Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Poleni sana ndugu wana jamii forum kwa msiba huo mzito uliowatokea.

Japo Ontario nilishawahi kubishana naye sana kupitia whatsapp na kundi lake lakini wafuasi wake wakanicheka na kunitusi mwishowe wakanitoa kwenye kundi lao la forex kupitia whatsapp, moyoni nilibaki kutabasamu nikafanya yanayonihusu unajua ni kwanini.... ?? Shetani wangu huwa haruhusu mimi kuamini na kukubali jambo lisemwalo na mtu moja kwa moja lazima niingie kusoma kwenye vitabu lakini nikaona siyo kweli hakuna pesa ya haraka haraka bila kuitolea jasho halali kuanzia kuanzia siku hiyo forex nikaachana nayo kuifatilia na sitaki kuijua, am hustle for my own..... Trust no bxtches. [emoji1] [emoji23] [emoji119] [emoji91]
Safiiii sanaaaa.... na me nilichogundua huwez tajirika na FOREX... forex is real sema huwez tajirika.... upo kama mimi...
 
Unapopewa wazo la kibiashara inabidi nawewe uliweke kwenye mizani, kwahio na mimi nilifanya hivyo hivyo nikagundua I'm not smart enough for that thing called Forex business.
Majibu mujarabu kabisa, umepevuka upstea mkuu,,bravo
 
Tamaa sio nzuri unajua training ilikuwa na session mbili ya watu nadhani 200 na ada ilikuwa 130,000/= kwa kichwa na kwa siku zinakuwa session 2 ya asubuhi na jioni.

Ukifanya mahesabu mshkaji alikuwa anatengeneza kiasi hiki 130,000×200= 26,000,000 in only five days. Na bado hakuridhika anataka kuchukua na za kwetu za madafu.

Life is always not fair.
 
Kuna watu kibao humu JF walituasa kwamba Forex ni utapeli hilo kwanza napingana nalo kwa nguvu zote sababu sio kweli kwamba forex ni utapeli kabla sijafunguka mengine niwathibitishie nimejiridhisha bila hata lepe la mashaka kwamba Forex is real and its my future lifestyle na binafsi sijioni nikikoma kufanya Forex licha ya haya magumu ninayopitia bali mawazo yao ninayachukuliaga kama catalyst ya kutaka kuzidi kuijua hii biashara kwa mapana zaidi kujua weakness na strength zake na kujua potential scammer, wezi na matapeli wakoje maana wametawala hii biashara kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na money liquidity kubwa kuliko soko lolote duniani..more than 6 trillion USD is traded daily on the Global financial market..hiki ni kiasi kikubwa sana hivyo matapeli huwa wanazengea zengea kwenye magap Kama haya yenye mkwanja mrefu..my economic cake pie is in Forex that's why I wont quit it easily.

But changamoto kubwa ya Forex ni hawa brokers na trainers..ninaposema trainers nazungumzia mtu kama Ontario hawa waliochungulia fursa mapema na kuintroduce kwa watu nchini kwa kigezo cha kuitoa elimu kwa bei sawa na bure tusijue wana agenda yao ya siri na Wasauzi ya kutaka kuwaliza watanzania wenzao.

Ontario ni mtunzi mzuri wa story na ana kipawa cha kusimulia na kushawishi kwa ufasha na ni mtu mwenye uelewa mpana wa mambo but anakosa kitu muhimu sana katika maisha uwezo wa kusocialize na watu in harmony..he is not a leader he is a boss na ukiangalia there is a thin line between a leader and a Boss..Ontario ana dharau, kiburi, na kejeli mbaya sana bila kujalisha umri wa anaeongea nae. Hana attentive listening ukiongea nae anakuangalia kama Choo na hajali lolote najua wengi waliokutana nae watakiri huu ukweli mchungu kwake ukiona mtu ana urafiki na Ontario ujue huyo mtu analazimika kujishusha sana kwa huyu dogo ili waende along. Huwa nashangaa ni rafiki sana na Bold. Pole sana Bold..I know what you going through.

Wahenga humu walituhasa kwamba ukiitwa kwenye fursa tafakari mara mbili yaweza kuwa wewe ndio fursa.anyways tulipoitwa kwenye fursa mwanzoni mambo yalienda vizuri na humu tulikuwa tunavurumusha screenshot za profit tu kwa maelekezo ya Ontario ili tuwakoge haters hadi haters wakafyata but kadri siku zilivyoenda mambo yakawa kimya ikawa ni loss daily tu watu wamechukua viinua mgongo vyote vikafyekwa sokoni. Hakyamungu!

Saga lilianza around mwezi wa kumi baada ya Ontario kula njama ya siri na broker awe anampa pips 2 kwa kila kichwa na zikiwa zinatoka calls kibao kombo kwa siku na zote zilikuwa sio accurate hivyo na watu kutengenezewa mazingira ya kutrade more often inamaanisha wakitrade watu 1000 wakafungua position 7 kila mmoja na idadi ya spreads pips anazopewa kutoka kwa broker kwa mtu mmoja ni 2..kimahesabu anapata 1000×7×2= 14,000 pips hizi ni dola kibao kwa siku ..wandugu wanojua mahesabu zaidi wanajua ni madola kiasi gani jamaa kavuta, hili suala alituficha but aliwahi kusema "Bob Marley you can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time"... Tukashtuka..tukamuuliza..akakubali ila akakiri alituficha na hayo mamilion yanayopatikana ni kwa ajili ya kuendeshea ofisi ya TMT co Ltd iliyoko pale Jangid plaza.. Watoto wa maskini tukakubali tu kwa shingo upande ila tukawa tumeghafilishwa na kusikitishwa sana na hizi njama zao..hili likapita na tukajilazimisha kukimeza maana ukipenda boga upende na ua lake.

Tamaa ni mbaya sana..licha ya kuchukua mamilion kutokana na hizo pips hawakuridhika..bado tena walikuwa wanachukua pesa kibao kwa siri kwa ajili ya IB link kwa affiliate program waliotuunga nayo siku tunamaliza mafunzo kutoka kwa broker kwa sisi tukipata loss sokoni wao wanapata chochote maana broker wao ni market marker. Hakyamungu! People are heartless.

Kama ilivyo asili ya watu wenye tamaa mbaya wakivurugana basi wao hukimbilia kutafuta sympathy ya Wateja..juzi wakavurugana broker na TMT kama ilivyo tabia ya wezi na matapeli kugeukana.. Majuzi wenyewe wanakuja na habari kwamba yule Broker ni market Maker na mwizi..kweli? Wakati wewe mentor umeishi South afrika na umekuwa Trader kwa miaka kibao bado hujui status ya broker unae trade nae? Na inakuwaje mrecomend broker mwenye walakini na competency na efficiency yake? Broker nae anajitetea kwa kutuma texts kwa Wateja privately akimtuhumu huyo mentor kuwa ni batili na mbabaishaji na kuwasihi watu wamuignore!? Blalifuli!

Tangu mwanzo mchakato uligubikwa na walakini mkubwa uliokuwa unaendelea..kwanza kumlazimisha mtu afungue real account baada ya siku tano tu za kumaliza mafunzo na aweke laki tano kuanza kutrade ilikuwa ni ishara ya wizi wa wazi sema tulikuwa na trust na maneno sukari ya Ontario, thus we were blind and fear of missing out easy Money.. Hatukujua!

Kutoa calls zaidi ya 7 kwa siku ni ishara mbaya ya kuwafanya clients waovetrade then wao wapige hela. Wizi huu.

Kuwaambia watu waongeze position ilhali wako in deep red ilikuwa ishara ya wizi, kuwataka watu waburn account zao wao wanufaike.

Kudiscourage matumizi ya stop loss ilhali ndio silaha ya kukinga mtaji wako kwenye Forex ilikuwa ishara ya wizi.

Watu wapoteze zaidi ili mpate zaidi maana kila ijumaa ilikuwa tunapunwa hela yote ya wiki nzima.

Mungu sio Sholo Mwamba, Yule broker market maker aliekuwa anatupiga sisi kwa tamaa kapitiliza kawafanyia mtimanyongo hadi kampuni ya TMT kaipuna zaidi ya nusu billion mapema mwezi wa kwanza. Imagine kampuni hii Changa ya huyu dogo imewazaje kupata nusu billion kwa muda mfupi hivi? Ni mikwanja aliyotuibia sisi misukule wake. But in life! "easy come..easy go"..ukikipata kiwepesi..kitaondoka kiwepesi pia. Nusu billion gone in a single month. Kweli JP Market broker ni hayawani!

Nitoe Rai kwa Ontario...sio kwamba namchukia hapana Bali naamini biashara inayohusisha watu moja kwa moja haiwezi kutokana na tabia yake mbaya ya asili..biashara na dharau, kebehi, utapeli na matusi havichangamani milele. Ni vyema akaendela na kilimo apate mil 19 zake kwa siku. Ameharibu kitu muhimu sana katika maisha yake ya biashara "Brand" and trust ya watu wengi aliowavuta kwa maandishi matamu humu JF..Trust ya watu pekee ni mtaji mkubwa kuliko hata mtaji wa fedha.

Namshukuru kwa kutuletea fursa hii adhimu lakini isiwe sababu ya kutuibia, kututapeli na kutunyanyasa economically and emotionally.

Rai kwa traders waliopigwa za uso na ndugu yao.."if you want to be strong learn how to fight alone" kwa kuwekeza Kwenye skills and self learning tunaweza kuwa self consistency profitable traders..let's ignore TMT they are scammer and predators and I don't recommend anyone to trust them.

Oooooopsiiii! Finally misukule wa Ontario tuko huru but tuko nyang'anyang'a kiuchumi. But it feels good kuwa huru.

Forex sio utapeli, matapeli ni mawakala wake.

Ni bora walimkavu...kuliko walimwengu!

Freedom!.


U were trading against TMT na JP ..

only a lunatic will think TMT and JP were on your side!

Please leave this shitty business!

Kusema Forex ni biashara ya kweli ni sawa,ila inahusisha utapeli!

Ni kama gold ni ya kweli,ni real,ila akina Papa Msofe wanaifanyia utapeli hiyo hiyo!
 
iLA HUYU DOGO atakua alikua anajua nini anachofanya,,Theme yake ilikua sio kusaidia eti vijana nooo.ni kutengeneza hela na amefanikiwa.Huezi kuwaambia watu waanze na real account wakat forex course ya siku tano tu,,Uliwaaminisha watu pumba.ukichanga na huyo mentor=mashudu na pumba
 
Na wewe hukua mmoja wao...? Kama nakukumbuka hiv....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] catching the early bird mara nyingi watu wanapigwa, kwa aababu bado wanakua na moto!
 
mkuu, mimi nafanya folex, na sijawahi kuwa na mentor na profit na make, na sijawahi pigwa lost. by now nipo na ma broker wa 3, forex.com, etoro.com na hawa templerfx.com... naishi mwanana tu, sijawahi hata ku attend training zaidi ya kujisomea mwenyewe
TemplerFx waliniambia Training ya wiki mbili na mentorship ya mwezi ni sh 500,000/ nikasepa!
 
Mmmh..me nimestop kidogo dear
Nikipata time ntaanzisha uzi...... huyu Dogo Ontario arudishe PESA za watu..... FOREX is real sema ni kama sports betting tu... utofauti wake FOREX n kusoma soma ma vitabu.... but n same na betting.. huwez tajirika through FOREX....

Ukiachana na utapel watu kama akina Ontario.. behind FOREX kuna kitu kikubwa sana ambacho watu hawakijui thus why wanapoteza.... FOREX ingekuwa kama Ontario na watu wengine wanavyoaminisha hakuna mtu angekuwa masikini.. watu wote tungekuwa matajiri.....

Kuliko mtu afanye FOREX bora afanye sports betting TU....
 
Ila kiualisia huyo Dogo Ontorio yuko smart na ana akili sana.
Dirty or clean.. Pesa inatafutwa kwa njia yeyote ile..

Kudos to him.. Ameweza kuwakamata wanaopenda mtelezo..

Ila hili sakata la Ontario limenionyesha ni kwa jinsi gani watanzania ni mbumbumbu. Yaani hata akili ya kawaida kung'amua kwamba tunaenda kuibiwa walishindwa. Ile lugha aliyokuwa anatumia ilikuwa inaonekana kabisa ni ya ujanja ujanja, wengine tulitoka mbele kuwafungua macho ila tuliambulia matusi tu na kuitwa tunawivu.

Binafsi nampongeza sana Ontario, ni wachache sana wenye roho kama yake.. Amepata, anebadilisha maisha ya watu kadhaa wanaomzunguka lakini daima alichokifanya kitamuwinda.

Watoto wa mjini, wajanja wajanja wanaojipatia pesa kwa njia danganyifu daima wanakuwaga na mwisho mbaya..
 
Tatizo la forex trading, watu tunataka kuivamia kama biko, yaani kucheza kwa kubahatisha. Forex trading ni topic ya kuishikia kalamu na karatasi, ikichangiwa na analysis lukuki. Na kabla washiriki hawajaielewa vizuri, waeleweshaji wakakaa mkao wa kujinufaisha kwanza….na faida nahisi inakuwa kubwa kama watu bado somo halijakolea….

Nina imani kwa sasa mtoa mada utakuwa umeielewa the hard way hasa kwenye eneo la participants wa market.
Forex haina ujanja, acheni kudanganya watu..

Forex is gambling, na duniani hakuna Insurance kwenye gambling business..

If you want to be rich, u need to sell goods or services, full stop.

Matajiri wote duniani na wote wenye maisha mazuri wana bidhaa au huduma wanaipeleka sokoni.

Forex haina tofauti yeyote na betting.
 
Back
Top Bottom