Mkuu
Humble African kwanza asante kwa uzi huu maana utazidi kufungua watu akili kujua kuwa ni FOREX SIO UTAPELI, nami nasema FOREX SIO UTAPELI.
Labda nikusahihishe jambo moja au mawili ili kuondoa utata.
MOJA ni kuhusu IB(Introducing Broker), Brokers kama wafanyabiashara wengine wanahitaji watu watakaofanya nao biashara kwahiyo walitengeneza affiliate program ambayo itamuwezesha mtu kuweza kupata faida iwapo atamuongoza mtu afikie maamuzi ya kufanya trading na Broker huyo, yaani kumtambulisha Broker!!Sasa kuna sehemu umesema kuwa IB inampa faida mtu iwapo huyo trader atapoteza pesa tu. Hii sio kweli kabisa. Mtu mwenye link ya IB anapata faida kutoka kwa broker kwa zile SPREADS wanazokatwa traders wanapofanya trading(Hapa traders watanielewa). Broker anakugawia sehemu ya ile faida ya spread pekee na sio kwamba hadi mtu apate loss. Mfano mtu akifungua trading account kwa kutumia link hii:
Templer FX Trader basi atamuwezesha mtu mwenye link kupata faida kutoa kwa broker, inamaana faida ya broker itapungua kwa sababu atamgawia na mwenye IB link au ukiamua kujiunga moja kwa moja basi broker atakuwa anachukua faida yote ya SPREADS. Sasa kwa trainers wanakuwa na wanafunzi wengi na akiishawafundisha waende wapi sasa, inabidi uwatafutie broker. Sasa hapo ndipo broker wanakupa link ya faida yaani IB.
PILI, Kuna aina kadhaa za brokers, Moja ni A Broker ambaye yeye anakuwa kama middle man tu anakuunganisha trades zako na liquidators na yeye anafaida na SPREADS tu mfano ni TemplerFX: Unaweza kuwaangalia hapa
Templer FX Trader, au wanaweza kutoza Commission mfano ni Tickmill: Unaweza kuwaangalia hapa
Tickmill: Trade Forex & CFDs with an FCA UK regulated Forex Broker.
Sasa kuna broker wanaitwa B Broker, hawa ni wabaya kwa sababu wanafanya trade against you, 'They Book traders' Yaani wewe ukifanya SELL wao wanafanya BUY kwa pair hiyohiyo kwahiyo kupoteza wewe yeye anapata na hao wanaweza kuwatumia mentors kuwahadaa traders ili wapoteze ili broker apate na hao wanafanya kwa makubaliano ya malipo haramu ambayo haya malipo sio ya IB bali uhuni, wizi, na utapeli.
Kwahiyo ni vyema kwa traders kuwa makini na kuchagua brokers wanaoaminika na ambao wana sifa nzuri kwa traders wengine na sio kuletewa tu.
Pili kampuni(Trainers) sasa zimeongezeka nashauri watu wawe makini sasa kujua wapi wanajifunzia mfano kwa sasa najua kampuni kadhaa ambazo wote wako vzr na wana broker ambao wana sifa nzuri za utendaji. Kampuni hizo ni kama DAR FOREX ACADEMY chini ya Carl, +255MillionairesFX(Sijui Mhusika), na Tanzania Forex Institute(TFI) chini ya bwana mmoja nadhani ni David (Naomba kurekebishwa kama nimekosea).
TAHADHARI
Kwa wale ambao wanadhani forex ni nafuu ndio hao wanaenda kuibiwa!!!!!Unafundishwa Forex kwa 100,000 kwa siku 5 halafu unaanza kufanya trading siku hiyohiyo ni wizi.
Forex ni gharama, kubalini kugharamika, wekezeni kwenye kupata elimu bora ili kujilinda na kupotea kwa fedha zako. Wengi wanapoteza hela kwa sababu wanaamini forex haizidi 100,000 na huko ndipo hao trainers wanaingia makubaliano na brokers wa kuwaibia!!!!!
Poleni sana mliokumbana na kadhia hii lakini FOREX IS REAL. Pata elimu sahihi tu na muongozo sahihi.