Hivi naweza kujenga nyumba kwa mshahara wa laki 5 kwa mwezi?

Optimists

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2021
Posts
379
Reaction score
1,082
Mbona naona kama nimekuja kuwasindikiza walimwengu? Age 30, kazi mshika chaki, familia na mke mtoto mmoja, elimu degree, uwezo wa kukopeshwa million 15, nina miaka 2 kazini.

Naweza kujenga nyumba? Au niachane na pressure za kujenga? Niende nikalime? Naona Kama nawasindikiza wanadamu hivi.

Sioni nikijenga kabisa.
 
Muulize mkeo kwanza hilo swali mkuu
 
labda nyumba ya buibui
 
Muulize mwalimu Mpwayungu Village yeye alitoboaje mkuu? Mshahara wa laki 5 unashindwaje kujenga wakati wenye mshahara wa laki 3 wanajenga fasta tu?
 
Mil15 ni kiwanja cha dogo langu kanunua pembeni ya jiji ila kwawengine ndo mkopo wa kujengea! Kweli maisha hayapo sawa, ila tukijitahidi kuwekeza tutapata ela nzuri kwa iyo ela utajenga ila utairudisha kwa mateso sana kheri kuwekeza kama unaujasiri kanunue ata shamba kubwa la miwa ni bora kuliko kujengea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…