Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Eeh mkuu una experience hivyo!!
Uwezo wa kumuoa kipindi hicho nilikuwa nao maana nilikuwa wakala wa crdb,nmb,Nbc pia agent wa vochana sigara karibia zote hama pia nilikuwa wakala super agent wa mpesa(kuweka float) na nilikuwa na laini ya lipa kwa mpesa kipindi hicho ilikuwa hakatwi mtu yaani kama unabuka hawakati kitu. hivyo nilikuwa naondoka hadi 300k ambazo boss hawezi jua kitu.

kwenye vocha kadharika maana hatukuwa na bei maalum box la vocha za m80 kutoka dar nikifika ndani ya siku2 zimeisha! hapo bei tuliyokuwa tunauzia tofauti kulingana na mteja anataka mzigo kiasi gani wapo tulikuwa tunauza 470/475/480. hivyo hesabu unakuja kufunga na bei na bei ya 470 kwa mzigo wote fadia nyingine juu yangu.

kumbuka mshahara nalipwa 70k kwa mwezi pamoja nakushika manot yote yale...nilikuwa na jamaa zangu kila weekend nilikuwa nawatoa 30k ama 50
 
Haka kauzi heading yake nilikuwa sielew,nikawa nakapitiliza tu,kumbe kana hadithi tamu sana hv

Ila huku mwisho umekuwa mjinga sana,kuforce kwenda kwa jamaa wakat unajua jamaa yupo nchini hz ni nyege gani

Niliwah kuwa na mke wa mtu kama huyo,yeye ndo alikuwa ananitafuta wakat jamaa yake yupo,mim sikuwa na muda nae kabisa,hata siku jamaa anaondoka yeye ndo alinitafuta kwa bashasha na nilitaka hata tumalize wiki mbili bila kukulana lakin alishindwa,alitaka tuendeleze chapu
 
Kuna uzi humu niliwahi eleza kisa chote nimesahau heading ilikuwa inasomekaje.

Yule demu alikuwa muuza maziwa pia alikuwa msabato. Hapo kitaa wahuni walikuwa wamejaribu kila njia lkn akawachomolea iwe hela bado kwao ilikuwa ngumu sana.

Baada ya muda nikaweka uteja kupitia mama yake na wamama wengine wauza maziwa sikuwa na mazoea na binti yyte pale.

lengo lilikuwa kumnasa yule binti.kwanza alikuwa mzuri sana na amepanda juu yaani tunalingana urefu futi5 cm kadhaa....

Nikabahatika kumteka mama yake kiheshima huku yeye ni salam tu na alikuwa na nidhamu kubwa sana.
Mama yake alipojaa kwenye mfumo basi siku mama asipokuwepo nitajifanya kusitikika kabisa.

kufupisha.....baada ya siku kadhaa nikaanza kumwingia kuwa anipelekee maziwa geto yaani awe ananiletea hata kama sipo anaweka tu getoikawa hivyo yeye hata mama yake .


Nilikuwa wakala kipindi hicho wa bank kadhaa hivyo nilikuwa na kawaida ya kuomba note za buku kiasi hata cha laki2 mpya. nikamuonyesha kuwa hela yako uwe unachukua hpa hapaswi kupajua mtu mwingine tofauti nawewe akakubali.

pia nikamwambia issue yoyote ya hela inayomuhusu awe anachukua hata bila kuomba ukumbuke hakuwa na simu. Mara kladhaa alikuwa anatumia ya mama yake.


Siku zikaenda mazoea yalishakorea sasa na nilikuwa hadi namsindikiza kwenda kwao hata mama pia.
kuna siku mama yake alileta maziwa geto siku hiyo alipofika mvua kubwa ikaanza nyesha mle geto hapakuwa hata na kiti nikamuomba ake kwa godoro akagoma badae akakubali mimi nkakalia ndoo. badae maza ake alienda mida kama ya saa2 hivi usiku biashara ishadoda.

Siku moja demu huyu alikuja nikamshawishi anipikie ukumbuke kule maziwa kaachia watu tu kumshikia wanauza ya kwao tu hadi saa2 mzigo uko vilevile . tukapita hoteli moja nilikuwa napenda kula pale hata mama nilikuwa nampeleka kula hapo nikawaambia leo biashara imegoma naomba nikuuzie haya maziwa kwa sababu wewe una firiji nakuuzia kwa bei ya ofaa akakubali tukauuza halafu helailiyopelea nikafidia.


hapo sijawahi mwambia nampenda wala nini hata hela aliwahi chukukua3000 tu.Mama yake alinikubali hadi akawa ananiletea nyama ama kuku wa kuchinja muda mwingine mahindi mabichi nachemsha kuchoma.

Baada ya kumuweka kiganjani mama yake hofu kubwa ikaja iwapo mama atajua hii ya mwanae ataniona wa ovyo sana.Siku moja nilijifanya naumwa ili aje tu kweli akaja ilikuwa siku ya sabato akaaga anenda kusali kanisa jirani walikuwa sijui na kusanyiko sijui wanafunga makambi whatever. siku hiyo ndo nikashinda nae alivaa nguo zangu kwa kuniomba nimpishe abadiri nikakataa sana badae nikakubali akavaa alifua hadi boxer mashuka nakupika nk.

Siku hiyo ndo nilimwambia kuwa namuhitaji akaniambia niende kwao hapohapo akasema ameshachumbiwa na wazazi hawatakubali niolewe mara2 iliniuma sana nikakumbuka hela zangu muda wa kumpeleka kwao kumbe ananichora tu.

Aisee japo yeye hakuona reaction yangu nikamwambia nami najua mzuri kama wewe huwezi baki bila kuwa na mme ama mahusiano. Basi katika story akaniambia hajawahi kusex kabisa....siku hiyo alienda .....

Dada yake aliuguliwa katoto akalazwa na akaombwa aende kwa dadake.Hivyo mama yake ndo alikuwa anakuja kuuza maziwa sisi tunapeleka chakula jioni hospital baada ya mimi kutoka job. hakuna aliyejua na dada yake alijua mi ni Dr Tu maana nilikuwa na koti lasuti jeupe na miwani ya kuzugia nilikuwa nikiingi wodini. nasalimia karibia kila mgonjwa (mtoto).

Hivyo dadake hakuhisi kitu chochote hata kujua tu tunafahamiana na mdogo wake.
Mama yake kuna siku alinambia nimtafutie sehemu ya kushona cherehani hii ilikuwa oda kutoka kwa jamaa na mama alinambia ndo nikajua kweli kaolewa kumbe......

Uzuri jirani ya ofisi yangu ya uwakala alikuwepo dada mmoja alikuwa anashona na anavitambaa nilimwambia akakubali mama nikamwambia aje kwanza apaone na amjue yule dada kabla ya kuja kuanza kazi ikawa hivyo...

Jamaa alimuuliza demu anapenda nn ili akija home amfungulie demu akasema kushona ndo akatoa go ahead hii..
Nilibahtika kumla huyu demu na kweli alikuwa silidi. Penzi likakolea sasa kuna siku sasa akaja akalala kabisa maana nilimuhakikisha nitamuoa yeye aangalie uwezekano wa kumuacha jamaa tu.

Sasa nahisi hata mama alihisi kitu lakini kwa nidhamu yangu hakuhofu. ilifikia hatua nikampa ufuguo wa geto maana kushona akawa hataki tena hivyo akifika ananiaga tu kuwa akija dada(mama ) fundi cherehani nimwambie anaumwa amerudi nyumbani. ukumbuke simu ya mama yake anayo kwahiyo akifika geto anapika anadeki na nilikuwa xmart tecno nikampa hivyo kazi yangu nikumuunga bando na kumwambia ingia youtube search vichekesho nk basi kazi nilimaliza kabisa.


Siku moja wazee wake wakaenda msibani lengo ilikuwa wakalale huko msibani ....yeye akaenda kwa dadake by saa11 akaja geto nikawa naye by saa3 mzee akapiga nikaiwahi maana ilikuwa vibration nayeye yuko busy na vichekesho. nikaacha hadi ikakata then nika weka kidenge yeye hakujua kitu akasema baba huwa anapiga kila usiku kuuliza kama tumelala vipi hajapiga tu nikamwambuia hajapiga.


Kumbe walirud bana na baada ya kumkuta hayupo wakapiga simu japo wenzake walisema alienda kwa dada na wakaamini.kesho yake tukaamka saa1 kumaliza kujiandaa saa2 hii hapa.Akaniambi my mi naenda home chap nikacheki halafu narudi kulala umenichosha sana. Huo ndo ulikuwa mwisho wa kumuona asee.....


Baada ya kufika kwao si akamkuta mzee wake na mama yake wakauliza mbona umetoka kwa dadako mapema hivi hata vyombo hujaosha wewe.Mzee wake akapiga simu kwa dada yake bahati nzuri haikupolewa na muda tu mzee akatoka akaenda kutembea hukohuko dada akamurudia mzee wake baada ya kuona alitafutwa mzee aliuliza rachel alilala huko? dada yake hapana alirudi mbona.

Mzee akamrudia mama yake muda huo anajiandaa aje kushona mzee akatoa amri rachel asitoke getini maana hajalala hata kwa dadake....hapohapo jamaa aliyechumbia akapigiwa simu aje achukue mke wake. huku akipewa maneno makali sana na mzee huyu rachel hasa laana iwapo hata sikia maneno yake.

kwa kifupi mkuu hii ni shot story tu na nimeruka vipengele na kuchnganya story utafute ule uzi ukiupata ndo utaelewa zaidi. Ukweli niliumia mno asee lakini nilijipa moyo konde. demu baada ya kwenda kwa jamaa kesho yake tu akanipigia simu ndo akanipa full strory kuhusu kwao tena ananiraumu kwanini sikwenda na ananimbia atoroke nikamfiche kijijni kwetu hata miezi3

Muda ananiambia hela anayo ya nauli kama mimi sina nafasi niwaambie tu nyumbani kuwa kuna mgeni anakuja wampokee atokomee na anasisitiza kuwa ukikubali tu mi naanza kwenda sasahivi.

lakini nilipiga chini kwa maumivu makali mno nikakataa.nilimblok kama mara3 nikachoka sasa maana alikuwa anabdiri no mara achukue kwa majirani zake tu badae akanipa masufuria ya kuanzia maisha ninayo hadi leo
Ni uzi wako afu umeusahau jina
 
Uwezo wa kumuoa kipindi hicho nilikuwa nao maana nilikuwa wakala wa crdb,nmb,Nbc pia agent wa vochana sigara karibia zote hama pia nilikuwa wakala super agent wa mpesa(kuweka float) na nilikuwa na laini ya lipa kwa mpesa kipindi hicho ilikuwa hakatwi mtu yaani kama unabuka hawakati kitu. hivyo nilikuwa naondoka hadi 300k ambazo boss hawezi jua kitu.

kwenye vocha kadharika maana hatukuwa na bei maalum box la vocha za m80 kutoka dar nikifika ndani ya siku2 zimeisha! hapo bei tuliyokuwa tunauzia tofauti kulingana na mteja anataka mzigo kiasi gani wapo tulikuwa tunauza 470/475/480. hivyo hesabu unakuja kufunga na bei na bei ya 470 kwa mzigo wote fadia nyingine juu yangu.

kumbuka mshahara nalipwa 70k kwa mwezi pamoja nakushika manot yote yale...nilikuwa na jamaa zangu kila weekend nilikuwa nawatoa 30k ama 50
Eeeh ulikua unapiga pesa mkuu 300k kwa mwezi parefu sana
 
Tuendelee EP 07

Nilipokea simu nikatega sikio kwa umakini. Recho " hello vipi". Mimi " Safi, Kuna usalama kweli..tulisha agana mpenzi wangu lakini!". Recho " kwakweli babaa hii dawa imeanza kunipa mawazo...sisikii chochote wakati nilitegemea mpaka saahivi mambo yawe tayari".
Mimi " ulimeza saa ngapi ?".

Alidai alimeza saa mbili usiku lakini sasa inaeelekea saa Saba hajahisi chochote kwa maana ya maumivu ya tumbo la chini au ishara za damu kumtoka. Nikamtuliza pale pamoja na kuwa Sina uzoefu na jambo la utokaji wa mimba na tukakubaliana alale tu tuone kesho itakuaje.

Kesho yake tukaendelea kuwasiliana huku Hali ikiwa vilevile. Toka tumeanza wizi Recho alipunguza kwa sehemu kubwa kunywa hasa Konyagi. Hakuacha kabisa lakini alipunguza, kuna kipindi alikua anaficha chupa kwenye viunga vya maua nje ili nikija nisione na anakula ndizi mbivu kuikata Ile harufu.

Bado niliweza kumgundua lakini kwasababu najua alikua akielekea kwenye uraibu sikumjia juu. Naelewa ingemchukua muda kuacha.

Hii siku ilipita pia pasipo dawa kufanya kazi na hapo tukaanza kushauriana atumie nyingine. Ila kabla ya kufanya hivo tuwasiliane na daktari tuone angeshauri nini. Asubuhi ile kimya, mchana kimya, usiku bado hakuna mabadiliko. Tukaagana saa 3 usiku kila mtu alale salama.

Binafsi ule usiku siku lala kabisa, nilikua kwenye hali ya kukosa amani na usingizi kabisa. Mungu saidia paka kucha. Nikapigia simu mwenyewe, "wewe upo sawa kweli, usiku sijalala kwa amani asee...na vipi bado tuu?!?". Recho " Z shukuru Mungu nimepokea simu yako...Mimi Leo nilikua nakufaaa". Akaendelea "Hivi kwenu huwa hamtoagi mimba eh?". Mimi nipo kimya namsikilizia kwa makini. " Hapa ndio nimemaliza kusafisha nyumba maana nilipakaza damu kila Kona".

Nikamdaka " So unamaanisha tayari!??". Recho " Sasa huelewi nini... ndio dawa imefanya kazi". Mimi " Dah! Anyway pole sana my love, kwahio damu imeacha kutoka au vipi". Recho " baby haiwezi kukata tu mara moja itaenda inapungua mwisho itaacha... ila mh! Ulizia vizuri kwenu, ukoo wenu itakua hamtoagi mimba!...kidogo nife".


Wiki ilikatika bado hajakoma kutoka damu, tukakubaliana aende kwa mtaalam/daktari acheki na asafishe masalia. Ikawa hivo na nafikiri ndani ya wiki mbili mambo yakawa shwari. Sasa likaibuka jambo hapa.

"Hivi mara yako ya mwisho kupima HIV ni lini?" Nikaulizwa swali. Mimi " Sikumbuki lakini jibu rahisi ni kesho twende wote hata maabara tu tukapime." Recho tena " unajua nimekuota vibaya sana leo... Yani Kuna mtu ananiambia huyo kijana unaetembea nae ni muathirika." Akaendelea " sasa na hivi baba ( .) anarudi nimejipata na hofu kweli".

Nikamuangalia kwa hasira kisha nikamwambia " Recho umefikia hatua ya kuniwazia mie nina umeme.... tumelala wote siku ngapi, na katika hizo siku tumetumia kinga mara ngapi?" Nikaendelea "Leo ni mwezi wa ngapi tupo kwenye mahusiano... kama na HIV ingekua hujaona dalili!?!?. Ok kesho mapema sana wote hospital ".

Kama ungeniona navoshout msomaji ungestaajabu. Recho ananizidi miaka 5, yaani ni mkubwa kwangu lakini nilikua kama Mzee wake katika kutoa kauli. Niliongea kiume na tena bila kupepesa macho pembeni wala kutafuna maneno.

Hapa chukua hii. Mwanamke ni mwanamke, hata awe ni Rais wa nchi ni mwanamke. Katika uumbaji mwanamke yupo kutii kile mwanaume utasema/amua juu yake. Ukitaka kuamini hilo mpe order mwanamke ya kufanya kitu kwa sauti ya kurembua huone reaction zake. Na baadae toa order hiohio kwa sauti ya mamlaka yani kiume uone tena reaction.

Hakika utekelezaji wa amri yenye mamlaka ndio utafanyiwa kazi chap pasina mapuuza.

Turudi kwa Recho. Baada ya kuongea vile nikaanza kuombwa samahani. "Basi naomba nisamehe mwanaume wangu. Jamani ndio unanikasikirikia hivo... alaf sijazoe unanikalipia hivi." Akaendelea " au hunipendi, usinigombeze bhana me nitaanza kukuogopa". Basi ili kutoa nyongo vizuri nikapelekwa chumbani. Kimoja tu nikasahau kwani nilikua nashoutia kitu gani.

Katika zile harakati za kuomba kazi maeneo tofauti tofauti kuna kazi moja mkeka ulitika japo ilikua ni nje kidogo ya mkoa na haikua ya kudumu, kama miezi sita tu. Sikua nimwemwambia Recho maana nilitakiwa kureport mwezi uliokua unafata na ndio kipindi hiko hiko mumewe Recho angerejea nchini.

Recho aliniomba kitu tena. Recho " kabla huyu hajaja naomba tujizoeshe mambo mawili." Mimi " enhee!". "Mosi, tupungeze kuwasiliana walau mara mbili tu kwa siku...pili, hii week nianche kabisa usiniguse tena". Kwangu Likija swala la kutomgusa Recho siwazi kingine zaidi ya kuhisia Recho ana mtu mwingine.

Nikamjibu "Kuhusu kuwasiliana nitajitahidi ingawa sina uhakika sana kama ntaweza... lakini kukula mama wangu utanisamehe. Wiki Hapana".

"Z lakini usisahau tunafanya hivi ili tusijestukiwa mapema...sio kwamba tutaachana my love". Akazidi kunisisitiza " tukiendelea kufanya sitaweza kumuigizia...ndio nitaweza siku ya kwanza lakini najua tu mbeleni atajua tu. Em nielewe basi jamani."

Kwasababu sipendi mijadala mirefu nikamwambia poa. Sasa hapa wivu ukaanza kunitesa. Mali sio yangu lakini ndio hivo nimepanda mtumbwi wa vibwengo tayari ntafanyaje. Kweli bhana siku hio pattern ya kuchat ilikua sio nzuri.

Rasmi sasa napiga simu zinaiita tu na hanirudii. Katika sms 10 Moja ndio inajibuwa tena zile 'K' au 'P'. Ajabu nikienda kwake mahaba kama yote ila kwa njia ya simu hapana. Hii ikanitesa kiasi na kufanya nizidi kupata hisia hasi dhidi ya Recho

Hayawi hayawi sasa sasa yamekua, wiki ijayo jamaa kathibitisha atatua katika Ardhi ya bongo. Toka nimeanza story huyu mwamba sijamzungumzia kabisa, ni kwasababu sio kiini cha ujumbe naohitaji uupate kupitia story hii lakini sio mbaya ukamfahamu kwa ufupi.

Jamaa ni mtumishi wa serikali na nafasi yake ni poa sana. Huyu mwamba alienda kujendeleza kielimu nafikiri, kwa bahati nzuri au mbaya nilikutana nae pasipo yeye kunijua na tukasalimiana kabisa. Hapa inahitaji moyo kidogo. Kipindi yupo nje mara kadhaa akiwa anavideo call na babe wake mimi nilikua nipo live. Hapo ndio tuwaogope wanawake.

Nikaoneshwa picha ya risiti ya ticket ya ndege, tarehe inasomeka ni siku tano mbele ndio siku ya safari. Na kweli sijamvua nguo Recho toka siku alioniomba nisifanye hivo.

Usichanganye, toka Recho agundue ana mimba, atoe na kupona ni mwezi sasa unakaribia kuisha. Kwahiyo mpaka jamaa anarudi unakua umetumia ule mwezi mmoja toka amjulishe mkewe kuwa angerudi Tz. Na nilimuweka mara Moja tu.

Sio kwamba nilishindwa kufosi penzi, Hapana. Najua udhaifu wa Recho upo wapi na ningeweza kutumia mwanya huohuo lakini niliona niheshimu tu kile alichoniomba kwani tayari nina jiona nimekua kirusi kuingilia familia ya mtu na bado niendeleze unyama. Hapa niliamua kuwa mpole kwanza.

Sasa silaha yangu kubwa ya mawasiliano iliobaki sio simu tena bali kwenda nyumbani kwa Recho. Mume wake anarudi, simu zangu hazipokelewi, ubwege wa mapenzi umenijaa. Je ntatoboa....
Mapenzi upofu
 
Haka kauzi heading yake nilikuwa sielew,nikawa nakapitiliza tu,kumbe kana hadithi tamu sana hv

Ila huku mwisho umekuwa mjinga sana,kuforce kwenda kwa jamaa wakat unajua jamaa yupo nchini hz ni nyege gani

Niliwah kuwa na mke wa mtu kama huyo,yeye ndo alikuwa ananitafuta wakat jamaa yake yupo,mim sikuwa na muda nae kabisa,hata siku jamaa anaondoka yeye ndo alinitafuta kwa bashasha na nilitaka hata tumalize wiki mbili bila kukulana lakin alishindwa,alitaka tuendeleze chapu
Karibu sana kaka. Mambo mazuri hua hayawekwi wazi sana. Share na wadau kaka.

Kuhusu ubwege wa mapenzi ni kweli, ktk hiki kipindi ninapitia ujinga mkubwa kama sio upofu lakini episodes ijayo nitaibuka shujaa. Karibu.
 
Tuendelee EP 08


Katika kipindi ambacho Z mimi nimekua bwege wa mapenzi ndio Recho anafanikiwa kupunguza kama sio kukata mawasiliano na mimi. Mwanzoni ilinipa shida sana kiasi nikawa nalazimika kwenda kwake kumuona. Ilifika point nikaona haina maana kuwa kila siku niwe nafosi mambo nikaamua kukaza.

Siku akinitafuta haya asiponicheck poa tu. Haikua rahisi lakini niliweza, na hapo nikaanza kuwaza nifufue koloni langu yani Nailah wa chuo.

Ndani ya zile siku tano za 5 bwana mkubwa kurudi kweli nikula msoto kihisia. Siku moja kabla ya jamaa kuja bila kutarajia nakutana na Recho njiani. Kashtuka sana kisha, " heeh! Utaniua bhana kwa presha... mambo". Mimi " Safi, naona hujatarajia kuniona kabisa...hivi haya maisha ndio unapenda sio?". Recho " sio hivo ila nimelazimika kufanya hivi kwajili yetu wote".

"Hivi unadhani Mimi sikumiss...nakumiss lakini najikaza tu". Mimi "hata kama, ndio kunitext au kujibu sms napo ni tatizo". Hatukua na mwisho mzuri wa mazungumzo ila alisisitiza kuwa jamaa yake anarudi kesho yake na nijitahidi ku 'behave'.

Kukubali kuingia kwenye mapenzi na Recho sasa kinanitokea puani. Nilikua nishazoea vyakuchinja sasa hivi vya kunyonga naona ni changamoto.

Nilizoea kujibondea mali kila nilipojisikia sasa hakuna tena. Kusikia sauti yake ya mahaba na maneno yake sasa hakuna tena. Mtu wa kuniuliza kazini leo mambo yalikuaje na umefikiwa wapi lile jambo lako sasa hana time.

Kweli katika mapenzi kinachouma ni mazoea. Narudia kweli nilipata msoto.

Kesho ikafika, Recho akapost status, picha ya mwamba na 'caption' iliosomeka "Welcome back home Daddy, I can't wait" ikasindikizwa na emoji za kopa kopa. Nikaview na sikusema kitu.

Nakiri kuwa ubwege ule niliokuwa nao ulinitesa sana. Ile siku bhana sikulala maana kila nikifumba macho naona jinsi Recho anazungusha kiuno kwa mumewe. Nimesahau kabisa kama mimi nilikua ni mwizi tena deywaka.

Hapa tuongee kitu. Ukitoka na mke wa mtu au mume wa mtu ni vema na wewe uwe mke wa mtu au mume wa mtu ili mzani ubalance. Sichochei watu kuchepuka ila kwa muktadha wa hisia na mawazo niliyokua nayo Ile siku nafikiri ningekua na mtu usiku ule ningepata liwazo. Ndugu zangu wa maudhui lichukulieni hili chanya zaidi.

Paka kucha nikiwa kwenye dimbwi zito la mawazo kana kwamba nimefumania mke wangu. Mara paa sms kutoka kwa Recho, " Good morning, naamini uko salama.. Mimi pia". Ikamalizika na neno 'USIJIBU' mwishoni.

Wadau mapenzi shikamo. Baada ya kusoma Ile sms nilijisikia faraja, nikajiwazia kumbe nakumbukwa. Yani kule kuumia moyo na kukosa raha kukabadilishwa na sms moja tu.

Mishale ya saa 4 asubuhi akanipigia. Chap nikapokea, " mambo Z..najua umekasirika". Nikamjibu " Niko poa usijali ila dah umejua kuninyoosha...siku zote hizo leo ndio unanipigia?". Recho " sorry bhana lakini unajua kwanini nilikua nafanya vile... kwanza hapa yupo anaoga ndio nimepata chance". Mimi kusikia vile basi nikazidi jifariji yes bado napendwa.

Wakati nataka kuendeleza maongezi Recho kwa kunong'ona akaniwai "Bye badae, please usinipigie wala sms". Simu ikakatika .

Muda wa kureport kwenye kile kibarua ikafika. Niliona niafadhali niondoke tu eneo lile ili nisimuone Recho maana sasahivi Mimi ndio imekua kama nagongewa mke wangu. Sikuona ni vyema niondoke bila kumjulisha, jioni yake nikapost status huku niki 'hide' all contacts except Recho yaani aione Recho pekee.

Nikaandika ujumbe wangu kuwa kesho ningeondoka nje kidogo ya mkoa kwajili ya kazi mpya na ningelitumia muda gani huko.

Najua hapo nimekupa njia mbadala ya kuwasiliana na mchepuko wako. Hahah! Ok ishi nayo. Recho aliview Ile status mishale kama ya saa tano usiku na hakujibu chochote. Asubuhi nipo safarini akanipigia, " wewe mbona ghafla hivo... na mbona hukunambia mapema". Mimi " nakwambiaje wakati sikupati kwa wakati..ipo hivo na nipo safarini sasa". Recho " sawa kwasababu ni jambo la heri sawa nimekuelewa. Ila ukipata kadem nisijue".

Mimi " fresh ila duh nimeshakumiss kinoma". Recho " mh! jamani I know my love ila vumilia kidogo, huyu week ijayo anaweza toka kidogo". Aisee wanawake watatuua. Nikasema poa yani akitoa tu kiatu chake Mimi natia ndala zangu.

Kuanzia hapo status ikawa means ya mawasiliano. Kwakweli ilifanya kazi kubwa kwa usiri mkubwa. Najua jamaa akili ya kuview status kwenye simu ya mke wake anatolea wapi. Naona na Recho aliielewa maana siku moja alisema. " wewe ni jambazi shindikanaa".

Ndugu msomaji uwe makini na si shauri uitumie na wewe maana si ajabu wewe na mkeo wote mnasoma Uzi huu.

Kweli week ikapita, Mimi wa kwanza kuulizia kama jamaa yupo. Nikaambiwa alihairisha kusafiri ila muda wowote atatoka. Sasa hapa nipo mkoani kikazi lakini Recho ndio kateka akili yangu.

Nafikiri hii ni kwasababu ya yeye kuhusika moja kwa moja kwenye upigaji wa hatua kwa maana ya kazi.

Ewe mwanamke chukua kitu hapo, sio lazima niseme uwe na kitu cha ziada kwa mmeo mbali na sex. Kuwa na kitu extra Inasaidia kuchukua nafasi nafsini kwa mtu.

Z Sikua na videmu wala nini. Baada ya familia yangu aliekua anafata ni Recho bila kuji ni mali ya wizi....
Kwa miaka hii ni 2% tu ya wanawake kama Recho wasiowazia hela
 
Tuendelee EP 09


Jana nilimalizia kwa kushauri, katika mapenzi mwanamke jitahidi uwe na kitu cha ziada mbali na sex ili uweze kuwin moyo wa mwanaume. Hii ni dhahiri mimi nikiwa mfano hai.


Haikutosha tu kuchezea shanga moja katika kiuno cha Recho, au kusikia na kusoma maneno ya mahaba kutoka kwake kunifanya niwe bwege na ninase mtegoni bali Recho kuhusika moja kwa moja kwenye harakati zangu za kujinasua kimaisha. Tuendelee.


Baada ya kuambiwa pacha wangu yani jamaa angetoka muda wowote kutokea siku hio nikawa napost status kila siku kuulizia. Ndani ya siku tatu toka nianze kuulizia sikuwa najibiwa. Nikiangalia kama ameview status nakuta hajaview. Nikirejea kwenye 'last seen' yake naona alikua online. Kichwa kinazidi kuniuma.


Kwanini Recho ananifanyia maksudi. Nikasema sasa ni muda nijue hatima yangu kwake, maana naona hizi ni dharau zilizojificha kwenye kichaka cha 'tutastukiwa'. Kesho yake mchana nikampigia simu, ikaita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa.

Recho " Haloo... nimeona namba Yako nakutumia pesa yako muda si mrefu". Mimi "Hello Recho..Hello!!". Recho akarudia maneno yake ya awali kisha akamalizia kwa ukali "Heh! wewe si nimekwambia nakutumia pesa yako... alaf acha kunipigia pigia simu." Akakata simu.


Wakati wote huo anaongea mimi kimya nikiwa najiuliza. Kwani imekuaje nimekusudia kumpigia Recho badala yake nakosea namba. Mh! Lakini hapana ni yeye. Mbona jina kwenye simu limetokea vile nilivyo msave.


Baada ya Recho kukata simu nikawasha data tena na kupost status kuuliza imekuaje ananiongelesha mambo ya pesa na hajanipa nafasi kunisikiliza. Vilevile haikuwa 'viewed'. Ndani ya dakika 10 akanipigia. " umefanya nini...tulikubaliana nini. Si tulikubaliana tuwasiliane kule WhatsApp?". Mimi "Hivi unajisikia wewe.. we una muda gani hu'view' status zangu". Nikaendelea "tangu juzi nakutafuta na hunirudii".


Recho " Yani umeshindwa hata kujiongeza, me nakwepesha mada badala ukate simu unaendelea kuongea... yani hata hujajiuliza kwanini nilikua nakukalipia...kwani niilishawai kuuongelesha hivo?". " Ndio ujue jamaa bado yupo tena yeye ndio aliniita nije nipokee simu". Mimi "Ok sasa imekuaje umeweza kunipigia kama yupo?. Recho "nimeaga tu naenda dukani ingawa nahisi yupo nyuma ananifatilia".


Mimi " poa, haya kwanini hu'view' status zangu". Recho aliniambia kuwa itakua ali 'mute' status zangu bila kujua na aliahidi angeweka mambo sawa. Tukaagana huku nikasisitiza kichupa kimejaa. "Vumilia tu hata mimi nimekumiss" ndio lilikua neno la kwaheri kutoka kwa Recho.


Ukisikia mapenzi uchizi, upofu, kikohozi, hata wewe msomaji wangu ukitaka ongezea lako mathalani mapenzi ni Lipuli Fc ni sawa tu. Ndio ilivokuwa baada ya maongezi yangu na Recho.


Kesho yake niliomba off kazini na wakanielewa. Nilirudi home pasipo kumjulisha Recho. Kituo changu cha kazi ilikua ni nje kidogo ya mkoa kwahivo niliomba siku mbili. Kinacho nirudisha home sio kuwamiss wazazi au family members hapana, ni Recho. Ndio maana mpenzi msomaji nimekwambia mapenzi yape jina lolote utakaloona linakufaa. Mimi nimechagua mapenzi ni upofu. Huoni unachokifanya mpaka uambiwe na wanao ona.


Baada ya kufika home jioni nikapost. " Nimerudi home one time, Fanya unitumie picha yako nikuone". Akaview chap na akanijibu. "Umerudi!? kwema?!?" ujumbe uliambatana na picha yake.
Mimi "tutaongea kesho kama utapata time".
Recho " Poa, na yeye ametoka ila sijui kama atarudi au atalala huko maana naye haelewekii".


Mimi "kwani kaenda wapi". Recho " Kaitwa makao makuu ghafla sasa sielewi kuna nini na sijui kama atarudi". Alivosema vile niikajua ni mkoa wa jirani tu maana ndio ofisi kuu za mkuu wa kaya zilipo.


Nikamwambia anipigie simu baadae tuongee vizuri. Alifanya hivo na kidogo lile gubu likapoa kiasi. Nikamchana nimerudi kwajili yake na nilikua tayari kufanya chochote ili Mradi nimtie machoni.


Hapo nafikiri unaendelea kunielewa ndugu msomaji kwanini nilisema mapenzi ni upofu. Naweka rehani usalama wangu kwajili ya mtu aliejipata kimaisha. Nasahau kabisa kuna wazazi, ndugu na marafiki wanatarajia kuuendelea kuniona na kufurahi pamoja nami.

Mimi namuona Recho tu. Siwazi kabisa kama kuna mafuta ya nazi, KY na smartphone zinazochukua, kutunza na kusambaza kumbukumbu ndani ya dakika moja.


Kulivopambazuka mapema sana nikamuuliza kama jamaa alirudi na kudai hapana.
Kwa ujinga wangu nikajiona nimepoteza nafasi Jana. What a clear chance. Lakini kuna kitu nilikua najiuliza kuhusu Recho. Nini kinaendelea kichwani/moyoni mwake. Nikajisemea 'anyways' wacha nifosi nibutue kwa mara ya mwisho then ni 'quit'.


Tukakubaliana sikuhio kama jamaa hatarudi basi usiku niende ikiwezekana tuwe na mkesha wa maombi. Kweli saa 12 jioni inafika report inasoma bado bwana mkubwa hajarudi. Saa mbili usiku bado clear. Nikamuuliza Recho "kwanini unsimuulize kama anarudi au lah!". Recho " Z naanzaje...atanichukuliaje... em imagine ni wewe mkewe anakuuliza hivo". Nikamwambia ok sawa itakavokua sawa.


Home nimeshawapanga kuwa nitaondoka saa tatu kuna workmates wangenipitia na usafiri kurejea kazini.
Mpaka saa tano bado nipo home nazuga na sababu kibao. Kwa Recho bado kimya na huku moja haikai mbili haikai.

Nikampigia simu, " Ei vipi mbona kimya hunipendi feedback". Recho "Nilikua naongea nae, anasema anatafuta gari ila akikosa atalala hatokuja". Mimi "sasa si nije tu mamaa.. kwanza sahivi inaenda saa sita gari gani atapata".

Mama wa watu akaona isiwe kesi. " Z njoo ila kwakweli Sina uhakika sana na usalama wetu"..........







Last but not Least.
Mpenzi msomaji wa Uzi wangu huu. Ninayo furaha kukutakia wakati mwema katika sikukuu hizi ( Christmas and Happy New year). Naamini lugha nayo tumia inakupa picha halisi ya Nini kinatokea baina yangu Recho. Sio ya matusi. Tutaendelea baada ya kesho yaani Christmas. Ahsante!
Daah...! Ila kwa kweli umezingua. Ulichotaka mpaka ashtukiwe. Mtu kakuambia,eti hajaview status? Hilo tu ndio uamue kumlipua mwenzio?. Halafu amecheza trick kukujibu hela yako nakutumia,bado umeng'ang'ana tu? Mbona simple tu mtu unaeelewa kinachoendelea upande wa pili. Umeshindwa kuvumilia kweli muda mfupi tu? Au ni uelewa tu?. Recho alikuzidi sana akili. Wewe akili imemezwa na mapenzi tu mpaka umefikia hujali ustaarabu mwingine.
 
Daah...! Ila kwa kweli umezingua. Ulichotaka mpaka ashtukiwe. Mtu kakuambia,eti hajaview status? Hilo tu ndio uamue kumlipua mwenzio?. Halafu amecheza trick kukujibu hela yako nakutumia,bado umeng'ang'ana tu? Mbona simple tu mtu unaeelewa kinachoendelea upande wa pili. Umeshindwa kuvumilia kweli muda mfupi tu? Au ni uelewa tu?. Recho alikuzidi sana akili. Wewe akili imemezwa na mapenzi tu mpaka umefikia hujali ustaarabu mwingine.
Umenielewa vizuri sana. Nilikua sioni chochote kana kwamba nimeshaoa. Tuone muendelezo Hali ipoje. Karibu sana.
 
Back
Top Bottom