Hivi ndivyo mahesabu CAF - 5 Year Ranking itakavyokuwa endapo Simba na Yanga zitaishia nafasi ya tatu makundi

MwananchiOG

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2023
Posts
1,970
Reaction score
4,037

Kwa mujibu wa Caf 5 year ranking system, kwa sasa Simba ikiwa nafasi ya 7 na Yanga nafasi ya 13 kutokanq na alama walizovuna miaka mitano iliyopita, hivi ndivyo hesabu ya jumla ya alama zitakavyokuwa kwa vilabu hivi viwili endapo zote zitaishia nafasi ya tatu makundi.

Coefficient ya mwaka husika huanzia 5, mwaka uliopita 4, mwaka juzi 3 n.k mpaka miaka mitano nyuma

Hii inamaanisha alama zilizovunwa mwaka husika zinazidishwa na coefficient ya mwaka husika na huo mwaka ukipita coefficient inakuwa 4,3,2 na 1.

Alama za Club bingwa ni tofauti na shirikisho kwa alama moja.

Hivyo Yanga akiishia nafasi ya tatu 2024/2025 anapata alama 2
Simba akiishia nafasi ya tatu 2024/2025 anapata alama 1

Haya tuje kwenye kuzidisha kwa coefficient ya miaka husika

SIMBA
2024/2025 - 1 × 5 = 5
2023/2024 - 3 × 4 = 12
2022/2023 - 3 × 3 = 9
2021/2022 - 2 × 2 = 4
2020/2021 - 3 × 1 = 3

Jumla = alama 33

YANGA
2024/2025 - 2 × 5 = 10
2023/2024 - 3 × 4 = 12
2022/2023 - 4 × 3 = 12
2021/2022 - 0 × 2 = 0
2020/2021 - 0 × 1 = 0

Jumla = alama 34

Hivyo Yanga atamzidi Simba katika CAF Ranking na huenda akaingia katika orodha ya vilabu 8 bora barani Afrika.

NB; huu sio utabiri, bali ni hesabu zitakavyokuwa endapo timu hizi zitaishia hatua ya makundi nafasi ya tatu. Huenda mambo yakawa tofauti, mwingine akasonga hatua ya mbele zaidi, au mwingine akaishia katika hatua za chini zaidi.Pia utagundua sifuri za Yanga zinazidi kupotea, Jambo ambalo ni faida kwake.
 
Kile kichaka chao walichobaki nacho Cha kusema ni wa 7 Afrika kinafyekwa msimu huu ndio mwisho wao, wajiandae kutafuta kichaka kingine na awatokipata itabaki historia, yanga ndio inaondoka ivyo waache wabaki na propaganda zao wanadhani mpira ni siasa!
 
🤣🤣🤣 leo w k 🤣🤣🤣 leo wk end umekula au unapakwenda
 
Pigia hesabu Simba anatolewa bila kuingia makundi, wale Waarabu wa Libya wana jambo lao msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…