hilo swali wanaona halina shida.
 
Sasa wangu mi hapendi kabisaa ugali anapenda tuu ndizi za kwao Marangu. So mkipika ugali na ndizi zake ziwepo.Hakuna kitu kigumu kama kuwaza una pika nini aisee ni kazi ngumuu
Na hapo kwenye kuwaza cha kupika ndo msingi hasa wa hiyo kero,

Angalia.... msichana aliekulia mazoea ya kupika huwa anapika tu, hata kama ni ugenn utamwona anaenda jikoni kusaidia kuandaa chakula.

Wale wanaokaa sebuleni na kusubiri chakula mezani (mboga saba) ndo hao ambao wanapta shida sana kuamua cha kupika mpaka wanauliza.

Huwa najisikia raha sana nikute chakula nisichokitemea mezani, tena kiwe cha kikabila chao!

Wakati mwingine namtuma mahali makusudi ili nipate nafasi ya kupika mwenyewe ninachokipenda ambacho najua yeye hakiwezi.

Nikihitaji kitu ninachopenda nitamwambia kabla, nisipomwambia afanye anavojua.

Halaf.....
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi
Yes, kwenye ratiba naongana na wewe kabisa. Hizo zingine ni porojo zenu tuu wanawake[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Extrovert wewe ni mgumu sana kuelewa ujue! Hivi wenzetu hamnaga moods na vyakula?

Kila mtu kuna vyakula anavyovipenda lakini kuna siku unakuta kati ya hivyo vyakula unavyovipenda kuna kimojawapo ndiyo una hamu nacho sana kwa siku hiyo kuliko vingine! Halafu mke wako akapika cha tofauti ambacho sawa unakipenda lakini siku hiyo hauna hamu nacho utajisikiaje?
We muulize tu hata akienda mgahawani tu unakuta mtu anang,'ata meno mmmmm sijui nile nn, hadi anamuukiza rafiki yake ale nn, kama unachukia swali hilo we una roho ya kudharau upendo wa mkeo unless kama mnakamfarakano kidg.
USHAURI WANGU

Kuna watu wanapenda sana kudharau emotions za mke au mme wake, nakushauri hivyo unavyoona wewe leo ni upumbavu eti kwa sababu ya michoro ya uengeneer, au bank kwenye hala za watu, au kazi zako, ipo siku hayo mengine utaona ni zero ndipo utataman kuonja hata tu kuulizwa swali hilo la kipumbavu hutalipata, utatamani ufanyiwe utoto unaouona sasa ni utoto ila hutaupata.

Jaribu kuheshimu watu.
Katika kuushi kwako ongeza na wema.

Watu wengi hasa wadhaifu ni wanaume kuliko wake zao kwa nn? Nisikilize.
Mtu yoyote thabiti hujishusha hasa kwa watu walio wake. Mfano mtu anayepiga mkewe ni dhaifu kwasababu utakuta kosa hilohilo akifanya mwanamke mwingine hawezi kukasirika kama kwa mke wake, huo ni udhaifu. Kwasababu kwa mwanamke mwingine anaogopa wababe watampiga sawasawa ila kwa mke anakuwa yeye ndio final say, huo ni udhaifu kuliko mkeo. Jitathmini.
 
Yupo sahihi sana kuuliza shemeji yangu. Hata kama kusingekuwa na msosi
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi
Swali hilo kwangu ni zuri sana linanifanya nichague aina ya chakula ambacho ninahamu nacho siku hiyo.pia ni sehemu ya maongezi ya mke na mume wakiwa wametulia
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
nikajua mi ndio nakereka tu, Hadi nikawa najisshtukia. Ila kiukweli inakera hasa Kama mtu unapenda kuwa surprised na chakula, fikiria unaingia tu ndani unashtuliwa na harufu ya biriyani, ama chips ama ule ugali wa Dona ulioiva, Yani ukipata mtu anayekujulia ni kwamba unaingia tu harufu inaanza kutengeneza appetite huku unaelekea kuoga, unula unaanza Sasa na story za apa na pale, sio unafika umechoka, kupika hajapika, ndio akuulize unakula nini, unaishia tu kuoga na kutoka huku ukimwacha anapika, kurudi ushakula bia zako na nyama huko hata huna mda na chakula chake, kinaanza kisirani kumbe makosa kaanza kuyafanya yeye
Mi nishasemaga sitaki ayo maswali
 
Hio kila siku ndio limenifanya niweke bandiko. Hamna raha kama ukute mama kasharekebisha we ni kula tu. Ndio raha ya mke 😁
Teeh! teeh! Ule tuu!! ??? Mkuu baba na kale kalimbwata ka bagamoyo!! kakupunguza life span yako!! unachekelea tu!!! msosi mtamu kumbe unameza naniliu ile nzima nzima anakuhesabia tu matonge yanavozama! duuu!!

Hapo sasa watoto wakikua tu!! yaani yule wa mwisho akienda seco, unalo!! ujiangalie!! hata salamu tu!! akikupenda saana!! ataenda kuungana na wanawe anakuacha hapo!
 
Mi Hilo swali sijaulizwa bado, Haya pisi kali ya JF aliyetayari kuniuliza hilo swali hadi kifo kitutenganishe aje PM.
 
Napenda ugali tembele na aina zote za mboga mboga napenda sana siku nikioa nipate mwanamke anayependa pia
 
Mkuu binafs mm sion kama kuna ubaya,,kwa mfano sisi wa kutoka asbh kurud jion,unakuta mchana umekula ubwabwa na maharage au ugali samak kwa mama ntilie sasa mara nyingi tukirud nyumban tukakuta chakula aina ile ile huwa inabore sana,so kwa upande wangu napendekeza mwanamke anaemuuliza mumewe chakula cha kupika nafikiri apewe ulinzi wa kutosha.
 
Mkuu mke wako kukuuliza swali kama hilo sio dhambi ni vizur kushirikiana mawazo labda jana nmekula ugali pia waweza kutoa neno lolote labda leo mke wangu tunaweza kula ndizi nyama ndio mambo ya ndoa ayo braza kaka
 
Daah..!!! Yan huwa najua hili swali naulizwa mimi tuu kumbe tupo wengi..!! It is a question i hate in my life...
 
kweli aliyesema binadamu hatuna chema hakukosea kabisa. Sasa mkuu kuna ubaya gani kuulizwa hivyo aisee. Si unamjibu tu unachojisikia kula siku hiyo kaka. Tena kakuuliza kimahaba kabisa aisee.

Laiti ungejua kiasi cha raia kisichoulizwa hayo maswali na wanaombea kiasi gani waulizwe!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] you are right
 
Inaboa sana,Niko job nimechoka bado nianze kufkilia chakupika
 
Mke anapenda apike chakula ambacho ni chaguo lako, na wewe haupendi? Lol
Wanawake tunaweza kupika kila siku tunavyovipenda lakini je ndio wanavyopenda wapenzi wetu?

Ni swali zuri sana kwa watu wanaopendana na kujaliana. Hamna siku unaona kapika hiki lakini moyoni unatamani angepika hiki?
Leo pika pilau basi.niache sh.ngapi[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom