Pre GE2025 Hivi ndio tuseme Wahariri wanaamini Tanzania hakuna ‘Electoral fraud’?

Pre GE2025 Hivi ndio tuseme Wahariri wanaamini Tanzania hakuna ‘Electoral fraud’?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimejikuta nimemuonea huruma Tundu Lissu.
Huruma ni sifa na silka ambazo binadamu hajifunzi.
Nilistudy body language ya Lissu kabla na baada ya kupata reaction asiyotarajia kutoka kwa Wahariri.
Wahariri wamemwangusha sana Lissu especially Deodatus Balile.
Wahariri wa Tanzania sijui mnahariri nini.

Pia nilipojaribu ku-study nyuso za hao wahariri kabla ya hata ya maswali yao nilidharau hapohapo.
Kwanza Inaonekana wamezolewa-zolewa tu.
Wapo wastaafu, Wengine watangazaji wa michezo..walikuwepo makada nk. Sikumuona Aloyce Nyanda pale wala Kikeke
Nilichoka.

Baada ya kusikiliza kwa utulivu ufafanuzi wa Lissu juu ya changamoto zinazozingira chaguzi za Tanzania, ni mwendawazimu tu ndiye ataamini kwamba Tanzania tuna chaguzi huru na za haki.

Ameleeza mambo mengi kwa kirefu, kiweledi, huku akitoa mifano kadhaa ya madhira aliyokutana nayo yeye binafsi na wenzake.

Ni dhahiri Tanzania tuna chaguzi zilizojaa election irregularities kila mahali....hili jambo hata watoto wetu wanajua.

Yaani ni afadhali hata Chadema wangefanya press na wadogo zetu wa Daruso...au Daruso za vyuo vingine.
Zamani ukijua unaenda kuhojiwa na Wahariri ulitakiwa uende umejipanga.
Kumbe siku hizi ndio zero kabisa. Nyakati kweli ni ukuta.

Hao tayari wako compromised. .... Toka wakati wa Bandari.... huyo Kikeke na Crown media yake ni mali ya MWENYE KIFUA KIPANA. So you should know who is behind it.
 
There is something in human, when they've an agenda of their own, it's been always manifested that no amount of truth will do.

Kabla ya kuwalaumu hao, zingatia kwamba hata ndani ya CDM yenyewe takriban nusu ya makada wakubwa haziivi na TAL.

Mfano mzuri ni kilichotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu chamani.

Pili, hao wahariri walitakiwa kufanya nini, kwa mfano? Kusimpathaiz na TAL?

I mean, what did you expect that did not happen?

Tambua kwamba politics ni a game of influence and winning all groups - media outlets included.

Kama TAL alishindwa kuwashawishi hao, hilo ni kosa lake. Kama wahariri hawakuwa tayari kushawishiwa vyovyote vile, basi hilo ni kosa lao na pigo kuu kwa taifa.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, hivi wahariri nao wana haki ya kuchagua upande wa kisiasa?

Kama ndivyo, hebu fikiria kwao wengi wao wako Sisiemu au chama kingine tofauti na CDM, unategemea nini?

Yote kwa yote, chama chochote cha upinzani kijifunze kwamba kutwaa madaraka, hususan kukiondoa chama tawala, siyo lelemama wala zoezi la usiku mmoja - it's a serious, constant business.

Until then, Sa100 mitano tena!
"Mfano mzuri ni kilichotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu chamani". Tueleze kasoro zilizotokea kwenye huo uchaguzi ili tuweze kufananisha.
 
"Tanzania ni Nchi Moja na ni Jamhuri ya Muungano "
Hivyo ndivyo Katiba yetu inavyoanza .
Wewe hilo la Tanzania ni Nchi mbili umelitoa wapi?
Unajuwa maana ya United republic of Tanzania au unajitoa ufahamu. Nakupa mifaano ya nchi zaidi ya moja kuungana. United Kingdom, United states of America, United arab emirates zingine endeleza wewe......
 
Lissu hoja yake ya uwakilishi bungeni dhaifu sana kumsikia akiletea mifano ya Zanzibar na Temeke, yeye hajui kuwa Tanzania ni nchi mbili? akili ya kawaida anataka Zanzibar wawakilishwe na mbunge mmoja tu kwa kuwa wachache. Kaja na mfano wa Dar na Mtwara kufananisha population na uwakilishi. Hajuia Mtwara ki size ni kubwa sana miundombinu sio rafiki kumfikia kila mtu wakati Dar hapo Temeke, Kigamboni, Ilala ni mdomo na pua pamoja na wingi wa watu lakini kufikia ni rahisi na mahitaji ya watu laki 4 temeke au hata wangekuwa laki 1 mahitaji na yaleyale. Mimi nadhani anataka kutuletea mfumo wa USA electoral vote kwenye nchi moja bila kulelewa USA zile ni nchi 50 zimeungana.
Dar miundombinu ni mizuri sana, je, mbunge wako amewahi kukufikia?
 
Unajuwa maana ya United republic of Tanzania au unajitoa ufahamu. Nakupa mifaano ya nchi zaidi ya moja kuungana. United Kingdom, United states of America, United arab emirates zingine endeleza wewe......
Tanzania tuna rais mmoja na bunge moja, achana na hilo la wawakilishi ambao hawatungi sheria za nchi.
 
Kuna baadhi yao hawaoni uzito wa yanayosemwa na akina Lissu juu ya demokrasia Tanzania kiasi kwamba mhariri mzima anauliza aliko Mbowe.
 
Yote kwa yote, chama chochote cha upinzani kijifunze kwamba kutwaa madaraka, hususan kukiondoa chama tawala, siyo lelemama wala zoezi la usiku mmoja - it's a serious, constant business.
Ni rahisi tu wakibeba mitutu au kutumia ugaidi wanakitoa asubuhi tu. Issue hapa ni namna ya kukitoa kidemokrasia, hao wakiruhusu katiba iheshimiwe mbona wanaondoka asubuhi tu. Si walisema kumuangusha Mbowe haiwezekani lakini uchaguzi ulipokua huru na haki aliondoka mapema kabisa.

Same to Samia, uchaguzi ukiwa huru na haki anaondoka wala haihitaji constant business sijui mapambano ni haki kuheshimiwa tu.
 
Kwani mmi nimemchulia,, na poa, Kwani Balele mimi nimesema Anakosa lolote mimi nimewaambia CDM wafanye kama wanavyo fanya wenzao wote wakiwaita waandishi wa habari wakitaka habari zao ziandikwe vizuri. Wawe na uhusiano mzuri na waandishi wa habari badala ya kuwafokea. Wawachukulie kuwa ni muhimili kamili wa nchi japokuwa hua wanaonekana kuwa watu wa kawaida. Ila wakiwachukulia poa watakuwa wanalalamika kila siku kuwa habari zao zinaandikwa zile mbaya tu nzuri haziandikwi. Ushawishi na mahusiano mazuri ndiyo yataweza kupata nafasi kwen,, nye vyombo vya habari vya nchi hii.

## "...nimewaambia CDM wafanye kama wanavyo fanya wenzao wote wakiwaita waandishi wa habari wakitaka habari zao ziandikwe vizuri. Wawe na uhusiano mzuri na waandishi wa habari badala ya kuwafokea..."

• Hiyo👆👆👆statement yako una maanisha nini bro?

• Kuwa na uhusiano mzuri na waandishi ni kwa kuwafanyeje?

• Na ile juzi pale wewe uliona atmosphere ya uhusiano mbaya kwani kati ya CHADEMA na waandishi wa habari?

• Unaweza ku - describe huo uhusiano mbaya ukoje au ulikuwa vipi?

• "Hao wengine" (japo hujawataja lakini tunajua una maanisha CCM/serikali) uhusiano wao mzuri na waandishi wa habari ukoje?

• Kila mkiitwa kwenye PC zao mnapewa bahasha za khaki zenye posho/hongo ndani yake ili mkaandike/mtangaze vizuri uongo na utumbo wao, au siyo.?

• Sasa aina hiyo ya journalism ya mpaka uhongwe hela Ili uandike/utangaze habari itakuwa journalism kwa ajili ya kuilisha jamii ukweli au mtakuwa wanahabari mawakala wa shetani mnaotumiwa na viongozi wabaya wa CCM kuiharibu jamii kwa kuilisha uchafu na uongo wao..?

• Dhana na mantiki ya pendekezo lako hapa ni kuitaka CHADEMA nao wawe wanagawa bahasha za khaki/hongo kwa waandishi wa habari zao, au siyo..?

• Hivi waandishi wa habari waliozoea kuhongwa Ili watangaze au waandike habari zile anazotaka aliowahonga ambazo mara zote ni uchafu na uongo kwa jamii, wanawezaje kuhongwa tena Ili waandike ukweli...?

## BY THE WAY: Ile juzi, Tundu Lissu na CHADEMA hawakuwa wanawafokea hao waandishi wa habari. Bali, Tundu Lissu specific alimkemea na kumuonya Deodatus Balile kuacha ujinga (nonsense thoughts and questions) badala yake ajikite kwenye uelewa na ufahamu juu ya katiba ya JMT ya 1977 pamoja na sheria mbalimbali zinazosimamia chaguzi za Tanzania. Alikuwa anasisitizwa kwa ukali aache upotoshaji. That's all...
 
Nimejikuta nimemuonea huruma Tundu Lissu.
Huruma ni sifa na silka ambazo binadamu hajifunzi.
Nilistudy body language ya Lissu kabla na baada ya kupata reaction asiyotarajia kutoka kwa Wahariri.
Wahariri wamemwangusha sana Lissu especially Deodatus Balile.
Wahariri wa Tanzania sijui mnahariri nini.

Pia nilipojaribu ku-study nyuso za hao wahariri kabla ya hata ya maswali yao nilidharau hapohapo.
Kwanza Inaonekana wamezolewa-zolewa tu.
Wapo wastaafu, Wengine watangazaji wa michezo..walikuwepo makada nk. Sikumuona Aloyce Nyanda pale wala Kikeke
Nilichoka.

Baada ya kusikiliza kwa utulivu ufafanuzi wa Lissu juu ya changamoto zinazozingira chaguzi za Tanzania, ni mwendawazimu tu ndiye ataamini kwamba Tanzania tuna chaguzi huru na za haki.

Ameleeza mambo mengi kwa kirefu, kiweledi, huku akitoa mifano kadhaa ya madhira aliyokutana nayo yeye binafsi na wenzake.

Ni dhahiri Tanzania tuna chaguzi zilizojaa election irregularities kila mahali....hili jambo hata watoto wetu wanajua.

Yaani ni afadhali hata Chadema wangefanya press na wadogo zetu wa Daruso...au Daruso za vyuo vingine.
Zamani ukijua unaenda kuhojiwa na Wahariri ulitakiwa uende umejipanga.
Kumbe siku hizi ndio zero kabisa. Nyakati kweli ni ukuta.
Wanajua sana kuwa ipo lakini teuzi zinawabana.
 
Hoja kuu ni bunge, wao kila jimbo (state) linatunga sheria zake ambazo haziingiliwi na jamuhuri.
Nenda kasome kidogo vizuri state wana vikao vyao vinaongozwa na Mayor huku kwetu kama madiwani na kuna congress hawa wantunga sheria za nchi kupitia Federal Goverment. Hapa Zanzibar wana baraza lao la wawakilishi pia wanasheria zao watunga za ndani ila kuna bunge la jamhuri wana deal na mambo ya Tanzania. Zanzibar wana mambo yao wanajiamulia hata kodi zao wanajipangia ndio maana bidhaa ya Zanzibar inapigwa tax tena huku na mambo mengine.
 
Tanzania hakuna wahariri kuna vibaraka wa chama tawala, na watawala ndio wana hariri kila kitu, wao wanaongozwa nini kiandikwe nini kitoke, lini na kwanini.
 
Wanapigania matumbo yao
Wakivizia teuzi

Ova
 
Back
Top Bottom