Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Safiiii sanaaaa.... na me nilichogundua huwez tajirika na FOREX... forex is real sema huwez tajirika.... upo kama mimi...
 
Unapopewa wazo la kibiashara inabidi nawewe uliweke kwenye mizani, kwahio na mimi nilifanya hivyo hivyo nikagundua I'm not smart enough for that thing called Forex business.
Majibu mujarabu kabisa, umepevuka upstea mkuu,,bravo
 
Tamaa sio nzuri unajua training ilikuwa na session mbili ya watu nadhani 200 na ada ilikuwa 130,000/= kwa kichwa na kwa siku zinakuwa session 2 ya asubuhi na jioni.

Ukifanya mahesabu mshkaji alikuwa anatengeneza kiasi hiki 130,000×200= 26,000,000 in only five days. Na bado hakuridhika anataka kuchukua na za kwetu za madafu.

Life is always not fair.
 


U were trading against TMT na JP ..

only a lunatic will think TMT and JP were on your side!

Please leave this shitty business!

Kusema Forex ni biashara ya kweli ni sawa,ila inahusisha utapeli!

Ni kama gold ni ya kweli,ni real,ila akina Papa Msofe wanaifanyia utapeli hiyo hiyo!
 
iLA HUYU DOGO atakua alikua anajua nini anachofanya,,Theme yake ilikua sio kusaidia eti vijana nooo.ni kutengeneza hela na amefanikiwa.Huezi kuwaambia watu waanze na real account wakat forex course ya siku tano tu,,Uliwaaminisha watu pumba.ukichanga na huyo mentor=mashudu na pumba
 
Na wewe hukua mmoja wao...? Kama nakukumbuka hiv....
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] catching the early bird mara nyingi watu wanapigwa, kwa aababu bado wanakua na moto!
 
TemplerFx waliniambia Training ya wiki mbili na mentorship ya mwezi ni sh 500,000/ nikasepa!
 
Mmmh..me nimestop kidogo dear
Nikipata time ntaanzisha uzi...... huyu Dogo Ontario arudishe PESA za watu..... FOREX is real sema ni kama sports betting tu... utofauti wake FOREX n kusoma soma ma vitabu.... but n same na betting.. huwez tajirika through FOREX....

Ukiachana na utapel watu kama akina Ontario.. behind FOREX kuna kitu kikubwa sana ambacho watu hawakijui thus why wanapoteza.... FOREX ingekuwa kama Ontario na watu wengine wanavyoaminisha hakuna mtu angekuwa masikini.. watu wote tungekuwa matajiri.....

Kuliko mtu afanye FOREX bora afanye sports betting TU....
 
Ila kiualisia huyo Dogo Ontorio yuko smart na ana akili sana.
Dirty or clean.. Pesa inatafutwa kwa njia yeyote ile..

Kudos to him.. Ameweza kuwakamata wanaopenda mtelezo..

Ila hili sakata la Ontario limenionyesha ni kwa jinsi gani watanzania ni mbumbumbu. Yaani hata akili ya kawaida kung'amua kwamba tunaenda kuibiwa walishindwa. Ile lugha aliyokuwa anatumia ilikuwa inaonekana kabisa ni ya ujanja ujanja, wengine tulitoka mbele kuwafungua macho ila tuliambulia matusi tu na kuitwa tunawivu.

Binafsi nampongeza sana Ontario, ni wachache sana wenye roho kama yake.. Amepata, anebadilisha maisha ya watu kadhaa wanaomzunguka lakini daima alichokifanya kitamuwinda.

Watoto wa mjini, wajanja wajanja wanaojipatia pesa kwa njia danganyifu daima wanakuwaga na mwisho mbaya..
 
Forex haina ujanja, acheni kudanganya watu..

Forex is gambling, na duniani hakuna Insurance kwenye gambling business..

If you want to be rich, u need to sell goods or services, full stop.

Matajiri wote duniani na wote wenye maisha mazuri wana bidhaa au huduma wanaipeleka sokoni.

Forex haina tofauti yeyote na betting.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…