Unakubali kuwa kukiondoa chama tawala ni kazi ngumu kwani chama tawala kinatumia nguvu kubwa ya dola, lakini mwishoni unatumbukia kwenye ujinga wa kusema Samia 5 tena! Akili za watanzania ndivyo zilivyo mbovu ndio maana CCM inasitawi sana.
Kosa kubwa alilofanya Lisu ni kutohamasisha vijana kujiandikisha kwa nguvu kubwa sana.
Yaani alitakiwa aseme bila kuwaandikisha vijana wote hakuna uchaguzi.
Muda wa kuandikisha watu umekua mdogo na daftari limejaa marehemu na wazee wa miaka 80 wa vijijini wasiohitaji tena ajira wala elimu bora wala kupigania nchi yao inayoangmiwa kwa rushwa na kuuzwa kwa wageni.
Vijana wasio na ajira na wenye umri wa kupiga kura ni zaidi ya mil. 28 . Hawa wakipiga kura wote hata tume iwe ya Machawa wa CCM wanashindwa kwa kishindo kikubwa .
CCM inashinda uchaguzi kwa sababu ya kuvuruga daftari la mpiga kura ndio maana haijawahi kupata kura zaidi ya mili .12.
Kura za CCM zinaangaliwa wanachama wake kwanza . Ndio maana wananunuaga kadi ili kupunguza nguvu za upinzani kupiga kura.
Kwa hiyo Chadema wamekosea sana kushindwa kuhamasishwa vijana zaidi ya mil 28 kujiandikisha kwenye nchi yenye watu mil 65 ,CCM atachaguliwa na marehemu wengi pamoja na wanachama hai wa CCM wasiozidi mil 9.
Lakini pia Tamko la No reform no Election sio la Lisu .
Lilitolewa na Freeman Mbowe akiwa mwenyekiti.
Hakuna Tamko la Mbowe liliwahi kufanikiwa .Kuanzia UKUTA na matamko mengine kama ya Samia Must go .
Yote ni kwa sababu ni matamko ya kukurupuka na kuacha mambo ya msingi .
Kama kuwaandaa vijana kupiga kura kwa wingi sana . Ni wazi kwa sasa Lisu ni Mwanasiasa mwenye jina kubwa kwa uwezo aliopewa na Mungu. Samia ana jina kwa sababu ya pesa nyingi,madaraka makubwa, mamlaka ya kuteua .Vyombo vya dola,vyombo vya habari kuwekwa mfukoni n.k. Lakini Lisu ni Mtu from ziro tu Hero . Watu kama Lisu ni wachache sana na ndio hasa Chaguo la Mungu. Watu wakimbeza Lisu hasa watanganyika watakuja kumkumbuka watakapoona kuwa nchi na ardhi yote sio mali ya mtu mweusi tena na kila kitu kimeshachukuliwa na wageni kuanzia madini ,wanyama, bandari ,ardhi ,misitu na viwanda na biashara zote kubwa ni mali za wageni . Wenyeji watabaki wakipigwa na mapolisi mpaka siku atakapotokea Shujaa mmoja mwenye uzalendo na utu na kuwaonea huruma waafrika wenzake kama ilivyotokea Kagame,Traore ,Museven,Gadaffi ,Sadam Husein n.k na kurejesha Tanganyika kwa wananchi mili.65 kutoka kwenye mikono ya familia ya watu wasiozidi 20.