Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Hivi ndivyo tunavocheat, palipo na viatu vya muwewe kuna ndala zangu

Mwanaume ni msimamo ukirudisha moyo wako utakuwa umeondoa dhana ya msimamo wako. Shikilia hapo hapo mkuu

Anyway, tupo na wewe mpaka na wewe umpende mwanamke naye akuzimie fegi kama ulivyomfanyia huyo. "What goes Around, comes Around"
Mkuu msimamo wangu haujawahi kuyumbishwa na yeyote kikubwa niwe sawa na simwonei mtu,

😂😂😂 Swala la kupenda kisha nizimiwe fegi fresh tu kama nimemkosea kosa lisiloruhusu kuendelea na hayo mahusiano yetu
 
Tuendelee EP 09


Jana nilimalizia kwa kushauri, katika mapenzi mwanamke jitahidi uwe na kitu cha ziada mbali na sex ili uweze kuwin moyo wa mwanaume. Hii ni dhahiri mimi nikiwa mfano hai.


Haikutosha tu kuchezea shanga moja katika kiuno cha Recho, au kusikia na kusoma maneno ya mahaba kutoka kwake kunifanya niwe bwege na ninase mtegoni bali Recho kuhusika moja kwa moja kwenye harakati zangu za kujinasua kimaisha. Tuendelee.


Baada ya kuambiwa pacha wangu yani jamaa angetoka muda wowote kutokea siku hio nikawa napost status kila siku kuulizia. Ndani ya siku tatu toka nianze kuulizia sikuwa najibiwa. Nikiangalia kama ameview status nakuta hajaview. Nikirejea kwenye 'last seen' yake naona alikua online. Kichwa kinazidi kuniuma.


Kwanini Recho ananifanyia maksudi. Nikasema sasa ni muda nijue hatima yangu kwake, maana naona hizi ni dharau zilizojificha kwenye kichaka cha 'tutastukiwa'. Kesho yake mchana nikampigia simu, ikaita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa.

Recho " Haloo... nimeona namba Yako nakutumia pesa yako muda si mrefu". Mimi "Hello Recho..Hello!!". Recho akarudia maneno yake ya awali kisha akamalizia kwa ukali "Heh! wewe si nimekwambia nakutumia pesa yako... alaf acha kunipigia pigia simu." Akakata simu.


Wakati wote huo anaongea mimi kimya nikiwa najiuliza. Kwani imekuaje nimekusudia kumpigia Recho badala yake nakosea namba. Mh! Lakini hapana ni yeye. Mbona jina kwenye simu limetokea vile nilivyo msave.


Baada ya Recho kukata simu nikawasha data tena na kupost status kuuliza imekuaje ananiongelesha mambo ya pesa na hajanipa nafasi kunisikiliza. Vilevile haikuwa 'viewed'. Ndani ya dakika 10 akanipigia. " umefanya nini...tulikubaliana nini. Si tulikubaliana tuwasiliane kule WhatsApp?". Mimi "Hivi unajisikia wewe.. we una muda gani hu'view' status zangu". Nikaendelea "tangu juzi nakutafuta na hunirudii".


Recho " Yani umeshindwa hata kujiongeza, me nakwepesha mada badala ukate simu unaendelea kuongea... yani hata hujajiuliza kwanini nilikua nakukalipia...kwani niilishawai kuuongelesha hivo?". " Ndio ujue jamaa bado yupo tena yeye ndio aliniita nije nipokee simu". Mimi "Ok sasa imekuaje umeweza kunipigia kama yupo?. Recho "nimeaga tu naenda dukani ingawa nahisi yupo nyuma ananifatilia".


Mimi " poa, haya kwanini hu'view' status zangu". Recho aliniambia kuwa itakua ali 'mute' status zangu bila kujua na aliahidi angeweka mambo sawa. Tukaagana huku nikasisitiza kichupa kimejaa. "Vumilia tu hata mimi nimekumiss" ndio lilikua neno la kwaheri kutoka kwa Recho.


Ukisikia mapenzi uchizi, upofu, kikohozi, hata wewe msomaji wangu ukitaka ongezea lako mathalani mapenzi ni Lipuli Fc ni sawa tu. Ndio ilivokuwa baada ya maongezi yangu na Recho.


Kesho yake niliomba off kazini na wakanielewa. Nilirudi home pasipo kumjulisha Recho. Kituo changu cha kazi ilikua ni nje kidogo ya mkoa kwahivo niliomba siku mbili. Kinacho nirudisha home sio kuwamiss wazazi au family members hapana, ni Recho. Ndio maana mpenzi msomaji nimekwambia mapenzi yape jina lolote utakaloona linakufaa. Mimi nimechagua mapenzi ni upofu. Huoni unachokifanya mpaka uambiwe na wanao ona.


Baada ya kufika home jioni nikapost. " Nimerudi home one time, Fanya unitumie picha yako nikuone". Akaview chap na akanijibu. "Umerudi!? kwema?!?" ujumbe uliambatana na picha yake.
Mimi "tutaongea kesho kama utapata time".
Recho " Poa, na yeye ametoka ila sijui kama atarudi au atalala huko maana naye haelewekii".


Mimi "kwani kaenda wapi". Recho " Kaitwa makao makuu ghafla sasa sielewi kuna nini na sijui kama atarudi". Alivosema vile niikajua ni mkoa wa jirani tu maana ndio ofisi kuu za mkuu wa kaya zilipo.


Nikamwambia anipigie simu baadae tuongee vizuri. Alifanya hivo na kidogo lile gubu likapoa kiasi. Nikamchana nimerudi kwajili yake na nilikua tayari kufanya chochote ili Mradi nimtie machoni.


Hapo nafikiri unaendelea kunielewa ndugu msomaji kwanini nilisema mapenzi ni upofu. Naweka rehani usalama wangu kwajili ya mtu aliejipata kimaisha. Nasahau kabisa kuna wazazi, ndugu na marafiki wanatarajia kuuendelea kuniona na kufurahi pamoja nami.

Mimi namuona Recho tu. Siwazi kabisa kama kuna mafuta ya nazi, KY na smartphone zinazochukua, kutunza na kusambaza kumbukumbu ndani ya dakika moja.


Kulivopambazuka mapema sana nikamuuliza kama jamaa alirudi na kudai hapana.
Kwa ujinga wangu nikajiona nimepoteza nafasi Jana. What a clear chance. Lakini kuna kitu nilikua najiuliza kuhusu Recho. Nini kinaendelea kichwani/moyoni mwake. Nikajisemea 'anyways' wacha nifosi nibutue kwa mara ya mwisho then ni 'quit'.


Tukakubaliana sikuhio kama jamaa hatarudi basi usiku niende ikiwezekana tuwe na mkesha wa maombi. Kweli saa 12 jioni inafika report inasoma bado bwana mkubwa hajarudi. Saa mbili usiku bado clear. Nikamuuliza Recho "kwanini unsimuulize kama anarudi au lah!". Recho " Z naanzaje...atanichukuliaje... em imagine ni wewe mkewe anakuuliza hivo". Nikamwambia ok sawa itakavokua sawa.


Home nimeshawapanga kuwa nitaondoka saa tatu kuna workmates wangenipitia na usafiri kurejea kazini.
Mpaka saa tano bado nipo home nazuga na sababu kibao. Kwa Recho bado kimya na huku moja haikai mbili haikai.

Nikampigia simu, " Ei vipi mbona kimya hunipendi feedback". Recho "Nilikua naongea nae, anasema anatafuta gari ila akikosa atalala hatokuja". Mimi "sasa si nije tu mamaa.. kwanza sahivi inaenda saa sita gari gani atapata".

Mama wa watu akaona isiwe kesi. " Z njoo ila kwakweli Sina uhakika sana na usalama wetu"..........







Last but not Least.
Mpenzi msomaji wa Uzi wangu huu. Ninayo furaha kukutakia wakati mwema katika sikukuu hizi ( Christmas and Happy New year). Naamini lugha nayo tumia inakupa picha halisi ya Nini kinatokea baina yangu Recho. Sio ya matusi. Tutaendelea baada ya kesho yaani Christmas. Ahsante!
 
Back
Top Bottom