Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Dah. **** mpaka bei uchi za sasa! Haya mambo sio madogo kwakweli
 
Pole sana.

Jipongeze pamoja na mtaji uliouanzia umetengeneza pesa na nyingine umeshazitumia.

Ukifungua ule uzi ukisoma mwanzo mpaka mwisho watu wengi walipewa warnings za mwanzoni kabisa tena na huyohuyo Ontario.

Ule uzi ulieleza mengi sana ikiwa na experiences za mtu mmojammoja.

Ila cha ajabu kwenye ule uzi, mtu hajamaliza hata pages 20 za kitabu chochote, anafungua demo account anaanza kutrade. Hapo unategemea nini?

Shida yetu watanzania wengi ni kutotumia 'reasoning' ya vitu vya kawaida kabisa. Tunapenda hela za harakaharaka ila kuziteseka hatutaki. Mfano unasikia mambo ya kitapeli yanaletwa kila siku watu wanapigwa na hawakomi. Anzia kwenye Desi, Sungura nk.

Sipendi mtu anayefanya makosa halafu anahamishia lawama kwa mwingine kana kwamba dhamana ya kufikiri na kuhoji sio yake ila huyo mwingine. Sijui anapata mamlaka yapi ya kusema nlitakiwa niwaonye wakati kwenye ule uzi kila mtu alionywa toka mwanzo mwisho.

Unaambiwa usitumie stop loss na hutumii, unaambiwa lazima utumie broker huyu unafuata, unapewa training hapohapo unategemea kuishi kwa signals. Kwa mtu mwenye akili ya kudadisi lazima ahisi kitu aanze kujitegemea mwenyewe.

Ndio maana nikasema, forex is not for everyone. Inahitaji practice, readings kwa muda mrefu hadi uwe intependent.
 

Call it betting or whatever…lakini hata vyuoni kwa waliosoma masomo fulani watakumbuka kuwa hii ni topic nzima inayojitegemea.
 


Umemaliza Mkuu wangu....mm mwenyewe nilishaamua kuwa sitaki tena mentor wala baba yake na mentor maana sijaona umuhimu wake kwa kweli.. Kwa Sasa naendelea kupiga tu books hapa na demo ili niwe nondo zaidi.
 
Mi hata sijui mentor anafananaje kwakwelii ila market naifundisha nayo inanifunza adabu mentor anaekulazimisha umtumie broker flan ni mwizi mkubwa poleni sasa nimejua ya ontario kwa urefuu sasa sijui atarudishaje uaminifu
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hizo comment za wadau hatari aisee
 
Ha haha we baki na tunguri zako bana
 
Hebu unifundishe namie mdogo mdogo mwaya
 
Unapopewa wazo la kibiashara inabidi nawewe uliweke kwenye mizani, kwahio na mimi nilifanya hivyo hivyo nikagundua I'm not smart enough for that thing called Forex business.

Ningeshangaa sana kama na wewe ungeingia kichwa kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…