Kwanza nitoe shukrani za dhati kwa Ndugu Humble African kwa hiki ulichokiwakilisha hapa Jukwaani.
Hongera hizi nakupatia ndugu yangu, kwanza kwa kuwa Mkweli wa kueleza kilichotokea bila kuficha kwa uwazi kabisa, nikushukuru sana kwa hili jambo.
Sasa nije kwenye suala lenyewe na niwe Mkweli kama alivyo Ndugu Humble African, mimi nimepita TMT na nimelipa ada ya 130K na kupata Training ya Siku 5 iliyokuwa inafundishwa na Mr Rea.
Kwa kweli tulipoanza na hawa TMT hali ilikuwa shwari sana lakini baada ya muda kidogo malalamiko yakaanza kutokea na mara hii watu wakilalamikia Spreads kuwa ni kubwa sana ukifananisha na Brokers wengine. Mr Cre alilalama sana kuwa yeye anatoa Calls lakini watu wanatrade na Brokers ambao si JP Markets, bahati nzuri hili lilipita na mambo yakaendelea. Nimekuja kushangazwa na hili lililotokea kama siku 4 zilizopita limenivunja moyo sana tena sana.
Nikiwa ni mmoja wa members wa Group za Whatsapp Mentorship zinazoongozwa na Mr Cre nimeikuta sms tena iliyoandikwa na mwenyewe Cre kuwa kuna tatizo kwa broker wetu JP Markets kuwa anachotufanyia sisi Clients wake ni B Bookings, kwa tafsiri rahisi ni kuwa tunapofanya trades na yeye anapokea order zetu badala ya kuzipeleka moja kwa moja kwa Liquidity provider yeye kama yeye anabaki nazo na anafungua order against sisi ili ukipata hasara yeye anapata faida na ukipata faida yeye anapata hasara. Huu ndiyo mchezo uliokuwa unafanyika na kututia hasara mara kwa mara na kuwafanya watu kufund akaunti zao kila wakati.
Mpaka sasa hatujui kipi kinachoendelea zaidi ya Mr Cre kupost kitabu kinachoeleza A Book Brokers na B Book Brokers na tofauti zao basi.
Kutokana na haya yaliyotokea tunajifunza nini?
1.Uaminifu tuliokuwa nao kwa TMT nikimaanisha kwa Ontario, Mr Cre na Mr Rea wote umeshu ka toka 100% hadi 15%.
2.Tuwe tunahitajika kupewa mae lezo yote muhimu yanayohusu Broker ambae tunatrade nae. Nafikiri wengi tumesahau ku wa moja ya sharti lao TMT ni kutrade na Broker wao walio mchagua.
Tukiacha sharti hilo ni kuwa bado tunaweza kuendelea kutrade nao kwa Broker watakae mchagua. Sasa tunataka kupata hakikisho kuwa ni kwa namna gani tunaweza kuepukana na suala kama hili lililotokea?