CAS ; CAF inasisitiza mchezo wa mpira uchezwe kwa gharama yoyote, Kwanini mmeahirisha mchezo halali wa Ligi? Kulikuwa na hali mbaya ya hewa?
TPLB; Hapana
CAS; Kifo labda cha mchezaji, kiongozi yeyote mkubwa?
TPLB; Hapana
CAS; Tishio la ugaidi, vita na uthibitisho kutoka mamlaka husika?
TPLB; Hapana
CAS; kwanini mmeahirisha mchezo halali wa ligi?
TPLB; Makomandoo wa Yanga wamezuia 5imba wasifanye mazoezi.
CAS; (wanacheka kwa nguvu, kisha wanakaa kimya)
CAS; Kwa mujibu wa kanuni zenu, kuna kipengele kinasema timu pinzani ikizuiwa kufanya mazoezi mchezo uahirishwe?
TPLB; Kulikuwa na tishio la usalama na dalili za rushwa
CAS; Tunaomba report kutoka mamlaka husika ikionyesha kulikuwa na mashabiki wenye mabomu, visu, mapanga au tishio la ugaidi kutoka idara za intelijensia au report kutoka TAKUKURU/ Police makao makuu/ JWTZ
TPLB; hatuna, ila mabaunsa jamani wametuponza! Tunaomba mtusamehe tuna familia zinatutegemea tukijiuzulu tutakula nini? Mguto atawaletea madafu ya Unguja, Mtusamehe
CAS; (wanacheka kidogo); Ok, Karia, Ukiwa kama rais wa TFF, Kwanini umeruhusu haya?
KARIA; sikutegemea tutafika huku jamani! Najuta kuwabeba wasiobebeka! Naomba mnisamehe nina familia inanitegemea!
CAS; Na nyie kwanini muandike barua ya kugomea mchezo halali wa Ligi na kuwalazimisha na kuwapangia bodi maamuzi?
5imba; Tulizuiwa kufanya mazoezi na makomandoo.Tulikuwa na mbuzi kwenye basi.
CAS; (wanaangua kicheko mara ya pili)
CAS; Kwahiyo mkizuiwa kufanya mazoezi, ndiyo muwapangie bodi maamuzi ya kuchukua na kususia mchezo halali wa Ligi na kugoma kuleta timu uwanjani?
5imba; (kimya, akiangalia chini) Lakini mkuu sisi hatuhusiki kwa sababu bodi ya Ligi ndiyo waliahirisha mchezo.
CAS; Kwa hiyo bodi ya ligi ndiyo waliandika barua ya kususia mchezo?
5imba; (Kimya akiangalia chini machozi yakimlenga)
ITAENDELEA...