LISU ajifunze na aone hali halisi ya mapokeo ya agenda zake ngumu kumeza kama hii ya No Reform No Election. Yaani huku mitaani SIO CDM wala CCM wote hayupo anayehangaika na agenda hii.
TL ajifunze kwa mtangulizi wake. Jamii ya watanzania haina huo utamaduni wa siasa za "kiuanaharakati".
Tukiongea na mapovu mdomoni huku shingo imekukakamaa tu, watanzania wanakudharau.
Watanzania wako tofauti kabisa na wakenya Mathalan ktk ishu ya Gen Z majuzi.
Kingine cha mwisho ni maendeleo na huduma za msingi zilivyosambazwa kote nchini
1. Maji
2. Umeme
3. Mabarabara
4. Shule na miundombinu yake
5. Fedha Iko mitaani
6. Private sector imepewa kipaumbele
7. Hela mitaani zipo
8. Ajira ndogo ndogo kibao, kuanzia bodaboda, viwandani, migodini n.k
UTULIVU huu wa nchi unawafanya hasa VIJANA wasite kutibua equilibrium kwa kuingia kwenye harakati za hovyo.
Akikubali kushauriwa basi aachane tu na na msimamo mkali wa no election.
Bora ashirikiane na WENZAKE kuhakikisha reform zinaendelea kutafutiwa platforms zingine ikibidi mashinikizo ya kimataifa zaidi. Ila kuzuia uchaguzi ni kujidhalilisha tu